Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Polisi kusema wanahitaji kuajiri wenye four ya mwisho inareflect katika hii kesi.

By the way naamini kwamba kila tukio linalotajwa kutokea lilitokea mfano Luteni kumtafutia watu Mbowe, kukutana na pesa kutumwa isipokua ugumu unakuja katika kuyatwist hayo matukio yafanane na ugaidi.

Pia naona hata kama upande wa mashtaka wamepika mashtaka basi walifanya hivyo haraka haraka na bila kuanticipate wapi panaweza leta mgogoro. Ndiyo maana inakua ngumu kwao kuthibitisha baadhi ya madai.
Kwa maneno machache baada ya kufuatilia hadi ilipofikia, nini imani yako kwenye hii kesi. Je, Mbowe na wenzake watatu, walikua wanapanga ugaidi?
 
Wameshamalizana kesho mbowe atakuwa huru chadema wasije na ngonjera za kuwa mbowe kashinda kesi wajue kabisa lisu washayajenga na mama
Na vipi ACP Kingai na wenzake, watapandishwa vyeo?
 
Nilivyoona kwenye kesi hii ni pale mipango yote ya upande wa Jamhuri yaliyokuwa yakipangwa gizani, yalikuja kuzungumzwa Mahakamani na Upande wa Utetezi. Hali hii iliwaogopesha Sana Jamaa wa Jamhuri. Walijiuliza Mambo yetu ya Siri tuliyoyazunfumza wenyewe imewafikiaje Jamaa wa Upande wa Utetezi?? Inamaana kuna watu miongoni mwetu wanaowapa/ wanaofujisha siri zetu.

Hata Jaji Tiganga mwenyewe alikujaona Hilo na akaanza kuwa na hofu pale anapohitaji kuwabebe upande wa Jamhuri. Unakumbuka hata Jaji Mkuu alifikia hatua ya kuwasemea Mawakili. Aliwalenga hasa wale wa Upande wa Mashitaka.

Mfano mwingine ni miamala iliyafanyika ktk kutuma fedha. Kuna miamala ilivyokuwa inamhusu Hussein Mwinyi (akiwa Waziri wa Ulizieni). Jaji Tiganga alipata hofu ni namna gani hawa Jamaa wa Utetezi waliipata miamala ile. Je waliipata kupitia Kampuni ya simu au kupitia Kwa baadhi ya maafisa wa Upande wa Mashitaka ama vipi.
 
Nachojua hata kama ameombwa kumwachia hawezi mwachia sasa hivi ataprove failure.kwahiyo watazungushwa weee siku zitapita.

Mpaka aachiwe lazima kuwe na ushahidi kuwa sio gaid. Sasa nani ataleta ushahidi huo kama sio kuacha kesi iendelee?

Tutaona huko mbele unless kuna makubaliano nje ya pazia
Mimi nadhani kwa ushahidi wa upande wa mashitaka ulipofikia, hadi wameshindwa kuendelea kuleta wengine, jaji kesho atatoa picha nzima ya hii kesi. Ushahidi gani unafikiri unatakiwa hapa ku prove kwamba Mbowe na wenzake ni magaidi? Labda kama hujafuatilia kwa karibu hii kesi. Swila ameimaliza hii kesi, ndiyo maana mawakili wa jamhuri wakaamua kufunga ushahidi.
 
Ila walishindwa kupangua ukweli kuwa Mbowe alimtumia pesa Urio
Hivi mkuu, kuna maeneo nikisoma hoja zako nakuona uko vizuri upstairs, lakini sehemu kama hizi inaleta mashaka kama uko vizuri upstairs. Hivi kwa pesa vile zilivyotumwa, zinakupa useme kuna ugaidi? Hata Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi naye alifanya ugaidi kumtumia pesa Bwire? (akiwa waziri wa ulinzi).
 
Lissu kamuomba Samia hiyo kesi ifutwe, wacha tusubiri majibu
Ifutwe kwa sababu hii kesi ni sawa na "hekaya za abunuwasi'
Wametesa sana watu wasio na hatia
wametesa familia zao bila kumuogopa Mungu
Ila laana yao ni kubwa sana kwani itatesa pia watoto wao hadi vitukuu! hilo walifahamu
 
Nafikiri wanachadema na wapenda haki wote Tanzania wanapaswa kuweka akiba mpaka hapo jaji atakapotoa hukumu yake. Naona wengi hapa wanashangalia kabla ya hukumu lakini ndio ile hali ya watanzania kusahau mambo ya msingi ndani ya muda mfupi. Watu wameshasahau jinsi mapingamizi ya wazi yalivyokuwa yanatupwa na jinsi maamuzi tata yalivyokuwa yanaamuliwa tokea jaji wa kwanza, wa pili na hata huyu watatu. Kama sheria na taratibu zingefuatwa tokea mwanzo hii kesi ilikuwa ni mfu tokea mapingamizi ya awali lakini ilitumika namna kuiendeleza mpaka Mungu alipoamua kuudhihirisha ukuu wake kupitia mashahidi wa mchongo kujichanganya sana kizimbani.

Kwangu mimi kama kuna makubaliano ya kuimaliza kesi bila masharti yoyote ni jambo la kupongezwa na ninaombea iwe hivyo. Sisi watanzania ni wamoja na hasa sisi tuliokulia enzi za Nyerere pamoja na shida zote za miaka ile lakini kuheshimu utu wa mtu na usawa ilikuwa ndio nguzo kubwa ya umoja wa taifa letu. Hakukuwa na matabaka ya aina yoyote lakini sasa hivi kuna watu eti wanataka kujiona wao ni bora na wanahaki zaidi kuliko wengine katika nchi hii kwa sababu tu wapo chama fulani. Hivi kuna raha gani ya maisha kumsingizia binadamu mwenzio mwenye familia na wategemezi kama wewe eti gaidi akaozee jela ili tu upate cheo? Hivi ni lini watanzania tulianza rasmi kuwa roho za kikatili kiasi hiki?
Kwa kweli inatia uchungu sana hasa nikikumbuka upendo wa watanzania tuliokuwa nao sio tu kati yetu watanzania kwa watanzania bali ulivuka mipaka mpaka Afrika nzima kiasi kwamba Tanzania ilisaidia nchi nyingine kupata uhuru wao.
Maneno machache, nini kifanyike kwa hawa waliotengeneza hili jambo kwa hawa watu wanaotegemewa na familia zao? Kingai na list nzima?
 
Mimi nadhani kwa ushahidi wa upande wa mashitaka ulipofikia, hadi wameshindwa kuendelea kuleta wengine, jaji kesho atatoa picha nzima ya hii kesi. Ushahidi gani unafikiri unatakiwa hapa ku prove kwamba Mbowe na wenzake siyo magaidi? Labda kama hujafuatilia kwa karibu hii kesi. Swila ameimaliza hii kesi, ndiyo maana mawakili wa jamhuri wakaamua kufunga ushahidi.
Kwa hiyo Mbowe ana kesi ya kujibu?
 
Maneno machache, nini kifanyike kwa hawa waliotengeneza hili jambo kwa hawa watu wanaotegemewa na familia zao? Kingai na list nzima?
Mimi ni muumini wa msamaha kwa hiyo naungana na Lisu (ametamka redioni) kuwe tuwe na maridhiano ya kitaifa watu waombe msamaha hadharani kwa mambo ya hovyo waliyofanya kisha tusonge mbele kama taifa.

Na naamini kuwa hata mheshimiwa Mbowe ni muungwana sana na mzalendo wa nchi hii kwa dhati ya moyo wake na yeye ni mtu wa maridhiano hasa nikifuatilia hotuba zake na hata matendo yake baada ya kufanyiwa hujuma ya rasilimali zake mbali mbali. Tufungue ukurasa mpya kwa kutengeneza katiba mpya ambayo itaziba mianya ya mambo haya ya ovyo kutokea tena.

Kusiwe na kulipizana kisasi kwani tukianza hivyo mzunguko wake hautakuwa na mwisho. Lakini pia biblia takatifu inatuambia kuwa kisasi ni cha Mungu kwa hiyo tumwachie Mungu mwenyewe.
 
Shahidi wa mwisho V/S mama mdogo wenu swali ni kwamba kati ya hawa wawili ni nani mwongo katika kesi hii tokea mwanzo
 
Tunaonyèsha kama kesi ni rahisi lakini tunapambana kutaka iondoshwe kwa amri ya Rais...
 
Hivi mkuu, kuna maeneo nikisoma hoja zako nakuona uko vizuri upstairs, lakini sehemu kama hizi inaleta mashaka kama uko vizuri upstairs. Hivi kwa pesa vile zilivyotumwa, zinakupa useme kuna ugaidi? Hata Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi naye alifanya ugaidi kumtumia pesa Bwire? (akiwa waziri wa ulinzi).
Hoja nzuri- sasa wakili Kibatala angalia alikopotezea mda
ulitumiwa 500,000 ukatoa 499000 umemwambia mh. Jaji 1000 imeenda wapi? halafu watu mnasema kaupiga mwingi na unaona una uwezo wa kupima uwezo wangu wa kufikiri- kwanza hicho kipimo hakipo
 
Mimi ni muumini wa msamaha kwa hiyo naungana na Lisu (ametamka redioni) kuwe tuwe na maridhiano ya kitaifa watu waombe msamaha hadharani kwa mambo ya hovyo waliyofanya kisha tusonge mbele kama taifa. Na naamini kuwa hata mheshimiwa Mbowe ni muungwana sana na mzalendo wa nchi hii kwa dhati ya moyo wake na yeye ni mtu wa maridhiano hasa nikifuatilia hotuba zake na hata matendo yake baada ya kufanyiwa hujuma ya rasilimali zake mbali mbali. Tufungue ukurasa mpya kwa kutengeneza katiba mpya ambayo itaziba mianya ya mambo haya ya ovyo kutokea tena.

Kusiwe na kulipizana kisasi kwani tukianza hivyo mzunguko wake hautakuwa na mwisho. Lakini pia biblia takatifu inatuambia kuwa kisasi ni cha Mungu kwa hiyo tumwachie Mungu mwenyewe.
Umenena vizuri sana mkuu ili Taifa lisonge mbele, tuanze upya. Lakini kama ingekua ni kitu kinawezekana kufanyika, unaona mtu kama ACP Kingai akiulizwa, anaweza kuongea ukweli na kuomba msamaha ili awe huru kwenye nafsi yake kwa yale aliyoyafanya kuifikisha hii kesi ilipofika?
 
Lissu kamuomba Samia hiyo kesi ifutwe, wacha tusubiri majibu
Kama ana akili timamu na ni mstaarabu atafuta tu bila kumuomba maana hata ye akitafakari iyo kesi haina kichwa wala miguu, kinachomsumbua anajua bila kutumia mabavu upinzani huwa wanawanyoosha vizuri tu kwenye election.....naye ni fever ya 2025 inamsumbua
 
Mwanzoni katika kesi ya Mbowe, Kila Pingamizi la utetezi lilikuwa linagonga mwamba na vielelezo vikawa vinapokelewa “by hooks and crooks”

Utetezi ukabadili mbinu kuokoa muda wa wateja kwani walijua mapingamizi yao yangekula muda na yangetupwa.

Pascal njoo Huku usome namna watu wanafanya analysis! Andiko safi kabisa!
 
Back
Top Bottom