Maumivu ya mwanamke kusalitiwa: Hana wa kumtetea, jamii inaona ni haki yake

Wanaume wengi wanaona raha wanapoona mke wake anateseka, anakonda na kulia kwaajili yake. Zama hizo zimeshapita. Tunawaacha mfanye mnachotaka.
Uzuri ni kwamba mabaya huwa yanawarudia wenyewe.
Elezea vizuri hapo. Mwanamke anateseka vipi wakati mumewe akiona raha?
 
Maumivu ya mwanamke anaposalitiwa yanaweza kuwa na athari kubwa sana kihisia. Hali hii inaweza kusababisha machungu na kuumiza moyo. Kila mwanamke anaweza kuhisi maumivu tofauti na kuonesha hisia tofauti kulingana na uzoefu wake binafsi na mazingira ya kijamii.
Kweli kabisa mkuu.

Mwaka jana wife alifuma sms ya Mwanahamisi kwenye simu yangu. Nilimwomba radhi yakaisha ila leo takriban mwaka lakini bado hali haijawa shwari.
Nahisi wife kapoteza kabisa imani na mimi, nahisi mabadiliko kwake!
 
Hakuna kitu kinauma kama kumsaliti mwanamke aliyekuamini, na kukupenda kwa moyo wake wote,sikia kwa mtu isikukute
 
Alafu ukute we ndo mwanaume wake wa kwanza hajui mwingine then umsaliti,ni dhambi kubwa sana sema tu hamjui,maumivu anayopata mwanaume akisalitiwa are the same to women too,lkn Cha kushangaza mwanamke anaambiwa avumilie ila mwanaume anaambiwa afukuze hafai,but ndio mfumo wetu ulivyoundwa so hatuna namna
 
Cha muhimu ni kupima kbla ya tendo hivi vingne vyote sjui maumivu ni kujiendekeza tu na ubinafsi ulio pitiliza.
 
Njemba tunaonaga fahari na kufanya ushindani kuwala kwa wingi kumbe ni ushamba tu.

Uaminifu, Heshima na Unynyekevu puyanga moja ukose vyote.
 
Haki sawa ni Ajenda ya Freemason na Illuminati. Feminists ndio ma agent wao wa kuwasaidia kuharibu jamii.

Yes
Kuna jarida 1 nilisoma anasema
Wanawake ni rahisi kushawishika na shetani huwatumia kwa ajili kufanikisha mambo yake.

Mf: Eva pale bustani ya eden

Au kumshauri Mwanamke anayeamini hawa manabii/wachungaji hao ni rahisi mno kiasi cha kutekeleza ndoa yake

Au mtoto wa kike umshauri kuhusu wanaume hakuelewi ni hadi apachikwe mimba ndo akili kidogo hurejea akisha zaa
baada ya muda utasikia wanaume mi siwataki muda si mrefu anarudi kule kule

Kwa ujumla mi naona asili ya mwanamke ni wa kushawishiwa sio kusalitiwa anajisaliti mwenyewe.

Kwenye ndoa mwanaume akiwa mtawala asiruhusu ujinga wa 50/50 aishi kibabe na mkewe ndoa inakuwa safi mke asizoee kuona meno yako!

Biblia inasema
Waefeso 5:33
“mke amtii mume na mume ampende mke”

Wakolosai 3:19
Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.

Eleweni hizo statements

Mwisho kabisa mji wako kama mwanaume au familia yako ili iheshimike mume fanya iliyo wajibu wako na ukitaka mji au familia yako idharauliwe ujue mume ndo chanzo cha dharau hizo!
 
Sio kwamba jamii imemjengea mwanamke huo mtazamo, hii ni nature tokea dunia imeanza mpaka leo hii kuanzia kwenye vitabu vya dini mpaka kwenye history za kiafrika polygamy ndo utaratibu.

Hivyo jamii imemnyanganya mwanaume haki ya kuwa na wake wengi na matokeo yake ndo haya uliyoyaandika.
Haki tunyimwe sisi nyie ndo mnalalamika
Polyginy ni nature?
 
