Maxence Melo ateuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Balozi Adadi Mohammed Rajab kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, na Bi. Fatma Mohammed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (MB.), kwa Mamlaka aliyopewa na Ibara ya 8(2) ya Sheria ya Ulinzi wa Tarifa Binafsi Na. 11 ya 2022, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kipindi cha miaka 3;

1. Bw. Ramadhan Athumani Mungi, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi;

2. Bw. Edward Samweli Lyimo, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Benki ya Biashara ya Taifa (NBC);

3. Bw. Hamid Haji Machano, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Zanzibar;

4. Bi. Frida Peter Mwera; Mwandishi wa Sheria Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali; na

5. Bw. Maxence Melo Mubyazi, Mkurugenzi Mtendaji, Jamii Forums;

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 18 Disemba, 2023 hadi tarehe 18, Disemba 2026.
View attachment 2846438

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 18 Disemba, 2023 hadi tarehe 18, Disemba 2026.[emoji173][emoji173][emoji173][emoji1548]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ugomvi wangu ulikuwa na mwendazake, na ameshafwariki
Kwa hiyo huko siasa hata siendagi tena.
Niko humu kuwazodoa mambulula....sioni tatizo kwa teuzi....
 
Ukiwa na hela,utaitwa kijana milele,mfano;January Makamba,Mo Dewji,Nape,Ridhiwani,Zitto Kabwe n.k,ila ukiwa huna hela ukifikisha miaka 36,utaitwa mzee,yaani rika la Makamba sr.
Hapo nimekupata vizuri kiongozi 👏
 
ALIYETAZAMWA KAMA ADUI WA SERIKALI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA BODI NYETI!

Baada ya miaka kadhaa ya kuandamwa na kesi akishtakiwa na Jamhuri, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo Mubyazi sasa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi katika moja ya Mamlaka za Serikali. Kwa muono wetu sisi, uteuzi wake si hisani bali Serikali imeona ujuzi na uelewa wake katika eneo husika kwani Melo amekuwa mstari wa mbele kupazia sauti juu ya haki ya taarifa binafsi za watu.

Je, nani ajuaye kama Yericko Nyerere na Dkt. Chris Cyrilo siku moja watalishauri Baraza la Usalama la Taifa? Kama mtu humjui Dkt. Chris Cyrilo, akatafute kitabu chake cha: 'Istilahi za Uhalifu na Usalama'! Je, huo ndio muelekeo mchapuko (paradigm shift) wa Rais Dkt. Samia katika kushirikisha watu walio nje ya Serikali Je, una neno gani kwa Max Melo Mubyazi? Je, ni nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 18 Desemba 2023; 4:21 usiku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maxcene anafit haswa hata juzi niliandika hapa kuwa anastahili but alipaswa awe Mwenyekiti na siyo mjumbe. Hongera kwake
 
Hapo nimekupata vizuri kiongozi [emoji122]
Sikubaliani na ki2c hususani kuhusu #Mo Dewji. Huyu jamaa yeye hujitangaza mwenyewe. Anayefahamu anisahihishe Kwa kuwa Kila mwaka jarida kubwa barani na kichwa la habari la ujana na utajiri wake . Matajari Africa wanafanya makubw ila kijana wetu b20 na Simba mgogoro Kila kukicha Kuna nini na tajiri wetu mdogo Afrika tangu 2004. Inamaana Bara nzima hakuna uzalishwwaji wa vijana matajiri. Mbona juzi dewji foundation ya tajiri mdogo Afrika imefungiwa n Jamhuri [emoji41][emoji2539]
 
Mbona mambo ni Mengi aisee 🤔
 
ALIYETAZAMWA KAMA ADUI WA SERIKALI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA BODI NYETI!

Baada ya miaka kadhaa ya kuandamwa na kesi akishtakiwa na Jamhuri, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo Mubyazi sasa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi katika moja ya Mamlaka za Serikali. Kwa muono wetu sisi, uteuzi wake si hisani bali Serikali imeona ujuzi na uelewa wake katika eneo husika kwani Melo amekuwa mstari wa mbele kupazia sauti juu ya haki ya taarifa binafsi za watu.

Je, nani ajuaye kama Yericko Nyerere na Dkt. Chris Cyrilo siku moja watalishauri Baraza la Usalama la Taifa? Kama mtu humjui Dkt. Chris Cyrilo, akatafute kitabu chake cha: 'Istilahi za Uhalifu na Usalama'! Je, huo ndio muelekeo mchapuko (paradigm shift) wa Rais Dkt. Samia katika kushirikisha watu walio nje ya Serikali Je, una neno gani kwa Max Melo Mubyazi? Je, ni nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 18 Desemba 2023; 4:21 usiku

Sent using Jamii Forums mobile app
"Kwa muono wetu sisi, uteuzi wake si hisani bali Serikali imeona ujuzi na uelewa wake katika eneo husika kwani Melo amekuwa mstari wa mbele kupazia sauti juu ya haki ya taarifa binafsi za watu". Uko sahihi sana. Melo ameonesha kwa vitendo na kwa ujasiri mwingi kulinda taarifa za watu. Aidha, ametumia muda mwingi kuishinikiza Serikali ianzishe hii Tume. Kwangu binafsi ni mtu sahihi sana kuwemo kwenye bodi ya Tume hii mpya kwa ajili ya kutetetea maslahi ya Sekta binafsi. Nikutakie kazi njema na Mwenyenzi Mungu akuzidishie ujasiri kutetea ulinzi wa taarifa binafsi za watu.
 
Kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Balozi Adadi Mohammed Rajab kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, na Bi. Fatma Mohammed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (MB.), kwa Mamlaka aliyopewa na Ibara ya 8(2) ya Sheria ya Ulinzi wa Tarifa Binafsi Na. 11 ya 2022, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kipindi cha miaka 3;

1. Bw. Ramadhan Athumani Mungi, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi;

2. Bw. Edward Samweli Lyimo, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Benki ya Biashara ya Taifa (NBC);

3. Bw. Hamid Haji Machano, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Zanzibar;

4. Bi. Frida Peter Mwera; Mwandishi wa Sheria Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na

5. Bw. Maxence Melo Mubyazi, Mkurugenzi Mtendaji, Jamii Forums;

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 18 Disemba, 2023 hadi tarehe 18, Disemba 2026.
View attachment 2846438

Akili nyingi. Hapa kinachotengenezwa ni kumgombanisha Melo na wana JF kwa kujenga taswira ndani ya wana JF kutokuwa na imani tena na Mkurungezi.

Hii itapelekea watu kuogopa kwa kuhofia sasa threads au comments zao zitakuwa chini ya uangalizi mkubwa na kufatiliwa kwa ukaribu.

Waswahili wanasema ukitaka umpatie mchawi mpe mtoto wako akulelee..

Yote kwa yote kila la Kheri Ndugu Mexence Melo.
 
Nenda Maxence, ila usikubali kuyumbishwa au kubadiri misimamo yako ya haki!
 
Back
Top Bottom