Mbarali: Ng'ombe zaidi ya 400 ambao ni mali ya Wananchi kupigwa mnada leo

Mbarali: Ng'ombe zaidi ya 400 ambao ni mali ya Wananchi kupigwa mnada leo

Watu weusi tuna shida kubwa sana siujui wapi tulikosea Mmungu atusamehe una mkuta mtu ana Ng'ombe na Mbuzi zaidi ya elf 3000 lkn maisha anayo ishi ni kama ndege anahama hama kila mahali kisa tu anatafuta Malisho na Maji huu ni uwendawazimu mkubwa kabisa sababu ukiangalia mifugo aliye kuwa nayo uki convert kwa pesa una mkuta wealth yako laabda BILLION Moja ya Tz au zaida unajiuliza maswali mengi unashindwa kupata jibu.
 
Lazima tulinde mazingira. Hakuna kuharibu mazingira kwa kigezo cha ufugaji
Kupiga mnada Ng'ombe za watu ndio kulinda mazingira?? hii ni dhulma, serikali gani kila ikipata nafasi ya kudhulumu raia inaitumia, mlifanya hivi kwenye samaki, DPP na mkimaliza hili mtaajiri wapiga roba wawasachi raia na kuwapora ili muendelee kupata pesa chafu.
 
Kupiga mnada Ng'ombe za watu ndio kulinda mazingira?? hii ni dhulma, serikali gani kila ikipata nafasi ya kudhulumu raia inaitumia, mlifanya hivi kwenye samaki, DPP na mkimaliza hili mtaajiri wapiga roba wawasachi raia na kuwapora ili muendelee kupata pesa chafu.
Ngoja tuone mwisho wao
 
Kuna eneo nilikua nakutaga nyasi za kutosha waliletwa ng'ombe 10 tu wiki moja nyasi zote kwisha kazi zimetafunwa zote pamekua peupe km uwanja wa mpira watoto wakafunga magoli wakaanza kucheza cha ndimu
Nyasi kipindi Cha kiangazi hukauka hata Kama ng'ombe wasingezila bado isingesaidia
 
Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kwamba ng'ombe hao wa wananchi wa Mbarali ambao idadi kamili ni 433, wanaodaiwa kukamatwa na Askari wa Wanyamapori kwenye hifadhi wanapigwa mnada leo 14/11/2022

Bali kampuni iliyopewa tenda ya kupiga mnada ng'ombe hao wa Wananchi inaitwa MBARALI HIGHLAND AUCTION MART LTD, Inayomilikiwa na Mbunge wa zamani wa CCM aliyetajwa kwa jina moja la Haroon , ambaye pia ndiye aliyeuziwa Mashamba ya Wananchi hao kwenye utawala wa awamu ya 4, yaani mtu aliyepora mashamba ya wananchi ndiye aliyepewa tenda ya kuuza mifugo yao.

Lakini Kanuni ya Mungu ile ya KILA UBAYA UTALIPWA ingali bado inafanya kazi.

Mungu wabariki wananchi wa Mbarali .

==
LEO, ng’ombe 433 waliokamatwa katika eneo la ardhi oevu ya Bonde la Ihefu, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wilayani Mbarali wanatazamiwa kupigwa mnada mkoani Mbeya.

Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kufanya oparesheni ili kuondoa zaidi ya mifugo 200,000 iliyovamia eneo hilo.

Mbali na kuhatarisha ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, mifugo inahatarisha pia Mto Ruaha Mkuu.

Akitoa taarifa ya uvamizi wa bonde hilo la Ihefu, Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha, Godwell Ole Meng’ataki anasema katika kipindi cha miaka miwili wamekamata mifugo 12,758 katika hifadhi hiyo.

Anasema licha ya kuwatoza faini wafugaji kiasi cha kukusanya zaidi ya Sh bilioni 1.2 katika kipindi hicho, wafugaji wameendelea kurejesha mifugo ndani ya hifadhi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune anasema eneo lililotengwa kwa ajili ya mifugo katika wilaya hiyo linatosheleza mifugo isiyozidi 60,000, lakini wilaya hiyo ina mifugo zaidi ya 200,000.

