Matunda ya Diaspora: Namna Wanawake Diaspora 2 walivyoweza kumuweka Kagame na Rwanda kwenye kona. Tanzania tuna la kujifunza

Kwamba mabeberu wameamua kuweka vikwazo baada ya kushawishiwa na hao wanawake!?..tumia fuvu lako vizuri
Kama unafikiri kuna jambo linatokea bila jitihada na kuchukua hatua basi wewe ndo unapaswa kutumia fuvu lako vizuri.

Mwenzako Kagame kamuondoa Balozi wake wa Umoja wa Mataifa huko kutokana na kushindwa kuhimili mishindo ya hao unaosema Wanawake wawili.

Kama Kagame kaona shughuli yao ilivyokuwa nzito na kachukua uamuzi we kapuku uliyesoma shule za kata ni nani hadi ukosoe kazi nzuri iliyofanywa na hao wanawake wawili?
 
Wishful thinking, PK anauwezo wa kuusoma mchezo mara milioni zaidi mabandiko yako hapa janvini. He is there to stay.
It's about time na sisi tuweke watu competent kwenye sehemu nyeti hasa TISS na Jeshini, tuache utaratibu wa kuweka watu kwa vimemo vya kujuana na kuokota kila chawa aliye UVCCM. Watu makini tunao lakini hatuwapi nafasi, uchawa imekuwa ni qualification muhimu sana Bongo.
 
Nakubaliana na wewe. Tanzania tuna watu makini ila hawapati nafasi kutokana na mfumo mbovu wa CCM.

Dawa pekee ya kuondokana na hili ni Katiba Mpya iliyo mpya inayosimika mifumo imara.
 
Nakubaliana na wewe. Tanzania tuna watu makini ila hawapati nafasi kutokana na mfumo mbovu wa CCM.

Dawa pekee ya kuondokana na hili ni Katiba Mpya iliyo mpya inayosimika mifumo imara.
 
Madini yetu wenyewe yanachotwa kiholela na nchi haifaidiki, hayo ya DRC hata yaachwe bila mwenyewe hatuyawezi sana sana tutabembeleza mabeberu waje wayachote na viongozi wachache wapewe ganji kwa kusaini kuruhusu wizi wa mchana kweupe tuendelee.
 
Huo mwingine mjimama haswa, km Chakachaka, Tshala Muana.
 
Kwahiyo unashauri tuwatumie Diaspora kuwekewa vikwazo? Huna akili kabisa.
 
Diaspora wengi si 'chawa' wa bibi yenu huyo ndiyo maana wanapigwa vita, Bongo hawataki mtu anayejitambua.
 
Dah! sisi tumebaki na walamba asali na waimba pambio wasio na utashi wa kulisaidia taifa kwenye diplomasia na mahusiano ya kimataifa.
R.I.P malengend wote wa diplomasia Sir Mahiga et al...
 
Kama muafrika anayelipenda bara lake hii comment yako imeniliza
Jambazi akija kwako heri mpe mali maana hata ukibaki nayo haikusaidii uhai ni bora.
Kwan wacongoman wanakula cobalt na cotan haya madini yanaenda kwa viwanda vya magari ya umeme kwenye Tesla, space x,nk sisi ni walinzi tu wa mali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…