Maumivu ya mwanamke anaposalitiwa yanaweza kuwa na athari kubwa sana kihisia. Hali hii inaweza kusababisha machungu na kuumiza moyo. Kila mwanamke anaweza kuhisi maumivu tofauti na kuonesha hisia tofauti kulingana na uzoefu wake binafsi na mazingira ya kijamii.

Mbaya zaidi mwanamke amezungukwa na jamii ambayo inamjenga kuwa yeye kusalitiwa au kuumizwa kihisia ni sehemu yake na hapaswi kuonesha hisia za kukataa hali hiyo, mwanamke kajengwa kuvumilia usaliti kutoka kwa wanaume huku akidanganywa kwa kusifiwa kuwa ndiye mwanamke bora na anapaswa kukubali hali hiyo.

Imekuwepo kampeni kuwa mwanamke anayevumilia mwanaume wake kuwa na michepuko ni mke anayefaa kwani hujenga familia, bila kujali kuwa anaumia kihisia na kuteseka kwa msongo wa mawazo kwani hana sehemu ya kupeleka lawama wala kulalamikia kwa kuwa jamii imeshamtengenezea mazingira kuwa hayo ndiyo maisha yake na akienda kinyume na hapo hushambiliwa kuwa hana uvumilivu na kwamba hafai kuwa mke wa mtu.

Jamii imekuwa ikihubiri kuwa mwanaume anahaki ya kuchepuka na kwamba huo ndio uanaume na ndio fahari kwao kitu ambacho kina athari sana kwa ustawi wa familia na kinamuathiri sana mwanamke japo hana namna kwa kuwa tayari kashawekewa mazingira ya kukubaliana nacho japo kinamuumiza sana.

Baadhi ya maumivu ya kihisia yanayoweza kujitokeza ni pamoja na:
  1. Kuvunjika kwa uaminifu: Kusalitiwa kunaweza kuharibu msingi wa uaminifu katika uhusiano. Mwanamke anaweza kuhisi kuvunjika moyo na kuhisi kama imani yake imesalitiwa.
  2. Kukosa thamani: Mwanamke anaweza kuanza kuhisi kuwa hana thamani na kuanza kujidharau. Hii inaweza kusababisha kupungua kwa kujiamini na kujiona kuwa si wa kuvutia au wa kustahili.
  3. Hasira na huzuni: Kusalitiwa kunaweza kusababisha hisia za hasira na huzuni. Mwanamke anaweza kuhisi kuvunjika moyo, kuhisi kudhalilishwa, au kuwa na ghadhabu kuelekea mwenzi wake au mtu aliyehusika katika usaliti huo.
  4. Kupoteza imani katika mahusiano: Kusalitiwa kunaweza kusababisha mwanamke kupoteza imani katika mahusiano na kuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kusalitiwa tena. Hii inaweza kusababisha ugumu katika kuamini watu wapya na kujenga uhusiano mpya.
Ni muhimu kutambua kuwa kila mtu anaweza kuhisi maumivu tofauti na kuharibika kihisia kwa njia tofauti. Kwa wengine, maumivu yanaweza kupungua kadri muda unavyosonga na kupitia mchakato wa kupona, huku wengine wanahitaji msaada wa ziada kutoka kwa marafiki, familia, au wataalamu wa ustawi wa akili kusaidia kupitia maumivu hayo.
Fata Uislam hautahisibuowekwnkqa sababu unakuwa umejisalimisha kwa Muumba wako.

Mradi usiwe Muislam jina, ufate mafundisho yake ya Uislam, utaelewa namna ya kuishi maisha yako bila wasiwasi.
 
Ngoja niheshimu uhuru wako wa kutoa maoni!
 
Tunachepuka kwa sababu ya ny*g* tu tunaoa kwa sababu ya maisha.

Shida nae wanawake wanatofautiana sana unakuta ana akili za maisha tabia njema lkn hana amsha amsha kitandan unapiga tu kupata watoto.

Kuna wengn aisee kitandan unamtafuna mpaka unatosheka lkn kwingineko kote hana jipya mitazamo yake ya kimaisha imekaa kitikotokitikitoki.

