Pre GE2025 Hatima ya Walimu Wasio na Ajira (NETO) kujulikana baada ya siku 45, wapongeza 4R za Rais Samia

Pre GE2025 Hatima ya Walimu Wasio na Ajira (NETO) kujulikana baada ya siku 45, wapongeza 4R za Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Mawaziri George Simbachawene (Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) na Prof. Adolf Mkenda (Elimu, Sayansi na Teknolojia) wamekutana na viongozi wa Chama cha Walimu Wasio na Ajira (NETO) kujadili hatua za kutatua changamoto ya ajira kwa walimu.

==

Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO), Joseph Kaheza, amesema umoja huo umeendelea kuwa na mshikamano katika kudai ajira kwa walimu waliokosa nafasi za ajira.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 13, 2025 , Kaheza ameishukuru serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa kulipa suala hilo uzito mkubwa na kuhakikisha linapewa kipaumbele cha kitaifa.

Amesema Waziri Simbachawene aliwakutanisha na mawaziri wa wizara tatu pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ili kujadili namna bora ya kushughulikia changamoto ya ukosefu wa ajira kwa walimu.

Ameeleza kuwa NETO inapongeza falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa imechangia kufanikisha mazungumzo kati ya walimu wasio na ajira na serikali.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NETO, Mwalimu Daniel Edward Mkinga, amesema katika kikao hicho, walimu waliwasilisha nyaraka yenye kurasa zaidi ya 22 inayoelezea changamoto wanazokutana nazo tangu hatua ya usaili hadi mwisho wa mchakato wa ajira.

Amesema katika mazungumzo hayo, walijadili mabadiliko ya mitaala, mfumo wa usaili wa walimu, umri wa kustaafu, na uzalishaji wa walimu, ambapo serikali ilikubaliana kuunda tume maalum ya wizara tano itakayoshughulikia changamoto hizo.

Ameeleza kuwa Waziri Simbachawene aliwataka walimu kuwa na subira kwa siku 30 hadi 45, wakati tume hiyo ikifanyia kazi masuala waliyowasilisha.

Ametaja wizara zinazohusika katika mchakato huo kuwa ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na Wizara ya Fedha.

Amesema moja ya mafanikio yaliyopatikana mara moja ni utatuzi wa changamoto ya walimu wa somo la Uchumi, ambao awali hawakupata nafasi ya kufanya usaili, ambapo mawaziri husika waliidhinisha kibali cha kuanza kwa usaili huo mara moja.

NETO imewataka walimu na wananchi kwa ujumla kuwa na uvumilivu na kushirikiana na serikali, kwani hatua zinazochukuliwa ni za msingi



Pia, Soma
 
Wanachekesha, haijulikani wanataka nini wapewe. Kama vipi wageuke chawa kama vile vikundi vya chawa wa mama, nyuki wa mama. Wanawake wa samia, TK movement, vikundi vya fursa za mama na vikundi vingine vya kichawa kuelekea uchaguzi mkuu huenda wakavuna pesa za kampeni huko. vijana wa hovyo sana hawa
 
Wameanza uchawa.

WhatsApp Image 2025-03-06 at 1.27.19 AM.jpeg
 
Hatutashangaa kuona vikundi vingi vya kichawa vikianzishwa kuelekea uchaguzi mkuu kwa ajili ya kampeni kabambe
 
Wakati CHADEMA ikikomaa na NO REFORM, NO ELECTION, ACT WAZALENDO nao wamekuja na mpya kususia vikao vya umoja wa vyama vya siasa kwa madai kama ya CHADEMA, CCM wao wako busy kubuni mbinu za kunasa makundi mengi ya wananchi waisapoti na kuipa kura nyingi uchaguzi mkuu. Wanabuni vikundi vya ajabuajabu kama wadudu wa Arusha, wapuuzi wa NETO, wanawake wa samia, vikundi vya walemavu, mama/baba lishe, wapaa samaki, washindilia vitunguu kwenye magunia, wajasiriamali wa aina zote, motivation speakers, ma MC, ma producer, wasanii wa fani zote, ma DJ, vikundi ni vingi na orodha ni ndefu, CCM imejipanga kwa kampeni kabambe, wanakuambia UTU NA KAZI, TUNASONGA MBELE. Kiufupi CCM tayari wako mbele kwenye kampeni kabla muda rasmi haujaanza. Kwa hali hii hawa hata wakishinda ni halali yao kwa jinsi strategy ya kupata kura wanayoipata. Nafuatilia na nahudhuria abrakadabra zao nyingi wanazoziandaa kujiweka tayari kwa kampeni na kuvuna kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu. Wapinzani bado wamezubaa sana,
 
Wanakutana na Viongozi kujadili hatua ? Au kwenye Udhia kupenyeza Rupia ?; Anyway hili janga / time bomb sio kwa waalimu tu bali Taifa kwa ujumla na tunachofanya ni delaying the inevitable...
 
Mara nyingi viongozi ndo humaliza wenzao
 
Back
Top Bottom