mangikule
JF-Expert Member
- Jun 11, 2012
- 6,369
- 5,866
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimpokea na kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya William Somoei Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Oktoba, 2022
Rais Samia Suluhu Hassan
Mambo yaliyojadiliwa na Rais Samia Suluhu na William Rutto ni pamoja na;
Kukuza na kuimairisha uhusiano kati ya Tanzania na kenya.
Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vya biashara.
Mkutano wa tume ya pamoja ya mashiriano ufanyike na kufanyiwa hatua kwa haraka.
Kuangalia zoezi la kuimarisha mpaka wa kimataifa kati ya nchi mbili hizi.
Mradi wa bomba la gesi kusafirisha gesi asilia Dar kwenda mombasa.
Kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyovuka mipaka, kama madawa ya kulevya, uharamia, ujangili na biashara haramu ya binadamu.
Kushikiana katika maswala ya kikanda na kimataifa kwenye Umoja wa Afrika na Afrika Mashariki.
Rais William Ruto
Lengo langu ni kuhakikisha misingi iliyoachwa na Uhuru Kenyata kuhakikisha kuwa naendelea kuijenga na wewe na kupeleka nchi zetu kwenye hatua nyingine.
Kuongeza mahusiano ya kibiashara mara mbili zaidi kati ya Kenya na Tanzania.
Nataka kuthibisha Mawaziri wa Kenya wakishathibitishwa kuanza kufanya kazi, kazi yao ya kwanza itakuwa ni kufanya kazi na wenzao wa Tanzania, kuondoa vikwazo vilivyobaki, JCC ifanyike Disemba ili biashara ziendelee vizuri na kukua zaidi kwa manufaa ya Kenya na Tanzania.
Hilo ni jizi jingine! Samia hamuwezi! Huyu si ndiye aliyesema mahindi ya Tanzania yana Aflatoxin! ili auze mzigo aliolimia DRC! Beware of a notorius LAND GRABEr