M'bananga chake hana kondo (If you spoil what is your own you have no quarrel)


..Sudan, Ethiopia, Somalia, wote walikuwa na matatizo yao ya kikabila yaliyosababisha vita na hatimaye kujitenga.

..Matatizo ya nchi hizo hayakusababishwa na mfumo wa majimbo bali na dhuluma za watawala wao.
 
..Sudan, Ethiopia, Somalia, wote walikuwa na matatizo yao ya kikabila yaliyosababisha vita na hatimaye kujitenga.

..Matatizo ya nchi hizo hayakusababishwa na mfumo wa majimbo bali na dhuluma za watawala wao.
Ukabila na Ukanda ni kitu kile kile, yaani hakuna kabila lisilimiliki ardhi (himaya) ama kuona ardhi hii ni HAKI yetu. Sasa mkiweza kuona Tofauti zenu iwe kwa Kabila, Dini au Ukanda ndio hapo uhasama huanza. Maadam, unaamini Wazanzibar sii wenzetu ni kukubali Tofauti baina yenu na wao na wao vile vile wanaona Utofauti huo hata kama Wazanzibar ndio waloanza kujitofautisha na Ukweli ni kwamba zaidi ya 2/3 ya hawa Wazanzibar asili yao ni Wahamiaji iwe walitoka Bara, Visiwa vya Ngazija, Iran, Yemen na Oman. Na kibaya zaidi idadi yao kubwa ipo BARA na hawajatengwa wala kuitwa Wazanzibara.

Kwa hiyo hizi Siasa za HIZBU ni lazima zipigwe vita sii kwa Uzanzibar bali kiini cha matatizo yetu ni ujio wa Siasa za Hizbu na kwa bahati mbaya sana Baraza la Mapinduzi hawana nguvu tena kuliko Baraza la Wawakilishi.
 
Reactions: Lax
..kosa kubwa alilofanya Mwalimu Nyerere ni kuifuta Tanganyika, huku akiiacha Zanzibar.

..sasa tumefika mahali ambapo huwezi tena kuwashawishi Wazanzibari wafute utaifa wao, kama walivyofanya Watanganyika, ili wawe WATANZANIA.

..Uendeshaji wa nchi yetu ni mgumu sana kuuelezea ukaeleweka kwa mwananchi wa kawaida. Muungano wetu hauna mantiki.

..Kwa Watanganyika muungano ni sawa ni sawa na mwanaume aliyeoa lakini unyumba hapewi. Na zaidi analazimishwa kutoa hela ya matumizi.
 

..Nchi yoyote ile lazima iendeshwe kwa USAWA.

..ukiweka mbele daraja la Uzanzibari, badala ya UTANZANIA unakuwa umedhoofisha muungano.

..Sote tungetambuana kama WATANZANIA muungano wetu usingekuwa na maneno maneno.

..Tatizo kuna wenzetu hawajakubali kuwa WATANZANIA. Hawajakubali kuungana. Je, wasubiriwe mpaka lini?
 
Hapana mkuu hata sisi Tunaweza semwa hivyo hivyo maana vijana wengi Maskini na hata wenye Elimu za juu hawana ajira wakitafuta kazi za maofisini kuvaa tai. Hawawezi kazi za shuruba.

Umaskini umetamalaki pande zote, sema sisi tuna nafasi kubwa ya kutoka katika Unaskini kupitia Kilimo na Ufugaji lakini sio kwenye Madini ama Utalii wanaofaidika ni Wageni.

Umaskini hutokana na mipango mibata ya maendeleo nadhani Magu alituachia mwanzo mzuri sana akijaribu kufuta Umaskini na ndiye rais pekee alopendwa Bara na visiwani.

Usichukulie maneno ya wale Wabunge wao wanao tubeza Bara, hizo siasa tu. Na mimi naamini Hussein Mwinyi akiendelea kuwa rais wa Zanzibar watapiga hatua kubwa sana katika maendeleo yao.

Mimi naamini Tanzania hii (Bara na Visiwani tuna nafasi kubwa ya kuondokana na Umaskini tukiweka nguvu kubwa kwenye kazi zetu za Asili kama Kilimo, Uvuvi, Ufugaji ambazo leo zina soko kubwa ndani na nje. Ubaya mmoja tu, hizi mbegu za MGOs zinawaharibu vijana wengi wa Kiume..😂😂 ( Mpango wa Bill Gates kupunguza uzazi)
 
Ndio nasema ASP na Baraza la Mapinduzi liko wapi? Wamesahau historia yao walivyokuwa wakitengwa enzi zile za Muingereza?

Hata kama leo wamefikia Muafaka kukubaliana wote ni Wamoja inakuwaje Baadhi yao wanatumia nafasi hii kurudisha Siasa za HIZBU?

Tatizo la Muungano ni kundi hili dogo sana lakini lina nguvu kubwa ya Siasa za Zanzibar na kibaya zaidi wanatumia viongozi wa Kiimani na Kisiasa. JK aliweza sana kuwathibiti lakini naona wamerudi kwa nguvu kubwa zaidi kupitia Uzanzibar wa Mama Samia.
 

..Mapinduzi ya Zanzibar chanzo chake kilikuwa ni hila na ugomvi ktk uchaguzi.

..Wanachofanya Ccm tangu mwaka 1995 ni kilekile walichokuwa wakifanyiwa ASP kabla ya Mapinduzi.

..Na kwa bahati mbaya Ccm wameuwa Wazanzibari wengi ktk uchaguzi kuliko waliouwawa na utawala wa Jamshid kabla ya 1964.

..Tatizo la muungano, au Utanzania, ni identity ya Zanzibar.

..Ndugu zetu wameachwa wakajenga imani na mapenzi kwa utambulisho wao wa Uzanzibari kuliko Utanzania.

