Mateo Kovasic
JF-Expert Member
- Aug 9, 2022
- 420
- 334
Mazuri hujisema yenyewe...ukiona mtu anatetewa sana ujue ni dhaifu sana.
Lusungo
Kwani Lisu hatetewi??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mazuri hujisema yenyewe...ukiona mtu anatetewa sana ujue ni dhaifu sana.
Lusungo
Kazi zake zilimtangaza.Kwani Lisu hatetewi??
Porojo
porojo zile zile, tarehe na viongozi tofauti. tulishazizoea hata tukizisikia hatushtukiUVCCM-TAIFA
OCTOBA 11, 2022
IKULU DAR ES SALAAM
MHE. RAIS AMESISITIZA MAMBO YAFUATAYO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN amesema kuwa amekubaliana mambo Mengi na Rais wa Kenya Mhe. WILLIAM RUTO ila amesisitiza kwenye mambo yafuatayo;
◇ Kukuza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zetu mbili.
◇Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara
◇Mkutano wa nne wa tume ya pamoja ya Ushirikiano ambao ulikuwa ufanyike agost.
◇ Kuangalia zoezi la kuimarisha mpaka wa kimataifa kati ya Kenya na Tanzania.
◇Mradi wa Bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa.
◇ Kushirikiana Kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyovuka mipaka.
◇Kushirikiana katika maswala ya kikanda ja kimataifa, tumekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri.
#AlipoMamaVijanaTupo
#ShirikiUchaguziKwaUadilifu
#VijanaGreenMarathon
#KaziIendeleeView attachment 2383293
Duh!Strategic point! Ndiko litaleta faida na return kwa haraka!, ulitaka lipelekwe huko usemapo bila tafakari ya kina. (busy city chattle and it's traffic light)
Kuna tatizo la msingi, na hadi hapo tutakapoweza kuliondoa tatizo hilo, maendeleo tutaendelea kuyasikia tu kwa wengine.Tuliowapa madaraka Tanzania ukiangalia kiundani ni kama hawana uchungu na hii nchi,inakuaje tuharakishe gesi yetu iende kenya ikiwa hapa kwetu bado haijakidhi matakwa ya wananchi,leo hii Tanzanite inapatikana Tanzania lakini kenya ndio inaongoza kuiuza nje ya afrika,avocado inalimwa Tanzania lakini kenya ndio anauza nje now tunawapelekea gesi,jamaa sijui wanafikiriaga nini!
Imagine kenya ndio mshindani wetu mkubwa ukanda huu kiviwanda,kibiashara n.k,badala ya hii gesi kuboresha itumike kwenye viwanda vya ndani ili tuipige gape kenya sie ndio tunaharakisha kumpa power zaidi mshindani wetu,hivi hii gesi ingekuwepo kenya wangekubali kuleta pipe kwetu?,viongozi wetu wanatia hasira maana hawana uchungu na hii na sisi wananchi wake,leo hii kitakwimu eti sisi ndio tunaongoza kuimport bidhaa toka kenya maana wao hata toothpick awaleti kwetu kijirani ila kiuhalisia wao ndio wanaimport vitu vingi mno kutoka kwetu lakini serikali aiweki hivyo vitu kwenye takwimu,vitu vyetu vinaenda kenya kiholela,kishkaji kiasi kwamba kenya anatumia hivyo hivyo kuuza nje anachofanya anaweka lable tu made in kenya vingine anakuja kuuza tena huku TZ na viongozi wetu wala awashtuki sababu tu familia zao maisha yanaenda sie tutajijua wenyewe,viongozi wamekosa uzalendoKuna tatizo la msingi, na hadi hapo tutakapoweza kuliondoa tatizo hilo, maendeleo tutaendelea kuyasikia tu kwa wengine.
Tanzania inahujumiwa sana, lakini viongozi hawaoni uchungu kabisa na hujuma hizo. Mbaya zaidi, na wao wanakuwa washiriki kwenye hujuma hizo hizo.
Jamaa wamefikia hatua ya kuja kulima vitunguu Manyara, wakivuna wanavusha mpakani na kwenda kuvifungasha vizuri na kuvipeleka ulaya kuuza kama mali iliyozalishwa Kenya. Sisi na viongozi wetu tupo tu tunakenua meno!wanaimport vitu vingi mno kutoka kwetu lakini serikali aiweki hivyo vitu kwenye takwimu,vitu vyetu vinaenda kenya kiholela,kishkaji kiasi kwamba kenya anatumia hivyo hivyo kuuza nje anachofanya anaweka lable tu made in kenya vingine anakuja kuuza tena huku TZ na viongozi wetu wala awashtuki sababu tu familia zao maisha yanaenda sie tutajijua wenyewe,viongozi wamekosa uzalendo
Ni ujinga tu wa viongozi wetu,kenya ilibidi tuwauzie unga na sio mahindi,na ukitaka kujua jamaa wamewazidi maarifa viongozi wetu kamwe hawawezi kununua unga wa kutoka kwetu,viongozi wangejiuliza hivi wanavyofanya wakenya kwetu serikali ya kenya inaweza kuruhusu watanzania tukafanya hivyo kwao!Jamaa wamefikia hatua ya kuja kulima vitunguu Manyara, wakivuna wanavusha mpakani na kwenda kuvifungasha vizuri na kuvipeleka ulaya kuuza kama mali iliyozalishwa Kenya. Sisi na viongozi wetu tupo tu tunakenua meno!
Wale wenye mashine zao za kusaga unga, wanakuja na malori yao hapa, wanaingia hadi vijijini kusaka mahindi kwa wakulima, hata bila ya kuwa na liseni ya kufanya biashara hapa. wanajaza malori wanapeleka kwao, viongozi wetu wanapiga tu kelele, mkulima asipangiwe wapi anauza mazao yake, kana kwamba hawajui kwamba mkulima hajaenda popote toka kijijini kwake; hata kumfahamisha tu mkulima huyo anavyoweza kufaidika zaidi na bidhaa yake kama yeye, au kundi wangeweza kuungana na kupeleka mzigo wao wenyewe huko sokoni. Hili ni gumu sana kwa hawa viongozi kulielewa!
Kuna kitu mahali nchi yetu imepungukiwa sana