Mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Lowassa, Februari 17, 2024

Mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Lowassa, Februari 17, 2024

Kuna watu walikuwa wakisema Marehemu hakuwa Mmasai je hili lina ukweli kiasi gani? Kama ni kweli vipi hizi taratibu za mazishi za kimasai zinazoendelea zikiongozwa na wazee wa mila au ndiyo ule msemo unaosema pesa inaweza kuvunja milima?
 
KikulachoChako hiyo picha uliyoweka unainasibisha na Nini??

Mwenyewe humu nina mabandiko ya kutosha kushinikiza Lowassa afikishwe mahakamani. Unajua ni kwa nini??

Sisi tulijua hata iweje CCM hawawezi kumfikisha Lowassa mahakamani kwani wanajua ni sawa na kufungua Sanduku la Pandora.
 
Chuganian hawana unafiki
That Lema is my vision kabisa sicheki na nyani wakijani
Lema hapendi unafiki
20240217_130454.jpg
 
Tanesco akili visoda, tukio la kitaifa linaendelea wao wamakata umeme, TANESCO nani amewaroga nie jamani, inaumiza na kuudhi sana
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Zamani wa Monduli (CCM) Hayati Edward Lowassa anazikwa leo Nyumbani kwake, Monduli. Mazishi haya yamehudhuriwa na viongozi wakuu wa Nchi wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Waombolezaji wametoa Salamu za Mwisho kwenye Jeneza la Hayati Lowassa, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kisha famili ya Lowassa, viongozi wengine wa kitaifa pamoja na Viongozi waandamizi kutoka vyama vya upinzani, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe.

Mazishi haya yataendeshwa kwa Sehemu mbili, Kidini na Kiserikali. Kwa upande wa Dini, Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa ataongoza ibada hiyo, kisha Jeshi la Wananchi la Tanzania litashiriki sehemu ya pili ya Mazishi hayo.

Kwa mujibu wa taratibu za Kijeshi, Hayati Lowassa atapigiwa mizinga 17 kwa heshima yake.

Saa 6:25 Mchana, Maafisa wa JWTZ wenye cheo cha Kanali wanauingiza Mwili wa Hayati Lowassa Kaburini. Zoezi hili linafuatiwa na kuweka mchanga kaburini kama sehemu ya kuaga.

Saa 6:55 Mchana, maafisa wa JWTZ wameanza shughuli za kufunika kaburi. Mizinga 17 imepigwa.

JK na RA vipi wapo hapo
 
Mkuu uku tupo live n muda wakuweka mashadaa ,,

Hakikaa kaburi limependezaaa ...

Rip lowasaa
 
Kuna mambo mengi hapa yamewekwa wazi tofauti na Chato, camera zilikuwa remotely controlled kutoka kusikojulikana
Kama Una angalia ITV, Sawa Ila kama ni TBC kuna vitu hawaonyeshi,

Hata nyumba ya lowasa , haionekani, utasema msiba unafanyika porini
 
Back
Top Bottom