..Mwalimu Nyerere aliposema hataki kuimeza Zanzibar, halafu akaifuta Tanganyika, matokeo yake ndio haya.

..Wazanzibar hawataki kuwa Watanzania. Hatuwezi kuwalazimisha kwani tutasababisha matatizo makubwa.
 
Hapana mkuu historia ya ASP umeisikia vibaya maana wao ndio walikuwa washinda, Muingereza akatengeneza hila za kutowapa Ushindi kwa sababu ZNP waliahidi kuwapa Pwani ya Kenya. Sale out!

Hata chama cha ZPPP kina Shamte walikuwa ASP wakatoka na ndio walotumiwa kuhatibu kila Uchaguzi. Na Uchaguzi wa 1963 ASP alishinda viti vingi, lakini walikosa Majority. Na kawaida ya Chaguzi zote mshindi akikosa Majority yeye ndiye atatafuta mshirika ili eapate Majority.

Xanziba hakiukufanyika hivyo badala yakr ZNP wakawashawishi ZPPP kuungana wao na Shamte (msindi wa 3) akapewa Uwaziri Mkuu. Haijawahi tokea popote dunianu mshindi wa 3 kuwa bdiye kiongozi wa nchi.

Labda nikurudishe nyuma zaidi, hata walipojitoa kina Shamte na kuunda ZPPP walishauriwa na vuongozi wa ASP waungane wote dhidi ya Hizbu, kina Shante walikataa. Kwa hiyo Mapinduzi yalikuwa lazima na yalipangwa na kitengo cha Pan-African Freedom Movement of East and Central Africa (PAFMECA) naambiwa mkutani ulifanyika Mwanza - Financed by Nkurumah.

Mapinduzi ya Zanzibar ndio Ukombozi wa kwanza wa Pafmeca kufanikiwa na zipo taarifa Okello alikuwa trained na stationed Pemba kusubiri wakati muafaka ikiwa Muingereza ataendelea kutumia mbinu zake.

Na kweli baada ya Uchaguzi ZNP kutangazwa mshindi walipewa eneo lote la pwani kuwa sehemu ya Kenya. Historia hii hutaisikia popote kwa sababu hatupendi kusikia Ukweli ndani ya historia(Yalopita) ikiwa yamebeba machungu..
 

..Je, walichofanya ASP kutumia nguvu kubadili serikali sio UHAINI?

..Kwanini ASP hawakufuata taratibu za KIBUNGE kubadili sheria za uchaguzi?

..Kwanini CCM [ ASP + TANU] wamevuruga chaguzi nyingi, na kuuwa Wazanzibari wengi, kuliko utawala walioupindua 1964?
 
Sheria ipi ikiwa hoha ilikuwa kuundia Utawala wa Sultan? Neno Uhaini inategemea na mtawala nani hata kina Mkwawa, Abushiri, Mandela waliitwa Wahaini South

Tatizo la Sultan alikuwa na mamlaka hata kuuza NCHI maadam ahakikishiwe Usalama wake. Hata hii pwani yetu toka Kusini hadi Tanga, Mjarumani alipomtiishia tu akakubali kuachia! He didn't care of indigenous, na hii ndio sababu kubwa ya Mapinduzi kama ilivyokuwa Rhodesia kwa Smith.
 

..Zanzibar ilikuwa nchi huru.

..Hata Umoja wa mataifa uliwatambua na kuwapa uanachama.

..Na walikuwa na Katiba ambayo ilitokana na muafaka wa vyama vyote ikiwamo ASP.

..Na ASP walishiriki uchaguzi hivyo hawawezi kusema nchi haikuwa huru.

..ASP walikubali kuwa Sultani ndiye mkuu wa nchi kama alivyokuwa Mfalme / Malkia wa Uingereza na ndio maana walishiriki uchaguzi.

..Je, kinachoitwa Mapinduzi sio UHAINI?
 
Define nchi Huru? Maana zipo nchi nyingi zilitambuliwa kama nchi Huru wakati bado zipo chini ya Utawala wa Wakoloni. Na nyingine zipp mpaka leo hii wametawaliwa lakini wanajiita Nchi Huru.

Kwenda UN haina maana yeyote ikiwa Palestina haikuwahi kutambuliwa kama Nchi huru badala yake ilitambuliwa Israel baada ya wazungu kuhamia pale na kuita nchi yao (Zionist). Ama labda wewe nambie South Africa ilikuwa Nchi Huru lini?
Nchi Huru ni ile Wananchi wanajitawala wenyewe na sii kutawaliwa.
 
Daah
 
Aione Pascal Mayalla
 
Pascal Mayalla
 
..wazee wa Zanzibar wanapewa pensheni na serikali, kwanini wazee wa Tanganyika hawapewi hata mia? Muungano unawabagua Watanganyika.
Mkandara anasema hivi, kwanini watu wahoji mchango wa Zanzibar ikiwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Ndio maana tunamuuliza, ikiwa Wazee wa Zanzibar ni Watanzania kama Wazee wa Tanganyika kwanini Watanganyika wasipewe pensheni. Ngoja Mkandara aje na majibu kwanza!
 
Waasisi sio Mungu kwamba hata baada ya miaka zaidi ya 60 walijua nini kitatokea. Kwahiyo tusiite mabadiliko ni usaliti. Dunia wakati wote iko kwenye mabadiliko haiwezi kusimama pale ilipo kuogopa eti mawazo ya Nyerere na Karume. Muungano ni wa nchi mbili wala sio wa mikoa 26 hivyo usifananishe mtu anayetoka Unguja kwenda Kasulu na anayetoka Tanga kwenda kasulu. Mmoja kavuka sehemu moja ya serikali na mwingine katoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…