Maumivu ya bajeti ya 2021 yako hapa kwa wananchi wa kawaida

(i) Kutoza tozo ya shillingi 10 hadi shilingi 10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa. Kiasi cha tozo kinatofautiana kulingana na thamani ya muamala wa fedha unaotumwa au kutolewa. Pendekezo hili litaongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 1,254,406.14; na

(ii) Kutoza kiasi cha shilingi 10 hadi shilingi 200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji. Pendekezo hili litapelekea kuongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 396,306.0.

d. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147

Kutokana na vinywaji vikali kuwa na kiwango kikubwa cha kilevi, napendekeza kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 30 ili kuwa na uwiano wa viwango vya kodi kati ya Vinywaji kali na Bia. Hatua hii inatarajia kuiongezea mapato Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 60,769.35.

Utekelezaji wa hatua hizi nne kwa pamoja unatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 2,033,639.66.

U. Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi

89. Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kikodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2021, isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo. Aidha, Marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).
☝️☝️☝️☝️☝️☝️☝️☝️☝️☝️☝️☝️
Binafsi naona huu ni mzigo kwa wananchi wa kawaida kwa sababu wao ndio watumiaji wakubwa wa huduma hizo. Kwanini hayo makato yasingekuwa kwenye miamala mikubwa ya kibenk badala ya kukata 100 kwenye vocha ya 500!?

Unapandisha bia ya 1500 kwa 30% unataka watu wanywe gongo? Kwanini iyo asilimia usiweke kwenye Hennessy au Jack Daniel? Unataka double kick tuanze kununua 2500 tena? Una hamasisha vijana kubet badala ya kazi?

Mods please msiunge uzi huu nataka kila mtanzania atoe maoni yake kwenye wazi tofauti na uzi wa bajeti yote.
Ccm wamefika mwisho kabis awa kufikiri hawana jipya
 
(ii) Kutoza kiasi cha shilingi 10 hadi shilingi 200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji. Pendekezo hili litapelekea kuongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 396,306.0.
Sijaelewa vizur hapa ina maana lain nitaanza kuilipia kila siku?
 
Kutokana na vinywaji vikali kuwa na kiwango kikubwa cha kilevi, napendekeza kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 30 ili kuwa na uwiano wa viwango vya kodi kati ya Vinywaji kali na Bia. Hatua hii inatarajia kuiongezea mapato Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 60,769.35.
Mshana Jr soma hapo mtani
 
Huo mtindo ulikuepo kabla ya JPM lakini haikupinguza wanywaji,alipokuja JPM bia zilishuka toka 2500 mpaka 2000 na 2000 mpaka 1500 na kwa miaka mitano hakikuwai kupanda
wanaonunua ni wachache
 
Mkuu mapendekezo yote yatamgusa mtu wa kawaida fikiria kuongeza ushuru wa kiasi 100 kwenye mafuta yote hapo lazima gharama za usafiri zipande hivyo kupelekea bidhaa kupanda bei na huenda mfumuko wa bei maana mzigo wote huo anaubeba final consumer

Halafu waziri haoni hayo anajichekesha eti hata akipendwa na watu wa jimbo lake na wa Yanga inatosha watakupendaje ili hali unaibana hali yao ya maisha au wao hawataathirika??
 
The government is preaching financial inclusion of the majority of the population at the same time it is increasing the cost of banking dervices by charging levies on deposits and withdrawals!!! You better synchronize these financial policies in order to achieve your goals,
 
Huyu mama hapo kwenye Kodi ya mihamala na Kodi ya laini anaenda kuchukiwa vibaya mno na wananchi wa kawaida ,yaan wamekaa wemeshindwa kuangalia angle nyingine had wakaja huku ambako kila mtu anaona wazwaz kuwa ananyongwa mchana kweupe, nilianza kuwa na iman nae ila kwa hili atapata wakat mgumu sana hasa kama ana nia mwaka 2025
 
(i) Kutoza tozo ya shillingi 10 hadi shilingi 10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa. Kiasi cha tozo kinatofautiana kulingana na thamani ya muamala wa fedha unaotumwa au kutolewa. Pendekezo hili litaongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 1,254,406.14; na

(ii) Kutoza kiasi cha shilingi 10 hadi shilingi 200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji. Pendekezo hili litapelekea kuongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 396,306.0.

d. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147

Kutokana na vinywaji vikali kuwa na kiwango kikubwa cha kilevi, napendekeza kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 30 ili kuwa na uwiano wa viwango vya kodi kati ya Vinywaji kali na Bia. Hatua hii inatarajia kuiongezea mapato Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 60,769.35.

Utekelezaji wa hatua hizi nne kwa pamoja unatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 2,033,639.66.

U. Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi

89. Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kikodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2021, isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo. Aidha, Marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).
[emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516]
Binafsi naona huu ni mzigo kwa wananchi wa kawaida kwa sababu wao ndio watumiaji wakubwa wa huduma hizo. Kwanini hayo makato yasingekuwa kwenye miamala mikubwa ya kibenk badala ya kukata 100 kwenye vocha ya 500!?

Unapandisha bia ya 1500 kwa 30% unataka watu wanywe gongo? Kwanini iyo asilimia usiweke kwenye Hennessy au Jack Daniel? Unataka double kick tuanze kununua 2500 tena? Una hamasisha vijana kubet badala ya kazi?

Mods please msiunge uzi huu nataka kila mtanzania atoe maoni yake kwenye wazi tofauti na uzi wa bajeti yote.
IMG-20210610-WA0118.jpg
 
Back
Top Bottom