Dili ni kuchepuka lkn usigundulike ili usimuumize mtoto wa watu
Upo sahihi kbsa mkuu, nakazia ujumbe
 
Ila wanawake ndio wanaongoza kwa kuwaumiza waume zao kihisia,sema wanaume hawanaga tabia ya kusema mateso wanayopata kwa wake zao ila wanaumiaga Sana Yaani.
 
Ai
Sasa mbona mnaringa?
Ukimuambia mke wa ndoa geukia huku muda wa usiku ataanza kutoa visingizio visivyo na miguu, Mara naumwa na tumbo, au siko kwenye mood au nimechoka. Mwanamke Kama huyo atakosa kusalitiwa?
Siku akiamua kukupa Ni Kama anakufanyia favour, kwa Hali hii mwanamme utaacha kua na mchepuko?
Wanawake up your game na hatasalitiwa....
Aisee!
 
Maumivu ya mwanamke anaposalitiwa yanaweza kuwa na athari kubwa sana kihisia. Hali hii inaweza kusababisha machungu na kuumiza moyo. Kila mwanamke anaweza kuhisi maumivu tofauti na kuonesha hisia tofauti kulingana na uzoefu wake binafsi na mazingira ya kijamii.

Mbaya zaidi mwanamke amezungukwa na jamii ambayo inamjenga kuwa yeye kusalitiwa au kuumizwa kihisia ni sehemu yake na hapaswi kuonesha hisia za kukataa hali hiyo, mwanamke kajengwa kuvumilia usaliti kutoka kwa wanaume huku akidanganywa kwa kusifiwa kuwa ndiye mwanamke bora na anapaswa kukubali hali hiyo.

Imekuwepo kampeni kuwa mwanamke anayevumilia mwanaume wake kuwa na michepuko ni mke anayefaa kwani hujenga familia, bila kujali kuwa anaumia kihisia na kuteseka kwa msongo wa mawazo kwani hana sehemu ya kupeleka lawama wala kulalamikia kwa kuwa jamii imeshamtengenezea mazingira kuwa hayo ndiyo maisha yake na akienda kinyume na hapo hushambiliwa kuwa hana uvumilivu na kwamba hafai kuwa mke wa mtu.

Jamii imekuwa ikihubiri kuwa mwanaume anahaki ya kuchepuka na kwamba huo ndio uanaume na ndio fahari kwao kitu ambacho kina athari sana kwa ustawi wa familia na kinamuathiri sana mwanamke japo hana namna kwa kuwa tayari kashawekewa mazingira ya kukubaliana nacho japo kinamuumiza sana.

Baadhi ya maumivu ya kihisia yanayoweza kujitokeza ni pamoja na:
  1. Kuvunjika kwa uaminifu: Kusalitiwa kunaweza kuharibu msingi wa uaminifu katika uhusiano. Mwanamke anaweza kuhisi kuvunjika moyo na kuhisi kama imani yake imesalitiwa.
  2. Kukosa thamani: Mwanamke anaweza kuanza kuhisi kuwa hana thamani na kuanza kujidharau. Hii inaweza kusababisha kupungua kwa kujiamini na kujiona kuwa si wa kuvutia au wa kustahili.
  3. Hasira na huzuni: Kusalitiwa kunaweza kusababisha hisia za hasira na huzuni. Mwanamke anaweza kuhisi kuvunjika moyo, kuhisi kudhalilishwa, au kuwa na ghadhabu kuelekea mwenzi wake au mtu aliyehusika katika usaliti huo.
  4. Kupoteza imani katika mahusiano: Kusalitiwa kunaweza kusababisha mwanamke kupoteza imani katika mahusiano na kuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kusalitiwa tena. Hii inaweza kusababisha ugumu katika kuamini watu wapya na kujenga uhusiano mpya.
Ni muhimu kutambua kuwa kila mtu anaweza kuhisi maumivu tofauti na kuharibika kihisia kwa njia tofauti. Kwa wengine, maumivu yanaweza kupungua kadri muda unavyosonga na kupitia mchakato wa kupona, huku wengine wanahitaji msaada wa ziada kutoka kwa marafiki, familia, au wataalamu wa ustawi wa akili kusaidia kupitia maumivu hayo.
Very true
 
Back
Top Bottom