Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Ndugu H. Polepole ameanza kwa kuelezea kifo cha Marehemu Raisi John Pombe Magufuli kilichotokea 2021. Huku akisema Magufuli alianza kuugua baada ya kufanya uzinduzi wa kiwanda cha Rostam kule Morogoro kisha wiki mbili baadae umauti ukamkuta.
Pia amegusia maadui wakubwa wa Marehemu Raisi John Pombe Magufuli na namna ambavyo Raisi Mstaafu J.M.Kikwete alivyokuwa akimfanyia figusi wakati wa utawala wake.
Pia amelezea namna Angela Kiziga kupitia tenda ya ku-supply uniform za jeshi alivyopagaza pesa za serikali na ukaribu wake na Raisi Samia.
Pia amelezea Rostam Aziz anavyohujumu uchumi wa nchi kupitia kampuni yake ya Taifa Gesi na kuiteka serikali. Huku akisema, Cuba mtungi wa gesi wa kilo 20/= unauzwa 2000/= TZS na Tanzania tunauziwa 55,000/=TZS.
Pia amesema CUBA huduma za kijamii kama elimu, umeme na huduma za kiafya ni bure.
Pia amegusia namna ambavyo mafisadi wanatakatisha fedha za umma na kununua magari ya gharama za juu.
Pia amegusia ufanisi wa serikali, uwajibikaji wa watumishi na viongozi serikalini na kusema kwa sasa ni sifuri.
Huku akishangaa kampeni za mgombea wa CCM -- kutokupinga ufisadi wa mali za umma, rushwa na utakatishaji fedha.
"Ukombozi huanza akilini." ----------- Next Press --> "Deni La Taifa"
Link Below
View: https://www.youtube.com/watch?v=Wf-eovLnI7c
Aisee