Mazungumzo ni njia pekee ya kutatua mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
95e92d2cb59d71856876a71bc31dd189.jpg
China na Marekani hivi karibuni zilifanya duru mpya ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara huko Stockholm, nchini Sweden, ambapo pande hizo mbili zilibadilishana maoni kwa kina kuhusu masuala ya kiuchumi na kibiashara.

Pande hizo zilifikia makubaliano kwamba, Marekani itaendelea kusimamisha ongezeko la ushuru wa asilimia 24 dhidi ya bidhaa za China kwa siku 90, huku China ikisimamisha hatua za kulipiza kisasi katika muda huo. Mazungumzo hayo yamezidi kuimarisha imani katika kusuluhisha mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, na kuthibitisha kwamba, mazungumzo ni njia pekee ya kuondoa mgogoro huo.

Kama nchi ya pili na ya kwanza kwa ukubwa wa uchumi duniani, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani si kama tu unahusisha China na Marekani, bali pia unahusisha dunia nzima. Kwenye mazungumzo hayo, China iliweka wazi kwamba uhusiano endelevu na thabiti wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi zote mbili na kuwa nguzo ya utulivu wa uchumi duniani. Kwa upande wa Marekani, pia ilikubali kwamba uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili una umuhimu mkubwa, na kueleza nia yake ya kuendelea kutatua mgogoro kupitia mazungumzo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imedai mara kwa mara kwamba uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na nchi nyingine duniani siyo wa haki, na unapaswa kurekebishwa, ili kutimiza uwiano. Lakini uwiano hauwezi kupatikana kwa shinikizo la upande mmoja, unapaswa kuwa na msingi wa kunufaishana na kupatikana kwa njia ya mazungumzo. China inajitahidi kupata maendeleo ya hali ya juu, na imefungua mlango wake kwa dunia nzima. China na Marekani zina maslahi mapana ya pamoja na nafasi kubwa ya ushirikiano katika nyanja za uchumi na biashara, na maendeleo ya China na sera yake ya kufungua mlango vimetoa fursa zaidi za ushirikiano wa kunufaishana kwa Marekani.

Uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani hauwezi kubaki tuli bila ya mabadiliko, lakini mwelekeo wa mabadiliko upo mikononi mwa nchi hizo mbili. Je, uhusiano huo utaelekea kwenye kunufaishana zaidi, au kuingia katika hali ya kuvutana? Jibu ni dhahiri. Wakati nchi hizo mbili zinakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi na kibiashara, njia pekee ya utatuzi ni mazungumzo.
 
Marekani inaanzisha yenyewe migogoro halafu inataka mazungumzo WTF!
 
Hamna mgogoro zaidi ya ubabe mavi wa USA .
Na ubaya miaka hii Marekani haina ubabe kwa China ni mwendo wa mutual respect na negotiating table

Huwezi kuona Marekani imekaa mezani na mataifa mengine aliyoyapiga tariffs kwa heshima kama anavyofanya na China

Utakuta tu Trump anapost kwa dhihaka "deal done" kuwa wamekubali hata kama hawajafikia muafaka, plus maneno yake ya shombo

Kwa China ni mutual respect, cooperation na win-win situation.

Hutaki win win cooperation basi rudi zako Washington nirudi Beijing till next time
​
 
View attachment 3430383China na Marekani hivi karibuni zilifanya duru mpya ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara huko Stockholm, nchini Sweden, ambapo pande hizo mbili zilibadilishana maoni kwa kina kuhusu masuala ya kiuchumi na kibiashara.

Pande hizo zilifikia makubaliano kwamba, Marekani itaendelea kusimamisha ongezeko la ushuru wa asilimia 24 dhidi ya bidhaa za China kwa siku 90, huku China ikisimamisha hatua za kulipiza kisasi katika muda huo. Mazungumzo hayo yamezidi kuimarisha imani katika kusuluhisha mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, na kuthibitisha kwamba, mazungumzo ni njia pekee ya kuondoa mgogoro huo.

Kama nchi ya pili na ya kwanza kwa ukubwa wa uchumi duniani, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani si kama tu unahusisha China na Marekani, bali pia unahusisha dunia nzima. Kwenye mazungumzo hayo, China iliweka wazi kwamba uhusiano endelevu na thabiti wa kiuchumi na kibiashara kati yake na Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya nchi zote mbili na kuwa nguzo ya utulivu wa uchumi duniani. Kwa upande wa Marekani, pia ilikubali kwamba uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili una umuhimu mkubwa, na kueleza nia yake ya kuendelea kutatua mgogoro kupitia mazungumzo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imedai mara kwa mara kwamba uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na nchi nyingine duniani siyo wa haki, na unapaswa kurekebishwa, ili kutimiza uwiano. Lakini uwiano hauwezi kupatikana kwa shinikizo la upande mmoja, unapaswa kuwa na msingi wa kunufaishana na kupatikana kwa njia ya mazungumzo. China inajitahidi kupata maendeleo ya hali ya juu, na imefungua mlango wake kwa dunia nzima. China na Marekani zina maslahi mapana ya pamoja na nafasi kubwa ya ushirikiano katika nyanja za uchumi na biashara, na maendeleo ya China na sera yake ya kufungua mlango vimetoa fursa zaidi za ushirikiano wa kunufaishana kwa Marekani.

Uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani hauwezi kubaki tuli bila ya mabadiliko, lakini mwelekeo wa mabadiliko upo mikononi mwa nchi hizo mbili. Je, uhusiano huo utaelekea kwenye kunufaishana zaidi, au kuingia katika hali ya kuvutana? Jibu ni dhahiri. Wakati nchi hizo mbili zinakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi na kibiashara, njia pekee ya utatuzi ni mazungumzo.
aliyeanzisha vurugu za taarif kwa kujiona mkubwa kuliko wenzake anaenda kuomba tena mazungumzo
 
Back
Top Bottom