Mawazo yangu kuhusu Bilionea wa Tanzanite

Mawazo yangu kuhusu Bilionea wa Tanzanite

msani

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Posts
1,801
Reaction score
1,191
Nimejaribu kufanya Hesabu Zangu za Darasa la 7 D kuhusu huyu Bilionea mchimbaji mdogo wa madini.

Hebu Twende Sawa Hapa na hesabu za Darasa la saba!!

Tanzanite thamani yake hupimwa kwa Carats.

1 Carats = 0.0002kg

Je 15kg ni sawa na ngapi?

= (15kgs x 1 carats) gawa kwa 0.0002kg

Hapa jibu ni = 75,000 Carats.

Kwa hapa chini nakuambatanishia bei za Carats ambazo ni kuanzia $500 -$1500 kwa carats.

Basi tuchukue Carats moja ni sawa na $500.

Thamani= 75000 carats x $500/Carats

= $37.5M

Sasa nimepita hapa Equity Bank nimekuta Exchange Rates kwa 1 USD($) ni 2345

Basi tuzidishe ili tupate kwa hela za Tz.

= $37,500,000 x 2345(TZS/$)

= TZS 87,937,500,000
Makadirio= TZS 87 Bilioni.

Mchimbaji kapewa TZS 7.8 Bilioni na zilizobaki ni Kodi ya Serikali?
 
Nimependa tu picha yake mambo mengine watajua wao...
tapatalk_1592992013965.jpg
 
Mkuu kwahiyo Kati yako na laizer Nani anajua Bei ya tanzanite.. kwahiyo unataka kutuaminisha hapa kuwa muda wote huo alioanza Kazi ya kuchimba tanzanite hajawahi kufahamu Bei yake?

Je, unafikiri yeye kabla ya kuuza huo mzigo mnono hakufanya ufuatiliaji wowote juu ya soko na Bei ya tanzanite ndani na nje ya nchi?

Watanzania tupunguzeni unafiki na uchochezi usiokuwa na maana.
 
Mkuu madini ni pasua kichwa sana,

Huwa wanathaminisha ubora kwa ugumu, kutokuwa na mipasuko na rangi ,na kama limekatwa basi wanaangalia na aina ya mkato.

Hizo kilo zote sio zitakazouzwa, lazima uzito uwe pungufu.
 
Back
Top Bottom