Mawakili wa utetezi punguzeni muda wa cross examination, kesi ya Mbowe yaweza kuamuliwa kwa haki kabisa hapa ilipofikia

Ni kweli! Lakini lazima wahoji ili kutoacha shaka yo yote kwenye Utetezi.
... na ukichunguza kwa makini utaona mawakili wa serikali kuna vitu vya msingi sana hawawaulizi mashahidi wao kwa sababu wanazozijua wao! Vinakuja kuwekwa hadharani na mawakili wa utetezi.

Mashahidi wa michongo wanatakiwa wawe screwed to the maximum extent possible sio tu kwa ajili ya utetezi wa shauri lililoko mahakamani lakini pia kupeleka "clear and loud" message kwa wahusika kwamba mipango yao ya kishetani inafahamika.
 
Shida yako ni kesi iishe mapema au haki ipatikane haya ni maisha na haki za watu.chakupambania ni haki ipatikane swala la muda halina msingi kwasababu hakunaga kesi ndogo.Kama hujui dhamira ya adui yako lazima kupambana kwa silaha kali kali hadi mwisho.
 
Mashahidi 12 wa Jamuhuri wametosha kabisa kumuonyesha jaji na ulimwengu wote kama Mbowe na wenzake wanapaswa kuachaliwa au kufungwa miaka 30 kwa hayo makosa wanayoshtakiwa nayo. Hakutakuwa na jambo jipya katika mashahidi waliobaki, labda kidogo sana aliyekiwa DCI.
 
Usisahau Mbowe hajasimama kizimbani na atadodoswa kwa miezi 6
 
Hela baba inaingia sio makelele ya bure pale mahakamani
Hela ipi inayokuuma wewe raia mnyonge?
Za mawakili wa Mbowe ambazo hazikuhusu au za mawakili wa Jamuhuri na Jaji ambazo ni kodi yako?
 
Huu ni ushauri wa kitasnia au wakisiasa? Mnataka ku-limit damage na aibu mnayoipata kutokana na Cross examination mahiri?
 
Ni vyema waulize maswali yote. Kwenye kuuliza pia unaweza ukagundua vitu kama ukiukwaji wa taratibu, mashahidi wengine haswa maaskari wanaweza shitakiwa baada ya hii kesi kupitia shahidi zao n.k
Hakuna shahidi wa upande wa Jamuhuri atakayeshitakiwa baada ya hii kesi kwisha.
 
Waendelee tu kuwahoji hawa mashahidi wa mchongo. Tungejuaje kuwa kwa jeshi la polisi mtu akitamka neno "Muda Umeisha" kwao huo ndio Ugaidi wenyewe. Basi Tanzania hii yote imejaa magaidi. Hata Jaji mwenyewe basi ni gaidi maana kuna siku aliwaambia mawakili wasirudie walichokisema wengine ili kuokoa muda, yaani muda usiishe bure.
 
Waendelee tu na muda mrefu. Maana maswali mengi hufanya muongo na mpandikizwa kujulikana
 
Lazimz tuhakikishe Jaji hapati kigugumizi cha kufutilia mbali hii kesi. Kila kitu kiwe wazi. Hii kesi imekuwa darasa.
Haitakaa itokee kwa mahakama ya Tanzania ya sasa Jaji kufuta kesi kama hii inayotokana na siasa.
Mwenye kuweza kuifuta ni serikali tu kupitia DPP.
 
Waendelee tu na muda mrefu. Maana maswali mengi hufanya muongo na mpandikizwa kujulikana
Wakiendelea hivi kesi itamaliza mwaka wote huu, hata mawikili wa utetezi watachoka.
 
Wafadhili wao wametoa Hela nyingi, ndio maana wanafanya hivyo kuwaridhisha
 
Cross examination ndiyo njia pekee ya kuona namna kesi ya mchongostic ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…