Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Mwanzoni katika kesi ya Mbowe, Kila Pingamizi la utetezi lilikuwa linagonga mwamba na vielelezo vikawa vinapokelewa “by hooks and crooks”

Utetezi ukabadili mbinu kuokoa muda wa wateja kwani walijua mapingamizi yao yangekula muda na yangetupwa.

Ikabuniwa mbinu mpya

Utetezi ukawa unakubali vielelezo na ushaidi uingie mahakamani.

Wakawa wana challenge ushahidi na vielelezo kwa mlango wa nyuma wa cross examination.

Mashaidi wakapwaya na vielelezo vikapwaya mbele ya jaji watanzania wakishuhudia.

Wakabainisha blunders mbali mbali zifuatazo

1. Washtakiwa walikamatwa kabla hata jalada halijafinguliwa. Hii inamaanisha waliwakamata ndipo jitihada za kupika kesi ndio zikaanza. Inaonekana wapangaji wa hili walihamaki kuona makomandoo wakimlinda Mbowe na Lissu. Pengine mawasiliano yao yakafatiliwa yakawaongoza kwa Urio

Inaonekana Urio “akafinywa” (Haya yanathibitishwa na maelezo ya watuhumiwa katika kesi ndani ya kesi kuwa walimuona urio akipigwa kituo cha Tazara)

Baada ya kufinywa Urio akaeleza jinsi alivyowatafutia kazi lakini akalazimishwa kuwa shaidi wa Jamuhuri ili kulinda kazi yake.

Katika hali ya kupanick wapangaji wa kesi hii wakahisi inawezekana makomandoo wote waliofukuzwa kazi watakuwa wameenda kufanya kazi kwa Mbowe hivyo katika kamata kamata ndipo Komandoo MHINA akakamtwa Tabora na kina Kingai na Mahita. (Mhina alitoa ushahidi akiwa defense side)

2. Nyaraka zilikuwa zinaungwaungwa. Utetezi uliooomba Detention register ya Chang’ombe na Central kwa tarehe walizokamtwa watuhumiwa, kwa kuwa Mashtaka hawakujiandaa na hili wakafoji nyaraka kwa kubackdate ikainekana wazi lakini Jaji akaamuru daftari lipokelewe.

3. Extraction report ya Tigo inaharibu kila kitu kwani inaumbua kuwa file lilifunguliwa 2021 lakini mashtaka walifai file lilifunguliwa 2020. Ripoti ya tigo inajibu file la polisi lenye refence ya mwaka 2021. Kipengele hiki kina legal implication kubwa sana kwa faida ya defense

4. Prosecution wameshindwa kuipa kesi miguu kwa kuonyesha ni jinsi gani pesa alizotuma mbowe ziliweza kuprocure ugaidi. Pesa zinaonekana ni za nguo,chakula, nauli. Pesa nyingine upelelezi hawakusema zilitumika vipi bali ukawa unajibu ni transaction fees.

Katika hoja ya transaction fee Kibatala alikuwa na swali moja tu.

Swali: Ulimwambia mheshimiwa jaji maswala ya transaction fee?

Jibu: Sikumwambia

Swali:Katika maelezo yako kuna sehemu tutaona umeelezea hivyo?

Jibu: Sikueleza

Hapa ndipo kesi ilipokatwa mtama

5. Polisi hawakijui kitendea kazi chao PGO. Kila ilipogusiwa PGO walikuwa wanatoa macho kama wanasoma talaka.

Hawajui Fomu ya Kuzuia mali, Fomu ya Gari la polisi, Fomu ya kulebbel vizibiti, nk.

1645095957107.png
 
Ikabuniwa mbinu mpya

Utetezi ukawa unakubali vielelezo na ushaidi uingie mahakamani.

Wakawa wana challenge ushaidi na vielelezo kwa mlango wa nyuma wa cross examination.

Mashaidi wakapwaya na vielelezo vikapwaya mbele ya jaji watanzania wakishuhudia.
 
Hii kesi nadhani ingekiwa imeshafutwa.
Kinachokwamisha ni kwakuwa mheshimiwa alilishwa matango pori mapema na yeye akayala bila kujiridhisha sasa wanaogopa kuifuta kwakuwa Chifu atadhalilika.
Ameshadhalilika mbona. Kitendo kwa swila kujibu kua hamna mtu aliyefungwa kwenye kesi hii tayari ilimuweka huyu mama mahali pabaya.
 
Extraction report ya Tigo inaharibu kila kitu kwani inaumbua kuwa file lilifunguliwa 2021 lakini mashtaka walifai file lilifunguliwa 2020. Ripoti ya tigo inajibu file la polisi lenye refence ya mwaka 2021. Kipengele hiki kina legal implication kubwa sana kwa faida ya defense
 
Prosecution wameshindwa kuipa kesi miguu kwa kuonyesha ni jinsi gani pesa alizotuma mbowe ziliweza kuprocure ugaidi. Pesa zinaonekana ni za nguo, chakula, nauli. Pesa nyingine upelelezi hawakusema zilitumika vipi bali ukawa unajibu ni transaction fees.
 
Back
Top Bottom