Mawazo ya ndugu kujiona entitled ni lazima wasaidiwe na waliofanikiwa husababisha kuridhika, uvivu, umasikini zaidi. Nazipongeza jamii zenye mipaka.

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Ni tabia iliyo kwenye default settings kwa baadhi ya watu kwamba ndugu akifanikiwa basi ni lazima wasaidiwe mpaka kiama.

Yani kinyume na hapo hata ukipunguza msaada aidha kwa matatizo yako ya kifamilia, marejesho ya mkopo, n.k. kelele zinaanza anajitenga, anaringa, mke wake kamnunulia gari, n.k. ni kelele na maneno.

Na hata uwe tajiri, Tabia hii kwa ndugu wanaoomba msaada kugeukwa kuwa sugu kama uraibu unaohitaji dozi ya ziada, matatizo yataanza kutengenezwa.

Misaada iwe na lengo la maendeleo mfano mtaji, kusomesha, kukodi shamba, n.k. lakini unakuta watu hata baada kuwapa mitaji wanaila wanarudi kukutegemea, umepeleka shule hawapo serious, umekodi shamba badowanaendelea kuomba misaada, n.k. lengo la msaada ni lipi ?

Ndio maana ukichunguza jamii zilizoendelea huwa kuna mipaka kwenye kusaidiana, mambo ya kutembeleana ni kwa wiki kadhaa mtu anarudi kuendelea kupambana na maisha, unasaidiwa na kuchangiwa mtaji kwa mategemeo utajikomboa kiuchumi sio kuanza kuomba omba misaada kila mara, n.k.
 
Usipotaka kusaidia Ndugu zako unataka usaidie watu gani?
Kila kitu kinapita hapa duniani, Ukiwa na uwezo wa kusaidia saidia 10000X10000.....
 
Hata biblia inataka usaidie ndugu au familia. Wewe ni nani upingane. Unakuta unapesa ila mama yako anahangaika, au mdogo wako anateseka kupata mtaji,sasa pesa za kazi gani hizo?!.

Cha msingi ni kuwashika mkono,sio unampa pesa ya biashara na biashara hajui unategemea nn?. Mtrain mkopeshe pesa umsimamie,wazazi nao waishi kama peponi.
 
Huzikwi navyo Ndugu saa nyingine ukipata sio kwamba wewe una akili au umepambana sana kuliko wenzako.... Sasa una pesa na huwapi Ndugu connection Kuna faida gani? Narudia connection siyo pesa.... Au nyie ndo wale unataka uabudiwe na ukoo mzima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…