Nadhani hujaelewa kuwa hii ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa.Katika ufuatiliaji wangu mdogo, watu wengi wameonekana kuwa na ushabiki na mihemko kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Wengine wameonekana kuwasifia mawakili wa mtuhumiwa kwamba wana ustadi mkubwa katika kuwabana mashahidi wa upande wa mashtaka (eti hadi wanaomba kwenda msalani). Binafsi, naomba niwe tofauti. Mawakili wengi wa Kitanzania wanafanya mambo mengi kwa kukariri.
Ningependa maswali yafuatayo yaulizwe, either ndani au nje ya mahakama.
1. Je, Serikali imewahi kumhukumu au kumtuhumu Mbowe kwa tukio lolote la ugaidi ambalo liliwahi kufanyika ndani au nje ya nchi?
2. Ni kawaida sana kuona vikundi vya kigaidi vikiwa na majina ya kujitambulisha. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, kikundi cha kigaidi anachodaiwa kuongoza Mbowe kinaitwaje?
3. Mbowe anajulikana zaidi nchini kama Mwanasiasa. Ugaidi kwa tafsiri ni lazima uwe na agenda fulani. Je, kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi, nini ni agenda ya kundi ambalo analodaiwa kuongoza Mbowe?
Sitegemei kama upande wa Mashtaka umejiandaa kujibu maswali ya namna hii hasa kama yataulizwa mwanzoni kabisa wa kesi. Majibu ya haya maswali kutoka kwenye vinywa vya upande wa mashtaka yana implications kubwa sana baada ya kesi, whether Mbowe amefungwa au ameachiwa huru.
Mawakili wa Mbowe, acheni kukariri kuhoji mapungufu ya technicalities. Hata kama kuna upungufu huko, kuyakomalia hayo hakuwezi kufanya kesi ifutwe kirahisi kama mnavyodhani. Nendeni moja kwa moja kwenye msingi wa kesi.
Hapa kinachotafutwa, ni je maandishi ambayo Polisi wanadai ni maelezo ya watuhumiwa, yapokelewe mahakamani kama kielelezo kwenye ushahidi, au yatupiliwe mbali.
Ndiyo maana katika kesi hii ndogo, husikii wakimwongelea Mbowe. Watuhumiwa wameeleza kuwa walilazimishwa kusaini maelezo yaliyoandaliwa na Polisi. Na katika maelezo hayo, Polisi wanadai kuwa waliambiwa na watuhiwa kuwa walikuwa wameandaliwa na Mbowe kufanya ugaidi. Nje ya maelezo hayo, Polisi hawana kielelzo kingine wala ushahidi wa kuthibitisha kuwa Mbowe amewahi kufanya mipango ya ugaidi.
Mawakili wa Mbowe wapo makini sana, na maswali yote yanayoulizwa, kwa anayejua sheria, na kinachotafutwa, ni ya msingi sana.