Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Kumekuwa na tabia iliyozoeleka ya mawaziri kuagiza makampuni na mashirika yaliyo chini ya wizara zao kutoa fedha kugharimia miradi mbalimbali bila utaratibu wa kisheria. Lakini kuna uwezekano mkubwa pia mawaziri huwa wanachukua fedha kutoka makampuni na mashirika kwa ajili yao binafsi! Huu ni ufisadi na lazima ukemewe vikali.
Athari tunazopata wananchi ni kuwa makampuni na mashirika hayo hupandisha gharama za vitu au huduma zao ili kufidia fedha wanazotoa bila utaratibu wa kisheria.
Wananchi tunapolalamika kuhusu ughali wa vitu au huduma tunazopata, mawaziri hutupuuza kwa sababu ya fedha ambazo tayari wanakuwa wamechukua kama rushwa.
Ni majuzi tu tarehe 15/7/2024 Waziri Nape alisema atachukua shilingi milioni 300 kutoka makampuni ya simu ili kugharimia ujenzi wa soko la Kashai mjini Bukoba. Fedha hizi atakazochukua siyo tozo wala kodi na wala siyo msaada ambao makampuni yalipanga kuzitoa kwa utaratibu wao wa kusaidia jamii, bali ni fedha zitakazotolewa kwa amri ya Waziri. Kitakachofuata ni kwa makampuni kutafuta njia za kuzirejesha fedha zao kwa kuwatoza wananchi moja kwa moja au kwa kutoa huduma hafifu!
Huu ni ufisadi na unapaswa kukemewa vikali!
Wananchi hatuna budi kuamka na kuanza kuwàkemea viongozi wanaotusababishia kuongezeka kwa gharama za maisha.