Mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Lowassa, Februari 17, 2024

Mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Lowassa, Februari 17, 2024

Demokrasia ina gharama zake tusiogope kuzibeba

Siyo siri kwamba Lowasa alikuwa mwanachama wa Chadema

Ni hilo tu

Mfungapo Kwaresma Msiwe kama Wanafiki Wenye Nyuso za Kukunjamana 😙
 
Demokrasia ina gharama zake tusiogope kuzibeba

Siyo siri kwamba Lowasa alikuwa mwanachama wa Chadema

Ni hilo tu

Mfungapo Kwaresma Msiwe kama Wanafiki Wenye Nyuso za Kukunjamana 😙
1708145013998.jpg
na ndiyo ukkweli wenyewe
 
1708145054581.jpg

Unafiki, uongo, fitna, majungu na siasa za majitaka za wanasiasa uchwara na chawa wao ndio zimetufikisha hapa leo.

Na kweli wamemdhalilisha na kumchafua kweli kweli, alaf leo wanajitokeza kudai eti mama yake na Lowasa alikuwa mwalim wao miaka 41 iliyopita. Siku zote za kumchafua hili swala hawakuliongelea 🤣🤣🤣

RIP Lowasa ulieitwa fisadi na wanafunzi wa mama yako.
 
Kujiuzulu kwa Lowassa ni Sawa na kustaafu kwa manufaa ya Umma

Nyie Vijana haya mambo hamuyaelewi kwa kina😀
Hapana, Mrema alipojiuzuru alinyang'anywa kila kitu humohumo bungeni Dodoma na alitembea kwa mguu kwenda nyumbani kwake Area D, wakati anatembea kwa mguu alitokea msamalia mwema akampa lifti, bahati mbaya akakamatwa.
Kujiuzulu ni kuacha kazi kwa hiari unapoteza haki zako zote na unatakiwa umlipe mwajiri wako labda kama umetoa notisi ya miezi mitatu hautamlipa.
Tuache kushuhudia upotoshaji wa makusudi.
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Zamani wa Monduli (CCM) Hayati Edward Lowassa anazikwa leo Nyumbani kwake, Monduli. Mazishi haya yamehudhuriwa na viongozi wakuu wa Nchi wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Waombolezaji wametoa Salamu za Mwisho kwenye Jeneza la Hayati Lowassa, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kisha famili ya Lowassa, viongozi wengine wa kitaifa pamoja na Viongozi waandamizi kutoka vyama vya upinzani, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe.

Mazishi haya yataendeshwa kwa Sehemu mbili, Kidini na Kiserikali. Kwa upande wa Dini, Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa ataongoza ibada hiyo, kisha Jeshi la Wananchi la Tanzania litashiriki sehemu ya pili ya Mazishi hayo.

Kwa mujibu wa taratibu za Kijeshi, Hayati Lowassa atapigiwa mizinga 17 kwa heshima yake.

Saa 6:25 Mchana, Maafisa wa JWTZ wenye cheo cha Kanali wanauingiza Mwili wa Hayati Lowassa Kaburini.

Waache "WAFU" wazike "WAFU" wao...
 
R I P

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
CCM ni kundi kubwa sana la watu wasio na haya.

Jinsi walivyokuwa wanamtusi, wanamnyanyasa Lowassa na familia yake, walivyomuita "maiti", wakamtweza kwa Kila Hali, leo wanajifanya kububujikwa na machozi.

CCM walimdhadhalilisha sana Lowassa kiasi kwamba Leo tunapowaona wameongozana kwenda kwenye mazishi yake, tunajiuliza, KULIKONI???
yaliyopita si ndwele tugange ya sasa na yajayo 🐒

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Mc ni Mavunde nini? Huyo mzee APUMZIKE sasa atakuwa amechoka mpaka ubongo! Awaachie vijana! Tangu nikiwa kijana yeye ni MC tu mpaka leo nimezeeka!
Kweli. 1988 nilikuwa Dodoma Peter Mavunde alikuwa mc kipindi hicho alishirikiana na rafiki yake jina limenitoka. Huyo rafiki alifariki kitambo sana.
 
Tangu wanaccm walipomdhihaki Lowasa ni miaka mingi imepita lakini hakuwahi kutokea kiongoxi yeyote wa CCM kumuomba msamaha kwa waliyomtendea, leo haohao wako mstari wa mbele bila aibu kumsifu! Mungu wa mbinguni anawaona kwa unafiki wenu eti leo mmemuona Lowasa mtamu.
 
Back
Top Bottom