Mawaziri akiwemo Waziri Mkuu, wanalipwa perdiem wawapo Bungeni kwa kigezo gani ili hali wanakaa katika nyumba za Serikali Dodoma?

Ni rahisi tu kupata majibu ya hili tukufaham majawabu ya haya:
Mwajiri wa Mbunge ninani, na Ofisi ya Mbunge inapaswa kuwa wapi?
Kwangu Mimi, kituo Cha kazi Cha Mbunge ni Kule alikochaguliwa. Uwaziri ni jukumu la matokei ya ubunge wake.
Kwaiyo, wanastahili kulipwaaaaa.
 
KATIBA MPYA NI SASA
 
Naunga mkono hoja
 
Tukijadili posho za Rais, waziri mkuu, mawaziri, jaji mkuu, spika, wakuu wa vyombo vya ulinzi na wengine wenye mamlaka kama hayo, ni vigumu kupata ukweli halisi.
Hawa wanaweza kujipangia pesa nyingi sana, zinazojulikana na zisizojulikana.
Cha muhimu ni kupambana nao waongoze kwa haki na uadilifu katika mambo ya wazi.
Kipaumbele kiwe kuwadhibiti kama wakitoa maamuzi ya hovyo, yasiyo ya haki na yaliyo kinyume na katiba au sheria, hayo ya vipato yatakuwa yamekwisha moja kwa moja.
 
Lakini mbona wenzetu wanawaadhibu viongozi wao kwa matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo ubadhirifu wa fedha, rushwa na kujilimbikizia mali, wao wanajuaje kuwa hawa jamaa wanakula kuliko urefu wa kamba zao?
 
***** zao, wanatukamua tozo kila uchwao ili wajineemeshe wao na familia zao
 
Tatizo mambo haya huwa tunakosa wa kutusemea hata wale tunaoamini ni watetezi wetu hukuti kupigia kelele masuala haya.
Iko hivi, hii nchi ina watu ambao akili zao zimelala sana. Unaweza kumtetea mtu maskini ili apate haki yake halafu mtu huyohuyo anayetetewa anakuponda vibaya. Hivyo acheni wakae Kimya tu, tena baada ya kuona wananchi wengi hawajielewi nao wameona waunge tu juhudi wapambanie familia zao.

Kina Zito, Mdee na wenzake wa Covid 19, Kafulila, Mbatia, Mbowe, Lisu, Lema, Kitila Mkumbo, Nassary, Msigwa, Heche, Wilbroad Slaa, Waitara nk nk nk nk ukifuatilia siasa zao za nyuma kwa kiasi kikubwa unashawishika kuwa walikuwa na dhamira ya kweli LAKINI BAADA YA KUCHOSHWA NA UMBUMBUMBU WA WATU ambao hawajielewi hata 1/4 nao wameona waunge juhudi waziwazi na wengine wanaunga juhudi nyuma ya bazia kimyakimya.
 
Tatizo yeye kakuta huu mfumo na nina imani haujaanza juzi au jana tuwangoje wajuaji waje kufafanua
 
Ungekia waziri usingesema yote haya
 
Huyo Heche aache unafiki. Zito kabwe aliwahi jieleza wabunge uharali wa kutopokea hiyo posho ya "Makalio"

Hao hao kina Heche waliungana na upande wapili kumshambulia Zito nakumuita majina mabaya.

Leo anataka kutushawishi tumuonee huruma? Kwani Chadema haikua nawa bunge wanao ishi Dododoma?
 
Bungeni ni sehemu ya kazi, tena yeye ndio msimamizi mkuu wa shughuli za serikali bungeni so ni sehemu ya ofisi yake. Hastahili kuwa na perdiem...
Bungeni ni sehemu ya kazi. Wabunge wa Chadema hiyo hoja waliikataa.
Kumbuka posho ya waziri mukuu, ni sawa na ya kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…