Mawaziri akiwemo Waziri Mkuu, wanalipwa perdiem wawapo Bungeni kwa kigezo gani ili hali wanakaa katika nyumba za Serikali Dodoma?

Huwa tunahangaika na vijizi vodogovidogo wakati mafisadi wakuu wapo pale juu kileleni na wakijiona ni halali wao kutuibia watakavyo!
 
Hayo unayotaka yaondolewa inatakiwa tupate rais jiwe na chizi chizi Kama mwendazake
 
Tz Bado inauchumi mdogo, mishahara inapanda lingana na uchumi😀 ,nchi ngum sana
 
HALAFU WAKIFANYA WENGINE HIVI VITENDO HAO HAO WANALETA NONGWA KWELI KWELI....NI TABIA ZA KIBINAFSI TU, KUJILIMBIKIZIA PESA ZA UMMA PASIPO HALALI, UNYONYAJI MKUBWA KABISA, HALAFU WAKIHUTUBIA UTAFIKIRI WATU
 
Haya mambo yaliwachanganya waliokuwa wazalendo toka kitambo tu ikabidi wayaache hivyo hivyo, kwa sababu hakuna mwenye majibu yasiyo na lakini.
 
Huo ni wizi na ufisadi uliohalalishwa kisheria.
 
Hivi ikiwa wanalipwa mishahara ya ubunge kama kazi yao tuliyowaajiri
sasa hizi posho za nini Tena kwenye vikao.
Ni matumizi mabovu tu ya fedha za umma na hakuna justification yoyote ya wao kulipwa hizo posho.
 
Lakini mbona wenzetu wanawaadhibu viongozi wao kwa matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo ubadhirifu wa fedha, rushwa na kujilimbikizia mali, wao wanajuaje kuwa hawa jamaa wanakula kuliko urefu wa kamba zao?
Katiba yetu, utamaduni wetu na fikra mbaya za wananchi walio wengi zinawafanya viongozi wetu kufanya hayo bila kuogopa. Hali hii huvifanya vyombo vya dola kuwa kama mbwa wa viongozi hao na hivyo kusababisha kuadhibiwa kwao kuwa kugumu.
Hivyo basi, kwa kuanzia ni muhimu kukemea pale wanapovunja katiba na sheria.
Hayo mengine yatarekebika moja kwa moja.
 
Kukemea kwa njia zipi zaidi ya hizi za kwenye mitandao ya kijamii ?
 
Ndio maana huwa tunasema hao wanaSihasa lao huwa moja tu! Wanatucheza shere tu sisi wananchi !!
 
Wanasema eti ni wivu tu na fikra za kimaskini
Atakaesema hivyo atakuwa ni mjinga, POPOMA, asie mzalendol wala kuwaonea huruma wale wanaoishi kwa kuunga, wale ambao hata ugonjwa wa elfu anashindwa kujipatia matibabu sahihi sababu ya kipato.

Tanzania ni yetu sote, mimi kuupata ugali maharage kusinifanye nisijisikie vibaya kwa wenzangu ambao hawapati hata kikombe cha uji kwa uzembe wa watu waliopo madarakani
 
Hapana. Mawaziri hawalipwi perdiem wakiwa Dodoma kwa kuwa wapo nyumbani. Wabunge wengine wasio mawaziri ndio hulipwa perdiem. Pokea taarifa hiyo tafadhali
 
Kwa hiyo waziri Mkuu Ni Sawa na Baba yako.
 
Hapana. Mawaziri hawalipwi perdiem wakiwa Dodoma kwa kuwa wapo nyumbani. Wabunge wengine wasio mawaziri ndio hulipwa perdiem. Pokea taarifa hiyo tafadhali
Nashukuru kwa maelezo yako yanayolenga kujibu hoja hii.


Swali ni nani tumuamini kati ya wewe na John Heche?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…