Huu ni ujinga sana na siku hizi naona unafanywa kama trend.
Kufanya mazoezi kwa lengo la kumfurahisha mwingine na sio kwa lengo la kuimarisha afya yako ni ujinga.
Kama wewe unafanya hivyo ili umridhishe, yeye anafanya nini ili akuridhishe?
Hii ndio mentality ya kijinga ambayo inawafanya watu waanze kutumia midawa ya ajabu ajabu hadi wengine kufikia maamuzi ya kufanya enlargment ilimradi tu kumridhisha kimapenzi mwanamke halafu mwisho wa siku side effects zinakuja kipindi ambacho hata mahusiano na huyo mwanamke hayapo tena .