Uchaguzi 2020 Mawakala wa CHADEMA Chato waeleza kuwa hawajaapishwa

Uchaguzi 2020 Mawakala wa CHADEMA Chato waeleza kuwa hawajaapishwa

Huyo mkurugenzi anautaalamu gani kubaini saini za mawakala Basi atuonyeshe sahihi original aliyonayo tulinganishe.
 
Haya ndiyo mambo yanayomuaibisha Maguguli na kumfanya adharaulike na kila mwenye akili.

Huyu msimamizi wa uchaguzi lazima ana uwendawazimu. Bila shaka anayejipendekeza kwa Magufuli. Watu kama hawa ni wa kufukuzwa na kisha kucharazwe fimbo mbele ya umma kwa kuvuruga uchaguzi. Magufuli asipofanya hivyo maana yake anataka kesema kuwa majitu kama haya yanafanya hivyo kwa maelekezo yake.

Msimamizi wa uchaguzi kama huyo, asiwapotezee watu muda. Huyo ni kusakwa kokote aliko, hata akiwa nyumbani kwake, popote atakapopatikana acharazwe fimbo. Watu wajinga kama huyo msimamizi wasituharibie Taifa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchaguzi una dalili zote za kwenda kama gari bovu!

Abiria Mungu atusaidie!!
As long as DEDs (mostly wana CCM na wateule) wanasimamia chaguzi hizi, itakuwa story ni hii hii miaka yote. Bahati mbaya kila mtu anajua haya yatatokea but still tunaingia kwenye uchaguzi
 
Uchaguzi una dalili zote za kwenda kama gari bovu!

Abiria Mungu atusaidie!!
NEC ndiyo ilitakiwa kuwa BOSS wa maDED lakini naona maDED ndio wanakuwa maBOSS. NEC inasema hivi maDED wanawavimbia na kuwagomea kwa kujua kuna mtu atawalinda.
 
Dah... Asante Sana mkuu. Kumbe wananchi wa Songwe siyo wa mchezo mchezo. Kwa nyomi hilo la binadamu lzm alainike, atake asitake

CHADEMA
Njooni hapa mpate somo
Sasa hii iwe nchi nzima, mbona watakaa hawa wadharimu
 
Hivi hao wakurugenzi wa majiji na manispaa walipewa seminar kuhusu uchaguzi kuhusu mawakala? Ni aibu Sana...wakurugenzi ni waharibifu wakubwa sana wa mchakato wa uchaguzi.

Hawa wakurugenzi ni makada wa CCM , walianza kuvuruga uchaguzi wa serikali za Mitaa na vijiji November 2019 sasa 2020 wakaanza kuengua wagombea wa udiwani na ubunge. Hili la mawakala ni muendelezo wa kuvuruga mchakato wa uchambuzi wa madiwani, wabunge na urais.

Mchakato wa uvurugaji uchaguzi unaendelea labda majina ya wapiga kura kutoonekana, mawakala walioapishwa kuzuiwa kuingia vituoni n.k tusubiri tukielekea tarehe 28 Oktoba pengine mengi ya ajabu ya wasimamizi wa uchaguzi tutayabaini.
 
13 May 2019

UCHAGUZI MKUU 2020: MWANASHERIA MKUU AFUNGUKA HATIMA YA WAKURUGENZI, SERIKALI KUKATA RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA MAHAKAMA KUU


Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi leo tarehe 13 mwezi Mei mwaka 2019 amesema athari za hukumu ya Mahakama Kuu kubatilisha vifungu vinavyowapa Mamlaka Wakurugenzi kusimamia chaguzi amesema hawapaswi kuwa na wasi wasi kwa kuwa ipo nafasi ya kukata rufaa ambapo inapotolewa hiyo inafanya hukumu isitekelezwe.
 
12 February 2019

SERIKALI YABWAGWA KESI YA KUZUIA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI


Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali pingamizi za upande wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye kesi ya kikatiba inayopinga Wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi
 
21 October 2020
Kigoma, Tanzania

HUKO KIGOMA, MAWAKALA WAPIGANA VIKUMBO KUGOMBEA KUINGIA KUAPISHWA


Mawakala wa vyama vya siasa jimbo la Kigoma mjini,wakigombania kuingia ndani ya ukumbi kwaajili ya shughuli ya kuapishwa

:
 
22 October 2020

LEMA ADAI KUMKUTA DC WA ARUSHA NA DSO KATIKA CHUMBA CHA FOMU ZA KIAPO ZIKIWA MEZANI "NAWAONYA WASINGILIE "


CHADEMA wahoji Mkurugenzi amewezaje kuhakiki fomu zaidi ya 11,000 za mawakala wa wagombea ndani ya dakika 10 katika mazingira yenye changamoto kubwa huku 500 na zaidi kukataliwa.


Mawakala wa CCM mjini Arusha mpaka saa 5 usiku jana walikuwa hawajaanza kuwakilisha fomu zao kwa mkurugenzi.

Wapiga kura zaidi ya 100,000 kufuatana na taarifa rasmi wameongezeka mjini Arusha hivyo CHADEMA wataanza kuchunguza ongezeko hilo ktk daftari la mpiga kura na CHADEMA kuanza kufuatilia kutafuta picha za inayodaiwa feki zilizokopiwa toka Facebook na Instagram kuhalalisha vitambulisho vya wapiga kura......
 
