Mawakili 386 wajitokeza kumtetea Mbowe Mahakamani 05/08/2021

Mawakili 386 wajitokeza kumtetea Mbowe Mahakamani 05/08/2021

Sisi wengine kazi yetu kusugua magoti kumlilia Mungu,na siku hizi majibu hayachelewi sana,yule aliyetusakizia tozo na ada za line za simu naye tia maji tia maji huko.
Screenshot_20210604-141546.jpg
 
Sio kosa wala sio jambo la kisiasa kuwakilishwa na mawakili 386, kwasababu sheria za nchi zinatoa haki kwa washtakiwa wote kutetewa na mawakili mbele ya mahakama (Natural Justice - Right To Be Represented).

Ila cha ajabu CCM wataligeuza jambo hilo la Gaidi Freeman Mbowe kuwa la kisiasa zaidi, kama alivyotangulia IGP Sirro kuligeuza la kisiasa jana kwenye press na waandishi wa habari. Akaenda mbele zaidi na kumtia hatiani hata kabla mtuhumiwa Gaidi Freeman Mbowe hajafikishwa mbele ya mahakama.

Cha ajabu IGP Sirro hakuwahi kuongelea kwenye vyombo vya habari swala la viongozi wa umma kutumia vijana wake wa police kufanya uhalifu. Mfano, Paul Makonda na Ole Sabaaya walivokua wakitumia vijana wa IGP Sirro kufanya uhalifu wa kutumia silaha na risasi (Kama alivosema jana tunanunua kwa hela zetu) kuteka na ujambazi Dar Es Salaam, Arusha, Moshi na Kilimanjaro.

IGP Sirro mungu anakuona, mmeshaisiriba kinyesi Tanzania kwenye swala la mbowe.
Shida ya vyeo vya kupewa inabidi kujivua nguo hata mbele ya watoto ili kumfurahisha aliyekupa cheo. Kwa nafasi yake hakutakiwa kuliongelea kwa vyombo vya habari kwa sababu suala liko mahakamani
 
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mh Boniface Jacob amesema hadi leo jumla ya mawakili wasomi 386 wamejitokeza na kujiandikisha kumtetea Freeman Mbowe mahakamani siku ya Agost 5 katika mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam.

Nawasalimu kwa jina la JMT.

My take; Huu utitiri wa mawakili siyo maandamano kweli?
Mwambie mkuu wa mijibwa ya CCM awazuie hao mawakili
 
Mama Samia either amekubali kudanganywa kindezi na hard-liners ndani ya taasisi za juu au hana total control juu ya baadhi ya mambo nyeti. Vitu vingine ni kujitafutia unnecessary attention zinazojenga taswira negative na kufuta yote mazuri yaliyokuwa yameanza kuonekana. Hata kama Mama anataka kustamp her authority, sio kwa vitu kama hivi.

Yaani wale Mashekhe wa uamsho sio magaidi ila Mbowe ni gaidi? Tell it to the birds..
 
CCM, ushawishi uliisha toka 2010.
Kilichopo sasa ni kuhangaikia moyo wao tu.
Tume ya uchaguzi imetumika, imeshindikana.
Hela yetu ya serikali imetumika, imeshindikana.
Jeshi limetumika, imeshindikana
Mahakama imetumika, imeshindikana.
Watakapo kuja kutafuta mwafaka kwa mazungumzo na makundi mbalimbali, itakuwa washa chelewa.
Kilichobakia ni kuondolewa kwa nguvu na kudhalilishwa kusiko kifani na kinyume na haki za binadamu.
Tusubiri hiyo siku haipo mbali.
Tulisema hivi hivi kwa mwenda zake, werevu wslishituka ,ila walevi wa madaraka wajabakia na hangover zao.
 
"kutokakana na uwepo wa janga la corona mahakama imeruhusu jumla ya watu wasiozidi kumi na tano kutoka pande zote mbili, kuhudhulia kesi unayomkabili Mh. Mbowe, 5/8/2021" Jaji

Corona!! Corona!!! Corona!!!....... [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23] Afrika ina vituko sana.
Wale wazungu wanaotusema na kutunanga, wanapoteza muda tu. Hizi mbichwa ni kizungumkuti.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom