Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

[emoji51][emoji51]Huu ni muda sasa wa [emoji1635][emoji482]na [emoji1298] kwa Watanzania.

Maana kesi imeshakwisha! Binafsi napenda sana kuona Watanzania wote tunaishi kwa amani, upendo, umoja na mshikamano! Huku tukiwekeza nguvu kubwa kwenye masuala ya maendeleo, maridhiano, uzalendo wa kweli kwa Nchi, na Demokrasia ya kweli!
Tuishi kwa amani, upendo, mshikamano na utelezi
Au siyo?
 
Nafikiri wanachadema na wapenda haki wote Tanzania wanapaswa kuweka akiba mpaka hapo jaji atakapotoa hukumu yake. Naona wengi hapa wanashangalia kabla ya hukumu lakini ndio ile hali ya watanzania kusahau mambo ya msingi ndani ya muda mfupi. Watu wameshasahau jinsi mapingamizi ya wazi yalivyokuwa yanatupwa na jinsi maamuzi tata yalivyokuwa yanaamuliwa tokea jaji wa kwanza, wa pili na hata huyu watatu. Kama sheria na taratibu zingefuatwa tokea mwanzo hii kesi ilikuwa ni mfu tokea mapingamizi ya awali lakini ilitumika namna kuiendeleza mpaka Mungu alipoamua kuudhihirisha ukuu wake kupitia mashahidi wa mchongo kujichanganya sana kizimbani.

Kwangu mimi kama kuna makubaliano ya kuimaliza kesi bila masharti yoyote ni jambo la kupongezwa na ninaombea iwe hivyo. Sisi watanzania ni wamoja na hasa sisi tuliokulia enzi za Nyerere pamoja na shida zote za miaka ile lakini kuheshimu utu wa mtu na usawa ilikuwa ndio nguzo kubwa ya umoja wa taifa letu. Hakukuwa na matabaka ya aina yoyote lakini sasa hivi kuna watu eti wanataka kujiona wao ni bora na wanahaki zaidi kuliko wengine katika nchi hii kwa sababu tu wapo chama fulani. Hivi kuna raha gani ya maisha kumsingizia binadamu mwenzio mwenye familia na wategemezi kama wewe eti gaidi akaozee jela ili tu upate cheo? Hivi ni lini watanzania tulianza rasmi kuwa roho za kikatili kiasi hiki?
Kwa kweli inatia uchungu sana hasa nikikumbuka upendo wa watanzania tuliokuwa nao sio tu kati yetu watanzania kwa watanzania bali ulivuka mipaka mpaka Afrika nzima kiasi kwamba Tanzania ilisaidia nchi nyingine kupata uhuru wao.
 
All in all nimempenda Kibatala nadhani ni miongoni mwa mawakili makini hapa nchini. Kesi yenye mashtaka magum kama hii kwa upande wangu ameimudu vizuri kwakweli.
Nadhani siyo nchini tu, ni East and Central Africa.
 
Hii kesi nadhani ingekuwa imeshafutwa.

Kinachokwamisha ni kwakuwa mheshimiwa alilishwa matango pori mapema na yeye akayala bila kujiridhisha sasa wanaogopa kuifuta kwakuwa Chifu atadhalilika.
Huko Brussels watakua wameliweka namna ya kupunguza aibu kwa Chief.
 
All in all, big up kwa wakili 'msomi kibatala na team yake' kwa namna alivyo wasambaratisha ma -mashetani ya CCM adi mengine Zaidi ya 10 yaka ogopa kuja kutoa ushaidi mahakaman!
Una maansha kwamba masuala ya mashahid ndio yameishia kwa Swila au sio???
 
Ameshadhalilika mbona. Kitendo kwa swila kujibu kua hamna mtu aliyefungwa kwenye kesi hii tayari ilimuweka huyu mama mahali pabaya.
Sasa vipi position ya IGP Simon Sirro kwenye kuhitimisha hili? Mbali na kwamba ndiye aliyemuaminisha president (maana ki protocol hakuna mwingine atafanya hivyo), lakini pia alisikika kwenye vyombo vya habari kwamba wana ushahidi mzito juu ya ugaidi wa Mbowe.
 
Hii nchi mwenye uchungu nayo alishaondoka. Wamebaki wapigaji tu. Sasa hii kesi haina miguu,wamepoteza mamilioni ya pesa ya kitupia kwenye ujenzi wa kipande fulani cha barabara,ksbb ya huu ujinga.

Ziro kaingizwa cha kike,akaingia mzima mzima. Nae kamuingiza mama chaka. Kama wana akili ndio wajifunze kufumua na kuunda kwa weredi idara zote zinazohusika na upelelezi.
Swali langu, hivi Sirro tunaendelea naye kama IGP hadi astaafu?
 
Kesi ya "UGAIDI" itafutika ki rahisi?.....
Walipanga kesi yenye jina kubwa, kufuta imekua ngumu sana. Lakini kwa ushahidi wa hovyo kutoka kwa akina Swila, Judge ataitupilia mbali. Ngoja tusubiri kesho tutapata mwanga.
 
Mungu ni mwema sana. Ile Extraction file kutoka kwenye ile Software ya waisraeli huwezi kufanya Editing. Mwisho wa siku ikabaki hivyo hivyo na tarehe ya 2021[emoji3][emoji3][emoji3]
Hiki kipengele sikujua kwamba kilivuruga ushahidi.
 
Back
Top Bottom