BIN BOR
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 1,013
- 407
Chupi mpya. Tako lilelile
Tulifahamu tangu awali kwamba ccm ni ile ile , ila kuna tofauti kidogo kati ya viongozi wanaopewa Mamlaka na Chama hicho , kiongozi mwenye exposure hutofautiana kidogo uungwana na kiongozi wa kutoka porini , tofauti ipo ya namna ya kuhandle issues , kujua wapi aongee nini na wapi atishie watu , badala labda ya kukamata mwingine aweza kuonya tu na mambo yakasonga.
Lakini kwa kiasi kikubwa kwenye masuala ya haki za kikatiba ccm bado ni moja , hawataki usawa hata chembe , viongozi wote wa ccm hawataki katiba itakayoleta usawa ndani ya nchi wala hawataki Tume huru ya uchaguzi , pamoja na mama kuondoa baadhi ya uchafu uliofanywa na awamu iliyopita , ambao kwa kiasi kikubwa uliidhalilisha nchi na kuitia aibu duniani , lakini kimsingi hana tofauti kubwa na viongozi wengine wa ccm waliomtangulia .
Labda kwa kuwakumbusha tu ni kwamba Mama ni miongoni mwa watu wasiopenda kusikia habari ya serikali 3 , huyu alikuwa makamu Mwenyekiti wa bunge la Katiba , aliyesaidia sana kuinyofoa katiba yote ya Warioba na kupachika madudu waliyoyataka , Mwenyekiti alikuwa Samuel Sitta , kwahiyo huyu hakuwahi kuwa mwema kwa Taifa , bali ni mtu anayeuma na kupuliza , inawezekana katika uongozi wake akawa ana nafuu kuliko yule mkomoa watu , lakini kuhusu Katiba mpya tuendelee tu kupambana naye kama tulivyopambana na wengine .
Huwezi kushawishi wawekezaji wakubwa ikiwa hauna mifumo imara ya kisheria , mifumo hii inawekwa ndani ya Katiba , Katiba ya sasa ya Tanzania inamwezesha rais wake kufanya chochote bila kuhojiwa , ni mwekezaji gani mwenye akili timamu awezaye kuja kwenye nchi ya hivyo ?
Inasikitisha tu kwamba imani ndogo aliyowapa Watanzania kwa siku 100 za mwanzo ameiteketeza kwa kauli ya dakika 1 tu ya KUENDELEA KUVUNJA KATIBA ALIYOAPA KUILINDA , huku akiwa kashika quran Tukufu mkono wa kulia .