Mawaziri waliotemwa katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Agosti 30, 2023 amefanya mabadiliko Baraza la Mawaziri ambapo Waziri mmoja na Manaibu wawili wameachwa na nafasi zao zimechukuliwa na wengine.


Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula

Miongoni mwa walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula ambaye nafasi yake imechukuliwa na Jerry Silaha Mbunge wa Ukonga.


Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja

Pia, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja naye ameachwa huku nafasi hiyo ikichukuliwa na Dunstan Kitandula.


Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ambapo kwa sasa wizara hiyo imegawanywa mara mbili; upande wa Ujenzi Rais Samia amemteua Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri na Uchukuzi amemteua David Kihenzile kuwa Naibu Waziri.

Mabadiliko haya yanatokea ikiwa ni siku 56 tangu afanye mabadiliko madogo katika baraza hilo kwa kuigawa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuunda Wizara tatu; Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Ambapo alimteua Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.

Pia alimteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha.
 
Atupele Mwakibete halali yake kutemwa hajafanya chochote jimboni kwake

Barabara ya kutoka Katumba hadi mwakaleli taabu tupu wakati hiyo barabara ndiko kunatoka gesi na chai inayoingizia Chi pesa za kigeni kwa wingi

Yaani serikali inavuna pesa kule lakini kutengeneza barabara hawataki na Mwakibete wao
 
Hawa wote ni Wasukuma. Mama anaswagia Sukuma gang ziIzini kwa amri ya IGP
 
Hata mimi mkulima wa Parachichi pale Suma Nditu nakubaliana na wewe. Ukitaka kwenda Lwangwa kwa njia hiyo ukiwa na gari ndogo ni almost haiwezekani
 
Hata mimi mkulima wa Parachichi pale Suma Nditu nakubaliana na wewe. Ukitaka kwenda Lwangwa kwa njia hiyo ukiwa na gari ndogo ni almost haiwezekani
Yaani kabisa kuna mandizi pia kibao yanaenda mikoa yote bado barabara serikali haitaki kutengeneza sehemu yenye uchumi mkubwa kama hiyo wanatengenezea barabara mitaani za wauza maandazi na vitumbua wa dar es salaam
 
Mabadiliko kila baada ya siku 56. Ukiwa na bahati. Huu umeshakuwa mchezo.
 
Lakini ubunge wake si unabaki kwa maana ya kwamba ataendelea kuwawakilisha? Au alivyotolewa uwaziri sasa barabara itajengwa kwa kiwango cha lami?
 
Daah
 
Ni mpishano tu kuna mkeka inakuwaga na muslim wengi kuzingi Wagalatia wenye nchi
 
Hata tupangue vipi hizi wizara, kama hatutoacha mfumo ufanye Kazi inavyotakiwa basi haya mabadiliko hayana maana.
Upanguaji kwa nafikiri unaangalia tu yupi anawafaa viongozi wa juu sio kule kwa wananchi kuwa kawasaidia nini au atawasaidia nini wananchi wa kawaida mfano ni hiyo barabara .Labda sasa kabaki.mbunge labda atapiga miyowe labda

Barabara ya kule jimbo la Mwakibete Katumba hadi Mwakaleli hovyo lakini akapewa cheo cha unaibu waziri
 
Huyo nae mzembe kweli acha wamteme
 
Kuna kitu labda kashtuka
Kuwa kuna mahali watu wanamdanganya na kumpeleka kusiko na minong'ono yao ya kumnong'oneza ya uongo

Uongo na udanganyifu huwa una mwisho

Mtu hadanganyiki milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…