Mawakili wa Mbowe waache maswali yasiyo na msingi, ulizeni maswali ya maana mteja wenu aachiwe haraka

Mawakili wa Mbowe waache maswali yasiyo na msingi, ulizeni maswali ya maana mteja wenu aachiwe haraka

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Wengine wameonekana kuwasifia mawakili wa mtuhumiwa kwamba wana ustadi mkubwa katika kuwabana mashahidi wa upande wa mashtaka (eti hadi wanaomba kwenda msalani). Binafsi, naomba niwe tofauti. Mawakili wengi wa Kitanzania wanafanya mambo mengi kwa kukariri.

Ningependa maswali yafuatayo yaulizwe, either ndani au nje ya mahakama.

1. Je, Serikali imewahi kumhukumu au kumtuhumu Mbowe kwa tukio lolote la ugaidi ambalo liliwahi kufanyika ndani au nje ya nchi?

2. Ni kawaida sana kuona vikundi vya kigaidi vikiwa na majina ya kujitambulisha. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, kikundi cha kigaidi anachodaiwa kuongoza Mbowe kinaitwaje?

3. Mbowe anajulikana zaidi nchini kama Mwanasiasa. Ugaidi kwa tafsiri ni lazima uwe na agenda fulani. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, nini ni agenda ya kundi ambalo analodaiwa kuongoza Mbowe?

Sitegemei kama upande wa Mashtaka umejiandaa kujibu maswali ya namna hii hasa kama yataulizwa mwanzoni kabisa wa kesi. Majibu ya haya maswali kutoka kwenye vinywa vya upande wa mashtaka yana implications kubwa sana baada ya kesi, whether Mbowe amefungwa au ameachiwa huru.

Mawakili wa Mbowe, acheni kukariri kuhoji mapungufu ya technicalities. Hata kama kuna upungufu huko, kuyakomalia hayo hakuwezi kufanya kesi ifutwe kirahisi kama mnavyodhani. Nendeni moja kwa moja kwenye msingi wa kesi.
 
Hayo Maswali yako Unayo-Propose na Kuyaita ya Msingi tofuti na Ya kwenye PGO ni Zero kwa kesi inayomkabili Mbowe na Wenzake. Hayo Maswali yako ni ya Kutafutia kura kwenye Mikutano ya campaign, hivi kwa mashahidi unaotolewa na Mashahidi wa upande wa srikali Utambaulia nini si utakuwa nje ya case. In Short Maswali yako hayana mantiki.

Serikali Imewaleta mashahidi na wanakuwa cross- eximined na Upande wa utetezi kulingana na kile wanachokuja kutestify. Maswali yako yatunze yatatumika siku Mbowe akiwa anaomba kura za uraisi- 2025
 
Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Mawakili wa Mbowe, acheni kukariri kuhoji mapungufu ya technicalities. Hata kama kuna upungufu huko, kuyakomalia hayo hakuwezi kufanya kesi ifutwe kirahisi kama mnavyodhani. Nendeni moja kwa moja kwenye msingi wa kesi.

We chichiemu tulia.ukishajitia kidole matokoni kubali kunusa tu
 
mtuhumiwa mlimkamata akiwa anakunywa supu au anatembea? tayari swali hilo la wakili msomi halafu baada ya jibu hakuna kinachofuata yaani alikuwa na maana gani kuuliza swali kama hilo
Ili hawara ya bibi yako huko nyarugusu aguswe na utopolo naujinga wa zero na genge lake ambao wako central kujaza vyoo tuu.

Nyambaaff
 
Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Wengine wameonekana kuwasifia mawakili wa mtuhumiwa kwamba wana ustadi mkubwa katika kuwabana mashahidi wa upande wa mashtaka (eti hadi wanaomba kwenda msalani). Binafsi, naomba niwe tofauti. Mawakili wengi wa Kitanzania wanafanya mambo mengi kwa kukariri.
Niliwaza hivi ila nikahisi kwakuwa ikisikilizwa kwanza kesi ndogo katika kesi ya msingi nikaona bora niache kwanza, ila kwa hisia zangu naona kabisa Mh Mbowe uenda akatiwa hatiani lakini wanajaribu kuwahi asifikie huko na ndiyo maana wameenda kufungua kesi mahakama ya kimataifa kupinga kukatwa kwa Mbowe kama kulikiuka haki zake.
 
Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Wengine wameonekana kuwasifia mawakili wa mtuhumiwa kwamba wana ustadi mkubwa katika kuwabana mashahidi wa upande wa mashtaka (eti hadi wanaomba kwenda msalani). Binafsi, naomba niwe tofauti. Mawakili wengi wa Kitanzania wanafanya mambo mengi kwa kukariri.

Ningep
Ww nawe umechemka kabisa......
utakuwa law school labda......
ama mwanasheria mzembe mzembe manake mpo wengi siku hizi.....
wataalam wa cross examination
huwa wanaangalia ingredients ama elements zinazounda kosa......
mathalan kama Mbowe ameshitakiwa kwa ugaidi....
unaangalia elements zinazounda kosa hilo....
kwa hivyo unakross examine kufatana na elements hizo ili kuibua mashaka......
 
Mtuhumiwa mlimkamata akiwa anakunywa supu au anatembea? tayari swali hilo la wakili msomi halafu baada ya jibu hakuna kinachofuata yaani alikuwa na maana gani kuuliza swali kama hilo
Nyie Ni vilaza,afande Kingai alisema waliwakamata watuhumiwa wakiwa wanakunywa supu, shaidi mwingine anasema waliwakamata wakati wakiwa wanatembea, Sasa ulitaka waulizwe kuhusu wewe mtoa mada ni kwanini ni mtoto wa haramu!!!!
 
Yaani wewe ndio sifuri kabisa kwanza hujui hata kama kinachoendelea mahakamani ni kesi ndogo ya kuhusu namna ya ukamataji? Na hapo kesi ya ugaidi bado haijaanza jifunze kusoma kabla hujakirupuka
Yaani Kuna mijitu humu inajitia kujua wakati hata kesi yenyewe hawafuatilii
 
Nyie Ni vilaza,afande Kingai alisema waliwakamata watuhumiwa wakiwa wanakunywa supu, shaidi mwingine anasema waliwakamata wakati wakiwa wanatembea, Sasa ulitaka waulizwe kuhusu wewe kwanini mtoto wa haramu!!!!
Labda walikuwa wanatembea huku wanakunywa supu! Utani pembeni, huo mkanganyiko una maana na faida gani kwa Mbowe katika kesi hii?
 
Back
Top Bottom