Mauaji yanayoongezeka yatokanayo na wivu wa mapenzi nini kifanyike?

Mauaji yanayoongezeka yatokanayo na wivu wa mapenzi nini kifanyike?

Jay El

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2020
Posts
459
Reaction score
728
Wakulungwa wa Jamii forums, wasalaam.

Kama tujuavyo hizi topic za mauaji kwa jina la wivu wa mapenz naona zimekua too much sasa Dodoma week hii nadhani kama sikosei yalikua matatu Mbeya napo mtu kaamua kunywesha sumu familia nzima.

Mimi kwa mtazamo wangu naona panatakiwa kufanyika jambo kwa kutumia wataalamu wa saikolojia wakishirikiana na serikali au basi ndoa ziruhusiwe kuwa za mikataba mana hatuwezi kuteketeza maelfu kisa vikojoleo tu.

Na kwa asilimia kubwa wanaume ndio tunashindwa kabisa kuhandle hizi stress. La pili family skills topic za namna ya kuhandle stress za kifamilia zingeingizwa kwenye mitaala ya vyuo, sekondari na shule za primary kwa msisitizo mkubwa.

Na nasisitiza hili kwa sababu mauaji yanayotojea sio baina ya walio kwenye ndoa rasmi tu bali hata kwenye mahusiano ya mapenzi kawaida kama uchumba na mengineyo. Mfano tukio la Dodoma kwa wale wanafunzi hawakua kwenye ndoa.

Wasomi wetu na maproffesor sijui wanawaza nini juu ya hili. Kulingana na taarifa za jeshi la polisi mauaji haya yanaongezeka ila Spika wa bunge anashauri yasitangazwe sasa sijui anatumia akili gani.

Badala atafute solution yeye anaminya uhuru wa habar, nilikua namuheshimu kulingana na elimu yake ya udaktari wa sheria ila kwa sasa napatwa maswali juu yake. Wadau wafanyie utafiti haya mambo waje na majibu sio kuzinyamazia hizi taarifa kama burudani za mziki.

Humu kuna great thinker naamini na wao watakua na mawazo makubwa pia. Natanguliza samahani ikiwa uandishi huu utawakwaza tujadili mada ila kuhusu mimi nisameheni. Naomba kuwasilisha. Asanteni
 
Mmh.. si ndio tutakua na taifa la watu wa ajabu kabisa mkuu? Mana bila taasis ya family tutakua na vijana wa hovyo zaid na zaid@Bufa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wakulungwa wa jamii forum wasalaam.
Kama tujuavyo hizi topic za mauaji kwa jina la wivu wa mapenz naona zimekua too much sasa Dodoma week hii nadhani kama sikosei yalikua matatu Mbeya napo mtu kaamua kunywesha sumu familia nzima. Mimi kwa mtazamo wangu naona
Hayo ni matokeo ya kampeni za 50/50, mwanamke kaaminishwa kushindana na mwanaume katika kila nyanja ndo u-superwoman, hawa fermists wanaopewa airtime katika media ni virusi hatari sana kwa ustawi wa jamii zetu za kibantu.

Nakumbuka mara yangu ya kwanza na ya mwisho kuangalia kipindi cha wanawake live ilitokea tu by coincidence nilienda kumtembelea ndugu yangu kwa kweli mawaidha aliyokua anayatoa yule joyce kiria nikasema huyu dada ni kansa hatari sana
 
Hayo ni matokeo ya kampeni za 50/50, mwanamke kaaminishwa kushindana na mwanaume katika kila nyanja ndo u-superwoman, hawa fermists wanaopewa airtime katika media ni virusi hatari sana kwa ustawi wa jamii zetu za kibantu., nakumbuka mara yangu ya kwanza na ya mwisho kuangalia kipindi cha wanawake live ilitokea tu by coincidence nilienda kumtembelea ndugu yangu kwa kweli mawaidha aliyokua anayatoa yule joyce kiria nikasema huyu dada ni kansa hatari sana
Nakubaliana na wewe kwa kiasi mkuu ila feminism ndio imetamalaki hapa duniani kwa sasa je tutakua salama kama taifa?lait tungekua hatujaijaribu.

Sasa nyumba nyeupe ndio wenyewe wapo na anakuambia wewe mchango wako ni mbegu tu mengine nafanya mwenyewe..

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wewe imagine mke anakucheat wakati unampiga mashine vizuri anakojoa ,mnakula na kunywa wote huku mnacheka ,mna watoto wazuri pamoja ,umempaa gari la kumsaidia mizunguko yake ,umewahi kumsamehe makosa makubwa makubwa nk nk- yaani kwa kifupi she cheated you at the best moment of your life.

RIP my friend Cosma
Kama mwanaume inauma sana lakini lait ukajipa nafas ya kuangalia pro na cons naamini utaacha vitu vinatafutwa watu wanatuacha na maisha yanaendelea imagine unafiwa na unaempenda sana unaumia unamuachia Mungu unasonga mbele hapo angeacha hai ata watoto..

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hii inatokana na kuikimbia asili, ki asili mwanaume anatakiwa kuwa/kuoa mwanamke zaidi ya mmoja, kwa akili za wanawake wakishajua wako zaidi ya mmoja kwa mwanaume mmoja wanaanza kupambana wao kwa wao, watapambana kukuonyesha mapenzi na kutimiza majukumu yao, na kila mmoja atakua na wivu dhidi ya mwenzie, hii itakusaidia kutokuwekeza hisia zako sehemu moja, wazee wa zamani walisema Usiweke mayai yote kwenye kapu moja.
 
Elimu ya mapenzi ifundishwe mashuleni, wengi udhani wanaishi na malaika
 
Tuendelee na 50/50 inayohamasihwa na wale weny vingereza vingi na elimu za nje.
 
Hii inatokana na kuikimbia asili, ki asili mwanaume anatakiwa kuwa/kuoa mwanamke zaidi ya mmoja, kwa akili za wanawake wakishajua wako zaidi ya mmoja kwa mwanaume mmoja wanaanza kupambana wao kwa wao, watapambana kukuonyesha mapenzi na kutimiza majukumu yao, na kila mmoja atakua na wivu dhidi ya mwenzie, hii itakusaidia kutokuwekeza hisia zako sehemu moja, wazee wa zamani walisema Usiweke mayai yote kwenye kapu moja.
Mimi naona hili nalo ni muhimu mana tunaona hata nchi za kiislamu ndoa zinadumu na wivu ni kidogo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ukiyachukulia mapenzi SAwa na dereva anaendesha gari barabarani mbele kuna watoto akili yake ipo kwenye pedal ya brake maana akili ya mtoto mda wowote inaweza akabadili maamuzi akataka kuvuka upande wa pili. Ukiwa na akili hii utoingia jela wala mochwari kisa mapenzi.
 
Elimu ya mapenzi ifundishwe mashuleni, wengi udhani wanaishi na malaika
Hili haswaa ni muhimu tena kwenye level za chini lifundishwe katika namna ambayo itasaidia kudeal generally na relation zote afu ikifika huku juu iwe inaenda specifically kwenye mapenz pia

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom