Mawazo yangu kuhusu Bilionea wa Tanzanite

Mawazo yangu kuhusu Bilionea wa Tanzanite

Nimejaribu kufanya Hesabu Zangu za Darasa la 7 D kuhusu huyu Bilionea mchimbaji mdogo wa madini.

Hebu Twende Sawa Hapa na hesabu za Darasa la saba!!

Tanzanite thamani yake hupimwa kwa Carats.

1 Carats = 0.0002kg

Je 15kg ni sawa na ngapi?

= (15kgs x 1 carats) gawa kwa 0.0002kg

Hapa jibu ni = 75,000 Carats.

Kwa hapa chini nakuambatanishia bei za Carats ambazo ni kuanzia $500 -$1500 kwa carats.

Basi tuchukue Carats moja ni sawa na $500.

Thamani= 75000 carats x $500/Carats

= $37.5M

Sasa nimepita hapa Equity Bank nimekuta Exchange Rates kwa 1 USD($) ni 2345

Basi tuzidishe ili tupate kwa hela za Tz.

= $37,500,000 x 2345(TZS/$)

= TZS 87,937,500,000
Makadirio= TZS 87 Bilioni.

Mchimbaji kapewa TZS 7.8 Bilioni na zilizobaki ni Kodi ya Serikali?

wamemkata kabisa kodi na hela ya CSR.coperate social responsility au. Ila mkuu siiamini hiyo calculation yako.kwa nini jamaa asiuze kwenye soko la madini? Au serikali wamelazimisha awauzie?
 
wamemkata kabisa kodi na hela ya CSR.coperate social responsility au. Ila mkuu siiamini hiyo calculation yako.kwa nini jamaa asiuze kwenye soko la madini? Au serikali wamelazimisha awauzie?
Hata mimi sijui mkuu,nilijaribu kufanya hesabu tu
 
Unaweza kuta jamaa anamalimbikizo ya madeni ya kodi kwenye vitalu vyake vya uchimbaji kwahiyo kilochopatikana nimali ya serikali yeye ni amelipwa hio kama labour cost
 
Mimi mwenyewe kwa hizo kilo na hiyo bei ndogo kwa nini wasingemwacha akauza kwa wahitaji mwenyewe kama ni kodi akalipa stahiki na hili la kumtangaza mtu naona kama ni kuhatarisha maisha yake mana inabidi aishi kama digi digi na ulinzi juu hapo bado ndugu jamaa na marafiki hawajaja kulia shida
 
Hapana si kweli, Tanzanite haiuzwi tu kwa kupima uzito vipo vigezo vingi vya kuithaminisha,naweza kuwa na gram 1 yaTznite nikauza lets say 500k na mwingine akawa na gram 10 akauza elfu 10 (kulingana na ubora) jiwe pekee linaloweza kuwa na fixed price ni dhahabu angalau ikipishana bei ni kiduchu sana kulingana na purity...ni darasa pana kidogo ingawa haliitajii zaidi elimu ya darasani
 
Mimi sijapenda walivyomtangaza kwenye vyombo vya habari. Kuhusu ndugu, jamaa na marafiki watakaomiminika kwenda kukopa na kulia shida ni wengi sana
 
Hapana si kweli,Tanzanite haiuzwi tu kwa kupima uzito vipo vigezo vingi vya kuithaminisha,naweza kuwa na gram 1 yaTznite nikauza lets say 500k na mwingine akawa na gram 10 akauza elfu 10(kulingana na ubora) jiwe pekee linaloweza kuwa na fixed price ni dhahabu angalau ikipishana bei ni kiduchu sana kulingana na purity...ni darasa pana kidogo ingawa haliitajii zaidi elimu ya darasani
Sasa kwanini wasilichambue hilo jiwe kwanza kisha waje na hesabu kamili kuliko kununua hivyo lilivyo? Kwani kuna haraka gani hapa?
 
Back
Top Bottom