Mauaji Moshi: RC Mghwira asema utaratibu wa kukanyaga mafuta uliandaliwa vizuri ila vibaka walivamia kutokea nje na kusababisha maafa

In Christianity neither morality nor religion come into contact with reality at any point-Friedrich Nietzsche
 
Ni ushirikina kuwaambia watu wakanyage mafuta wakati tuna Jina la Yesu linalopita majina yote

Sent using Jamii Forums mobile app
Marko 6
Β―Β―Β―Β―Β―Β―Β―Β―Β―Β―
⁷ Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;

…
ΒΉΒ² Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu.
ΒΉΒ³ Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza.


Nimekuwekea andiko hilo ili uchunge kauli zako. Usikaririshwe, soma maandiko. Habari za Mwamposa baadaye kwanza, tuanzie hapo.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Ndio maana watu wanahusisha hili janga na mpango wa serikali kuua soo ya makonda na USA
Hawa watakuwa wachawi haswa wenye mawazo mfu hivi

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Ni kweli inaumiza sana,lakini RC kaongea ukweli tuache mihemuko, tupunguze chuki haya mambo yanatokea Nigeria, South Africa n.k mambo ya iman na Uhuru wa watu wa kuabudu uheshimike
 
Unachukua mstari mmoja halafu unafanya kuwa ndio msingi wa mafundisho. Kuna tofauti kati ya kupaka mafuta na kukanyaga mafuta.

Je waliokuja kukanyaga mafuta ni wagonjwa? Wagonjwa gani wanakanyagana mpaka wanakufa?

Halafu mafuta ni symbol ya Roho Mtakatifu ambaye already tunaye tangu siku ya Pentekoste, huu mbadala wa Roho Mtakatifu una umuhimu gani wakati Mungu Roho Mtakatifu yupo duniani leo?

Hili la watu kukanyagana kwenye ibada mpaka wanakufa ni jambo linalotia mashaka sana, yaani Mungu wa Mbinguni Yehova anashuhudia watu wanakufa kwenye ibada yake???? I don't take it in...honestly!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli lonatia mashaka. Lakini nimekwambia ya Mwamposa kando kwanza nikuone uelewa wako. Hayo ni mafungu yanayotumiwa zaidi. Nikusaidie tu kunielewa, mimi sijengi mafundisho kwa mstari mmoja. Nasoma sura nzima na kuoanisha na sura nyingine.

Hayo mafutavhayakuwa yakipakwa wagonjwa tu, labda husomi biblia. Lakini pia katika zama za agano jipya baada ya Kristo kudhihirishwa na kutwaa MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI, hatuhitaji tena kuwa na religious gudgets ili kumwona. Ndiye aliyetuagiza kwenda ulimwenguni kote KUIHUBIRI INJILI. Kwa sababu neno MASIHI lina maana ya MPAKWA MAFUTA (The annointed one), Kristo akiwa ndani yako una haja gani na mafuta mengine? Unataka ukanyage mafuta ili upate nini? Huoni kama huko ni kumkana yule aliye ndani yako?

Kumbe tukikaa ndani ya Kristo (Neno) naye akikaa ndani yetu, na tuombe lolote kwa jina lake na Baba yetu aliye mbinguni atafanya ili FURAHA YETU ITIMIZWE. Tatizo lilishasemwa na Kristo, hatujui kuomba itupasavyo, ndipo hapo Roho Mtakatifu anapoingilia kati, sio MAFUTA YA UPAKO. Tukiomba V8 Roho ansema mwanangu anahitaji nauli ya kumfikisha kazini, sasa sisi tunawaka hasira. Tukiomba nyumba Yeye anatuwekea mazingira ya kupata pesa ya kutosha kulipa kodi na kusaza huku tukijipanga zaidi. Mioyo yetu inajaa jazba sana, tunaanza kuulizana je, katika Israeli hakuna mungu mwingine ambaye hujibu papo kwa hapo? Ndipo wenye maarifa huujibu, yuko Mungu wa Mwamposa, yeye hahitaji mambo mengi na masharti yake ni mepesi tu. KANYAGA MAFUTA!!

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Kumbe mlikuwa mnatuandaa kisaikolojia ili muweze kumuachie Mwamposa kwa kisingizio cha dhamana? Hongera mama mghwira kwa kuungana na mashetani
 
waziri wa mambo ya ndani...kaangushiwa zigo la kinyesi πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ...hili taifa matukio yake yanachekesha kuliko hata clip za charlie chaplin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…