Mbarali: Ng'ombe zaidi ya 400 ambao ni mali ya Wananchi kupigwa mnada leo

Ukame una wachapaga huko monduli longido na maeneo mengine simanjiro nk

Mifugo ina pukutika kama kuku wa mdondo
Sahihi kabisa. Lazima tuyalinde mazingira kwa gharama yoyote ile, huo ndio uhai wetu na watoto wetu. Monduli na Lungido hakufai kabisa, ni kukame balaa, nenda huko Shinyanga ni kukame hatari. Mifugo lazima ifugwe kwa kuzingatia usalama wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji. Hiyo mikoa ya kilimo tusiiharibu kwa ufugaji uliopitiliza.
 
Ufugaji wa kuhama hama hauna nafasi tena kwenye Karne hii ya 21. Kama mtu hawezi kufuga kwa kutulia auze tu ng'ombe wake wote. Tukiwachekea wafugaji siku si nyingi nchi hii itageuka jangwa
Mabadiliko ya hali ya hewa yanasababishwa na mengi, wala sio wafugaji pekee, hata hao matajiri wanasiasa wanaochepusha maji ya mito nao wanasababisha mito kukauka, hao wafugaji wasitupiwe kila lawama kwamba ndio chanzo.
 
Ukame upo kote, hata huku Dsm ambapo hakuna wafugaji nako kuna ukame, jua kali kila upande, hao wafugaji wameonewa, wao pekee sio chanzo kikuu cha huu ukame unaosababisha ukosefu wa mvua na kuleta migao ya maji.
 
Ukame upo kote, hata huku Dsm ambapo hakuna wafugaji nako kuna ukame, jua kali kila upande, hao wafugaji wameonewa, wao pekee sio chanzo kikuu cha huu ukame unaosababisha ukosefu wa mvua na kuleta migao ya maji.
Hujatembea hii nchi, tembea uone mkuu.
 
Hii story imejaa politics nyingi,mala mifugo ya wakulima inapigwa mnada,mala kampuni inayoendesha mnada ni ya Mbunge wa zamani wa ccm aliyeuziwa mashamba ya wakulima!!
Sasa hapa Kuna hoja kama nne,
Mosi,Hawa ngombe wa wananchi,mamlaka iimewafata kwenye makazi yao ikawchukua kwa nguvu,au wafugaji walivunja sheria kwa kuingiza mifugo kwenye hifadhi,serikali ikakamata hiyo mifugo.!
Pili Huyu Mbunge wa zamani,kosa lake lipo wapi kuuziwa mashamba na kampuni yake kupewa kibali,Tena na mahakama ya kusimamia mnada,kwani utaratibu haukufwatwa?
Tatu,kwanini wafugaji hawana eneo la kunyweshea mifugo?walitengewa eneo au la!!
Nne,Hayo mashamba wanayodai,wamepolwa,ni kiasi gani walikuwa wanazalisha,wanalipa Kodi kiasi gani,na huyo Mbunge aliyeuziwa ana plan ya kuzalisha kiasi gani?na kulipa Kodi kiasi gani?
 
Bora umeuliza maswali objective sana
 
Hivi unashahidi kuwa Ng'ombe waliokamatwa ni mara yao ya Kwanza kukamatwa au unataka kulaumu maamuzi sahihi ya serikali.Mm naunga mkono hoja acha Ng'ombe wapigwe mnada tuuu
 
Hivi unashahidi kuwa Ng'ombe waliokamatwa ni mara yao ya Kwanza kukamatwa au unataka kulaumu maamuzi sahihi ya serikali.Mm naunga mkono hoja acha Ng'ombe wapigwe mnada tuuu
Wangesema kwenye taarifa, wewe kama una ushahidi hao n'gombe kukamatwa hii sio mara yao ya kwanza weka hapa, maamuzi sahihi ya serikali maana yake nini.
 
Endeleeni kuishi kwa kutegemea Mungu atalipa, dunia ya hivyo imebaki Tanzania na ndiyo sababu viongozi wamejijengea viburi na kutuambia tuhamie Burundi tunawaghasi.
 
Wacha wapige mnada tu
Nimeshuhudia kwa macho jinsi mifugo inavyoharibu ardhi

Unakuta sehemu kuna umande mwaka mzima ila mifugo ikipita mwezi tu Ukame tayari

Wauze na hela hizo zipandiwe miti na kuchunga vyanzo vya maji

Huwa napinga mengi ila kuhusu haya nasapoti kwa kila hatua
 
Umeuliza maswali ambayo majibu yake kila Mtu anayo , ama labda wewe ni mgeni Tanzania au umeamua tu kutusumbua
 
We jamaa una dhambi sana !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…