Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Huelewi kitu.China imejaa wawekezaji lakini katiba haina uhuru wa habari wala wa vyama vya siasa.
Hoja kwamba wawekezaji hawawezi kuja kisa hakuna uhuru wa habari ama vyama vya siasa ni hoja ya kitaahira kabisa na inasemwa na watu wasio na akili kabisa.
Mimi nimekuwa nikifanya na multinational companies. Na moja ya shughuli zangu ilikuwa kushauri kamouni, nchi za kuwekeza. Kuna vigezo vingi lakini kimojawapo ni utawala wa sheria.
China, mfumo wa uongozi hauna demokrasia za kimagharibi lakini ndani ya Serikali na chama cha Kikomunisti, kuna utiifu wa hali ya juu katika kufuata sheria.
Sheria yao ya uwekezaji ni madhubuti hasa. Kiongozi mkuu wa nchi hana uwezo wa kubadilisha hata aya moja. Ili kubadilisha kitu, ni lazima mchakato wake upitie hatua nyingi.
Tanzania ni nchi holela. Sheria inaweza kuwa inatoa haki fulani, lakini Rais anajiropokea anachokitaka, na hakuna wa kuhoji. Nchi kama hiyo, mwekezaji makini hawezi kuwekeza. Unawekeza kwa kuangalia sheria, halafu Rais kwa kauli ya dakika moja tu anabadilisha kila kitu, na hakuna wa kuhoji. Nchi ya namna ulinachochea uchuuzi na siyo uwekezaji.