Mazungumzo ya Rais Samia na Rais Ruto, Ikulu Dar es Salaam Oktoba 10, 2022

Rais Samia Suluhu amefanikiwa kuimarisha mahusiano ambayo yalikua yamepotea hongera sana mama

Kwa rais wa Kenya kuja Tanzania ndio mahusiano kuimarika?! Kipindi cha Magufuli Uhuru si alikuwa anakwenda hadi Chato na akapewa na ndege aina ya taus kabisa? Inawezekana kuna mahusiano Samia kayaleta, lakini hilo la ujio wa rais wa Kenya sio kipimo cha hilo.
 
Nasikia amewasili na gunia la Mirungi.
EeeeenHeeeee!
Sitashangaa kamwe tukihimizwa kuanza kutafuna mirungi ili biashara kati yetu ishamiri zaidi.
Ninakuhakikishia, muda si muda utasikia habari ya bidhaa hiyo ikipigiwa kelele sana tuka huko inakolimwa ili iingizwe hapa.
Hiyo bidhaa ni zao muhimu kwenye jimbo (Meru County) lililomuunga mkono sana Ruto; kwa hiyo hao wakulima wa zao hilo ni watu wake wa karibu sana kwake na atawapigania kwa kila njia.
Tayari Somalia shawapatia soko muhimu huko.
 
Hilo bomba mnufaika ni Taifa Gas ambaye ni Rostam Aziz.

Na Rostam wote tunamfahamu ni nani nchi hii.

Utawala huu haufurukuti kwa watu kama hao.
 
Pamoja na kupiga kiberiti vifaranga vyao lakini Wakenya hawana noma yaani !!
 
Wakenya wamekuja kuturingishia na demokrasia yao. Wanajidai sana.
 
Nyerere au Magufuli Ikulu Ruto asingepita getini kavaa hivyo.

Wanajua huyu Mama is a door mat, they can walk all over her
 
Pamoja na kupiga kiberiti vifaranga vyao lakini Wakenya hawana noma yaani !!
EeeenHeeeee!

"---hawana noma"?
Unapokula na kipofu utasogeza mkono wako karibu na wa kwake ajue unamega tonge zito kuliko yeye?
 
Strategic point! Ndiko litaleta faida na return kwa haraka!, ulitaka lipelekwe huko usemapo bila tafakari ya kina. (busy city chattle and it's traffic light)
 
Uamuzi umetoka yote inaenda Zanzibar na Pemba!
 
Tuliowapa madaraka Tanzania ukiangalia kiundani ni kama hawana uchungu na hii nchi,inakuaje tuharakishe gesi yetu iende kenya ikiwa hapa kwetu bado haijakidhi matakwa ya wananchi,leo hii Tanzanite inapatikana Tanzania lakini kenya ndio inaongoza kuiuza nje ya afrika,avocado inalimwa Tanzania lakini kenya ndio anauza nje now tunawapelekea gesi,jamaa sijui wanafikiriaga nini!
 
Huwezi ukaziona faida zake kwa kuwa ulishaipa akili yako kazi ya kupinga na kuona kila kitu Ni kibaya
Kuna faida gani mkuu,hivi bibi yako huko mwandiga vijijini anapata gesi ya kueleweka kwenye matumizi ya hapo kijijini kwake kiuhakika kuanzia kwenye umeme,kupikia n.k hadi hiyo gesi ipelekwe kenya,muda mwingine tuweke mapenzi yetu ya siasa pembeni tuangalie hali halisi ya Mtanzania mmoja mmoja
 

hamna shukurani halafu kila kukicha mnawatukana wahindi na bado wanasaidia
 
Hivi Rais wa nchi anapokwenda kwenye nchi nyingine ki protocal ana lala Ikulu au kwenye hotel zetu hizi hizi za Kempiski?
 
Acha upotoshaji kinachofanyika sisi tuawauzia gesi na Tanzania tunaendelea kunifaika na gesi yetu kwaiyo hata kupiti huu mradi ukiwa unatekelezwa Tanzania na Kenya wote tutapata fursa mbali mbali ikiwemo ya ajira
Wewe tulia...huwajui wakenya!
Ukikua utaelewa somo.
 
Mwenye Enzi Mungu ibariki nchi yangu Tanzania [emoji1241] na Watu wake, tuepushe na shari zote hapa duniani walahi [emoji2972]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…