Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Mimi ni muumini wa msamaha kwa hiyo naungana na Lisu (ametamka redioni) kuwe tuwe na maridhiano ya kitaifa watu waombe msamaha hadharani kwa mambo ya hovyo waliyofanya kisha tusonge mbele kama taifa. Na naamini kuwa hata mheshimiwa Mbowe ni muungwana sana na mzalendo wa nchi hii kwa dhati ya moyo wake na yeye ni mtu wa maridhiano hasa nikifuatilia hotuba zake na hata matendo yake baada ya kufanyiwa hujuma ya rasilimali zake mbali mbali. Tufungue ukurasa mpya kwa kutengeneza katiba mpya ambayo itaziba mianya ya mambo haya ya ovyo kutokea tena.

Kusiwe na kulipizana kisasi kwani tukianza hivyo mzunguko wake hautakuwa na mwisho. Lakini pia biblia takatifu inatuambia kuwa kisasi ni cha Mungu kwa hiyo tumwachie Mungu mwenyewe.
Kama ni msamaha kina Kingai na wenzake ndiyo wanatakiwa kuomba msamaha kwa kutesa watu na familia zao bila sababu. Mbowe hana sababu ya kuomba msamaha kwa sababu hana kosa
 
mama leo akihojiwa na mtangazaji wa DW ameshangaza Sana kwamba hakuna mtuhumiwa wa ugaidi aliyefungwa kesi iko mahakamani tuache Jambo kesi iamuliwe na mahakama hiyo kesho ,bbc akihojiwa alisema washafungwa au alishindwa kutofautisha mahabausu na kufungwa gerezani
Nadhani walimmisslead. Alipohojiwa na BBC alisema "nadhani wenzake (Mbowe) wanatumikia vifungo vyao" . Hivyo alijua kuwa tayari wamehukumiwa na ni wafungwa na siyo mahabusu
 
Roho mbaya haitawasaidia lolote...

Baada ya hii kesi watu watakuwa makini sana na namna wanavofanya mambo yao

Vile vile Jeshi la police litapoteza uaminifu baina yao wenyewe,,,na wale makomandoo wastaafu wataendelea kuwa walinzi wa mheshimiwa...

Na sasa kina kingai na genge lake wajipange sana
Even if ikiwa hivyo. Next time mbowe anatafuta walinzi awe extra careful maana now ajue vyombo vinatafuta kila upenyo wa kumuweka ndani
 
Kwani kuna dhambi gani Mbowe kumtumia Urio pesa? Lakini pia upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kuwa hizo pesa zimetumika kufadhili vitendo vya kigaidi.
Subirini kesho- ndiyo mjadala utanoga
 
Je unajua kwamba Samia Suluhu Hassan akihojiwa na BBC SWAHILI, alisema kwamba MBOWE ni GAIDI?

Je MBOWE kaacha lini ugaidi? Naomba majibu, na nitakudai
Lissu akizungumza na Samia alitaja hiyo kesi kama haina maana. Hii ina maana hata maoni ya mama kuhusu hiyo kesi hayakuwa sawa, alipotoshwa na waliofungua kesi sababu rais siye aliyefungua kesi ila wakamuingiza mkenge.
 
Kuna sababu zozote wametoa??
Mawakili wa mashitaka wanadai ushahidi wao umekamilika, hivyo mahakama ione kwamba Mbowe na watuhumiwa wengine wana kesi ya kujibu. Sababu yao ni kiwango cha ushahidi kimejitosheleza kuishawishi mahakama kutoa maamuzi na kuwaona washitakiwa wana kesi ya kujibu.
 
Ni ngumu sana kuisemea nafsi ya mtu. Lakini naamini akijua hakuna adhabu ya ziada baada ya kuomba msamaha naye anaweza kukiri ukweli na kuomba msamaha. Na hii dhana ya kuomba msamaha ni dhana ngumu sana kwetu Tanzania kwasababu mara nyingi viongozi wanakosea lakini badala ya kuwaomba msamaha wananchi utasikia wanakanusha au wakati mwingine wanajikausha kabisa kama sio wao waliokosea wananchi. Na wakati mwingine tu hata katika ngazi ya familia suala la kuombana msamaha linakuwa gumu sana. Lakini kama taifa lazima tufike mahali tuwe na sehemu ya kuanzia. Na ingependeza zaidi tukanzia hapa kwenye kesi ya Mbowe jumlisha kumharibia vitega uchumi vyake na Lisu kupigwa risasi kisha tusonge mbele pamoja kama taifa.
Hoja nzuri sana. Nadhani hata wale wenye ubishi wa kisiasa, wasome hapa ili tusonge mbele kama Taifa. Tuanze upya.
 
Hata mimi sijaelewa hapa, siasa ni michezo kama michezo nyingine.

Tumsubiri chifu arudi nchini tuone kama atasema lolote.
Judge anatoa uamuzi tr 18/02/2022. Chifu akihojiwa na Sudi Mnete wa DW, amesema kesi iko mahakamani na iachwe iamue kama watuhumiwa wana hatia au la. Chifu kajiweka mbali na hili. Watu wasimuingize huku kwa aina yoyote ya maamuzi ya mahakama.
 
Judge anatoa uamuzi tr 18/02/2022. Chifu akihojiwa na Sudi Mnete wa DW, amesema kesi iko mahakamani na iachwe iamue kama watuhumiwa wana hatia au la. Chifu kajiweka mbali na hili. Watu wasimuingize huku kwa aina yoyote ya maamuzi ya mahakama.
Ati chifu kajiweka mbali😂 yeye ndo mtoa order kutoka juu leo kajiweka mbali, siasa zina vituko
 
Back
Top Bottom