Mbali na kuwa Rais, Magufuli alikuwa nani katika nchi hii? Tumechoka sasa

Mbali na kuwa Rais, Magufuli alikuwa nani katika nchi hii? Tumechoka sasa

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
download (3).jpeg

Kipindi cha nyuma nilikua nampenda na namkubali JPM kwa utendaji wake kazi lakini kwa sasa naona kama vile nikisikia hata jina lake napata kichefuchefu sasa maana imekua too much

katika hali isiyo ya kawaida mimi nashangaa na ninasikitika sana, nimejiuliza sana Hayati JPM alikua na kipawa cha namna gani hiki? sasaivi baadhi mambo hayaendi kwasababu yake, hata marais wengine wastaafu sasahivi hawaheshimiki kabisa kisa JPM

Rais wa sasa anapata wakati mgumu sana kueleweka kwa watanzania, kila anachokifanya watu wanabeza wanataka afanye kama alivyokua anafanya JPM

Nashangaa sana Rais akitengua uteuzi wowote aliokuwa ameteua JPM watu wanaongea sana, wanafadhaika sana hawataki yani Rais Samia atoe mtu yyte aliyeachwa na JPM

Jana baada ya utenguzi wa mawaziri wa JPM watu wanalalamika sana, koment nyingi za wananchi wa kawaida mitandaoni wanamlilia JPM, yaani watu wanaona yoyote yule aliyeachwa na JPM hastahili kutenguliwa

Imefika hatua hadi watu wanamchukia Samia kisa tu ameenda tofauti na baadhi ya mambo ya JPM

Huu sio ustaarabu kwanza mimi ningekua ni Rais Samia, natengua baraza lote navunja hata na bunge tunaanza upya uchaguzi na mambo yangu ninayoyajua mimi , maana nimeona kuwa mstaarabu kwa watu ambao hawajastaarabika ni kama kupaka rangi upepo,

nakushauri Rais bora ufanye mambo yako kivyako kwa mujibu wa katiba asiyekubaliana na wewe afanye mapinduzi akupindue na dunia nzima ijue

JPM tulimpenda kama Rais wetu lakini sasa tumechoka na huu upuuzi kila kitu JPM kila Kitu JPM Laiti kama mimi ndio ningekua ni Rais wa sasa kwa moyo wangu jinsi ulivyo ningevunja baraza la mawaziri nikaanza upya kabisa na mambo yangu mapya

Sasa hivi Tuko na Rais mwingine hatuwezi kuongozwa na aliyeishazikwa, Tuwe wastaarabu watu wapuuzi dizaini ya polepole na askofu kibwetere hawafai hata kukanyaga kwenye ardhi ya bunge la nchii hii ndio wanapandikiza chuki dhidi ya serikali ya sasa

IMG_20210913_082845.jpg

IMG_20210913_082749.jpg
 
Ulikuwa unampenda na kumkubali utendaji kazi wake akiwa hai lakini unaskia kichefuchefu baada ya kufa? Hii kali ya mwaka!😂
Ni kosa gani amelifanya akiwa ameshafariki? Au wewe ni mnufaika wa hizi teuzi mpya labda?!
 
Ulikuwa unampenda na kumkubali utendaji kazi wake akiwa hai lakini unaskia kichefuchefu baada ya kufa? Hii kali ya mwaka!😂
Ni kosa gani amelifanya akiwa ameshafariki? Au wewe ni mnufaika wa hizi teuzi mpya labda?
Achana nawo hao, ni kama baba, katusomesha, katupa malazi, katatuwa shida zetu zote mpaka tukasimama, halafu akifa twaanza mponda na kumuona fala tu, lofa, fulani, ila ukweli wajulikana, hautafunikwa kamwe, hata iwe nini.
 
Hahahah, nimependa reaction ya watanzania. Kweli zama hizi ni zama za utandawazi.

Watanzania ni werevu Sana.
Mama kazi anayo.
Kwa Kalemani, ameonyesha biff.

Sasa matokeo ya biff, hua nimatumizi ya nguvu kuzima Resistance. Ajiandae kuitwa Dictator Muda si mrefu.

Make naona anatoa watu wenye akili Sana na wenye uelewa mpana. Kakurwa, Pole pole, Kalemani, .,.eh!!? Kabudi kabaki eh!?
 
Mleta mada naona unajaribu kupima imani za watu kuhusu viongozi wetu. Lakini ukweli ni kwamba hauwezi kuzungumzia mazuri ya Tanzania bila kumzungumzia JPM hivyo hivyo kwa viongozi wengine waliopita.

JPM anazungumziwa sana kwa sababu ndio alieacha uongozi kwa raisi Samia. Hata Magufuli alipokuwa madarakan watu walimuongelea sana JK mpaka kufikia hatua ya kulinganisha uongozi wake na wa JK kana kwamba hakuna viongozi wengine waliowahi kutawala nchi hii kama vile hayati Mkapa na Mzee Mwinyi.
 
JPM ndio aliharibu kila kitu, Samia anajaribu kurekebisha nae yamemshinda. Kwani hao waliopo si ndio aliwaacha huyo JPM. Hao ma V8, na huyo anaefufua watu, JPM alitiharibia hii nchi.

Samia angepaswa kuvunja balaza lote la mawaziri, kuanza na PM na hao wengine. Aunde balaza lake, hao mikia wa J awapige chini.
 
Ukifanya mema utakumbwa tu,hawwmlilii bila sababu wanasababu zao
 
watu wanalalama kwa sababu magufuli aliitoa nchi mikononi mwa wanyang'anyi bila kuogopa lawama ila kwa sub zinazofanyika direct zinaashiria nchi imerudi kwa wanyang'anyi na hiki ndo kinawaumiza watanzania wengi.
Kwamba zile zama za kubeba pesa kwenye sandarusi zimerudi? ngoja tuone hiki kichaka kinachoitwa tozo kitakuja na matokeo gani....
 
Back
Top Bottom