Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Naipongeza sana JamiiForums kupata seat hapo.Kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Balozi Adadi Mohammed Rajab kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, na Bi. Fatma Mohammed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (MB.), kwa Mamlaka aliyopewa na Ibara ya 8(2) ya Sheria ya Ulinzi wa Tarifa Binafsi Na. 11 ya 2022, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kipindi cha miaka 3;
1. Bw. Ramadhan Athumani Mungi, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi;
2. Bw. Edward Samweli Lyimo, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Benki ya Biashara ya Taifa (NBC);
3. Bw. Hamid Haji Machano, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Zanzibar;
4. Bi. Frida Peter Mwera; Mwandishi wa Sheria Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali; na
5. Bw. Maxence Melo Mubyazi, Mkurugenzi Mtendaji, Jamii Forums;
Uteuzi huu unaanza leo tarehe 18 Disemba, 2023 hadi tarehe 18, Disemba 2026.
View attachment 2846438
Nampongeza Maxence Melo kwa kuaminiwa na kutruliwa. Sina shaka naye hata kidogo kwani anajua kujenga hoja na ana ushawishi wenye tija.
Tunatarajia wajumbe wa Kamati hii watatimiza majukumu yao kwa maslahi mapana ya Taifa.
Mungu awatangulie