Bahati mbaya kila mtu anajua haya yatatokea but still tunaingia kwenye uchaguzi
Nadhani Kadiri miaka inavyoenda mambo yameendelea kubadilika; Ishu za mawakala hazikuwa ishu sana miaka ya 2000 na 2005; Enzi hizo ishu ilikuwa kutangaza mmshindi, Sasa ivi hali inabadilika, mambo yanaanza kabla ya Uchaguzi, maana Loop hole ni chache sana.

So watu wamefunguka sana.
 
22 October 2020
Jimbo la Mbeya mjini
Mbeya, Tanzania

MAANDAMANO CHADEMA MBEYA WALIA OFISI ZA MKURUGENZI



Wananchi wa meandamana mpaka halmashauri ya jiji la Mbeya huku wakimtaka mkurungezi DED kuwarudisha wagombea udiwani waliofutwa Jana tarehe 21mwezi huu siku ya jumatano
 
Bahati mbaya kila mtu anajua haya yatatokea but still tunaingia kwenye uchaguzi
Mkuu, unataka ccm wabaki wenyewe kama ilivyokuwa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka Jana, au? Kama ndivyo, tija yake ni nini?
Siyo itakuwa sawa na kususia Fisi kitoweo?!

Em dadavua
 
Chato, Geita
Tanzania

Polisi yaruhusu mawakala 600 wa CHADEMA kuapishwa.​



Polisi yajiridhisha hakuna udanganyifu wa saini kuwatambulisha mawakala wa CHADEMA kwa mkurugenzi Halmashauri ya Chato, hivyo zaidi ya mawakala 600 wa CHADEMA waapishwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2020.

Na huko Bukoba mkoani Kagera mgombea ubunge wa Bukoba mjini Chief Kalumuna naye aachiwa baada ya kukamatwa na Polisi kutokana na mgombea hhuyona mawakala wa CHADEMA Bukoba mjini kumshindikiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba kuonekana kusuasua kuwaapisha na hivyo kukatokea kutoelewana ktk ofisi za Mkurugenzi na Polisi kuitwa.
 
26 October 2020
Chato, Geita
Tanzania

"CHATO HAWAJAWAHI KUJIPATIA MBUNGE WA WANANCHI" - AFAFANUA MWL. MICHAEL LUCAS​

Mgombea ubunge Kamanda Lucas Michael Massai katika kampeni za 2020 kuomba ridhaa achaguliwe kupitia CHADEMA


Historia ya mgombea ubunge wa CHADEMA : 2015
M/kiti CWT aingia matatani kwa kuhudhuria mkutano wa Lowassa

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Chato mkoani Geita, ameshtakiwa kwa kosa la kwenda kuhudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Serikali imemfungulia mashtaka Mwenyekiti huyo, Lucas Michael maarufu Masai kwa madai ya kukiuka maadili na utaratibu wa utumishi wa umma.

Michael ameshtakiwa kwenye Tume ya Utumishi wa Umma, Idara ya Utumishi wa Walimu wilayani hapa.

Michael anadaiwa siku ya mkutano huo wa kampeni, alimweleza mgombea huyo kuwa serikali imeshindwa kuwasafirisha walimu waliostaafu kurudi makwao, kulipa madai ya walimu na kutowapandishwa madaraja.

Pia, alidai kusikitishwa na kitendo cha uongozi wa Wilaya ya Chato kuwaandama baadhi ya walimu wanaoonekana kuunga mkono upinzani na wanaoiunga mkono CCM hawachukuliwi hatua yoyote ya kinidhamu.

Mwenyekiti huyo wa CWT alihudhuria mkutano wa kampeni za mgombea huyo alipofika wilayani Chato Septemba 19, baada ya kupokea mwaliko wa Chadema Wilaya ya Chato akiwa kama mdau wa elimu.

Kwa mujibu wa mashtaka hayo, Michael anadaiwa kukiuka maadili na utaratibu wa utumishi, Kanuni namba 65(1) na kutakiwa kujieleza.

Chanzo: Mwananchi
 
15 October 2020
Geita, Tanzania

MGOMBEA UBUNGE CHATO CHADEMA AVAMIWA



15 October 2020 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita,Henry Sikoki Mwaibambe amesema Jeshi hilo linaendelea kusaka kundi la watu waliovamia na kuvunja geti nyumbani kwa Mgombea Ubunge Jimbo la Chato kisha kuchoma moto turubai ya Bajaji No. MC 148 BFQ na MC 533 CBD vitu vyote vikiwa na thamani ya Sh. 672,000.

Mwaibambe amesema kundi hilo la watu lilivamia nyumbani kwa Lucas Micahel Masai ambaye anawania kiti cha Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Aidha kamanda huyo amebainisha kuwa mbali na Mgombea huyo pia kundi hilo lilivamia nyumbani kwa Nicolous Khamis pamoja na nyumbani kwa Maduka Marko ambaye ni Mgombea Udiwani kata ya Muganza Chato kwa tiketi ya CHADEMA.
 
Hata mm nimemkwida mkurugenzi. Mpk OCD alipofika alikuwa anahema kama kuku anayeumwa mdondo. Nyambafu!

Akashauriwa aapishe mawakala wangu 6 aliyokuwa anawafanyia figisu.

Tuacheni uwoga watanzania. Lisu anachechema lkn ujasiri 100% wewe uko kamili na viungo vyote ujasiri 0%
Hahaha I like it
 
Back
Top Bottom