Tatizo la mifugo kuvamia maeneo ya misitu haliko Ihefu pekee bali pia maeneo mengi, hasa katika mkoa wa Lindi, Pwani na Morogoro ambayo ina mito muhimu kwa ajili ya kutoa maji ya kunywa na hata mabwawa ya kuzalisha umeme.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, aliwahi kueleza namna misitu mingi ya mkoa wake inavyovamiwa na wafugaji, akisema baadhi ya wafugaji walioko Lindi wanazungumza lafudhi sawa na waliomaliza misitu mkoani Shinyanga ambako aliwahi kuhudumu pia kama mkuu wa mkoa.

Telack ambaye wasifu wake ni pamoja kusomea shahada ya uzamili katika maendeleo ya vijiji, Chuo Kkiku cha Sokoine cha Kilimo (SUA) anasema kilimo tunachosema ni uti wa mgongo kitashindikana kama hatutakuwa na misitu kwa sababu kilimo chetu kinategemea mvua na misitu ina nafasi kubwa ya kuvuta mvua na kulinda vyanzo vya maji.

Faida nyingine ya misitu kwa mwanadamu na viumbe hai wengine ni kunyonya hewa ukaa na kutoa hewa safi, kuwa makazi ya viumbe mbalimbali na kutoa miti-dawa.

Misitu huwezesha pia ufugaji wa nyuki, kutoa mbao za aina mbalimbali na nishati za kupikia kama mkaa na kuni na hasa kama vitu hivyo vitavunwa kwa njia endelevu.

Pamoja na kwamba Watanzania wanahitaji mifugo kwa ajili ya nyama na maziwa na pia kutoa ajira, ni wakati wa kuhakikisha wafugaji wanafuga kisasa, wanatumia maeneo waliyopangiwa, wanapunguza idadi ya mifugo na kulima malisho kwa ajili ya mifugo yao. Lazima wabadilike, ‘wahifadhi’ mifugo na si ‘kuichunga’.

Ni muhimu Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na viongozi wa mikoa mbalimbali kuboresha hali ya ufugaji ili kupunguza pia migogoro ya ardhi. Wahusika wasione kigugumizi kupiga mnada kila mahala ng’ombe walikovamia.

Chanzo: Habari Leo
Huu ni unyama na wizi wa walala hoi!
Viongozi husika Jitafakarini je mko sawa??!
 
Serikali ni wanainchi. hakuna inchi pasipo Wana inchi.wana inchi Wana miliki mifugo na mifugo imekutwa kwenye aldhi yao alidhi ambayo ni Mari ya serikari yao.kisha serikari inauza mifugo ya wanainchi ambao ndiyo ma boss wa serikali hiyo. Najiuliza je nihaki kufanya hivyo? Je kufanya hivyo hakuta tokomeza ufugaji? Je serikari haitambui Kama kina wafugaji maeneo Yale? Je wame wapa maeneo kwa ajiri ya ufugaji?isije ikawa wafugaji hawana maeneo ya machungo ndiyo maana wamegikia hatua ya kuingia mbugani. Kama ndivyo Basi nivema serikari iwa tengee wanainchi alidhi ya mifugo kabra hawaja waukumu hao wafugaji vinginevyo tutegemee tusiyo yajua na magum kuliko haya
 
Huko Songea/Ruvuma naona kuna wafugaji na mifugo yao wanahamia kwa kasi sana.

Sijui kama serikali ya mkoa haioni tatizo lolote kwa siku zijazo.

Baadhi ya viashiria vya hatari ni pamoja na mifugo kuingizwa katika mashamba ya mahindi yaliyo vunwa.

Sasa fikiria mkulima awe amelima mahindi yake kwa gharama kubwa za mbolea, halafu mfugaji anaingiza ng'ombe. Nini kitatokea hapo. Utulivu wa wakulima wa mkoa wa Ruvuma huenda ukabadilika, sababu wafugaji kupewa uhuru wa kuingia watakako.

Upande mwingine ni madhara ya uwingi wa mifugo kuvuruga mito, vijito na vyanzo vya maji. Bila shaka athari za muda mfupi na muda mrefu zita jitokeza.

Muda utaongea.
 
Hii story imejaa politics nyingi,mala mifugo ya wakulima inapigwa mnada,mala kampuni inayoendesha mnada ni ya Mbunge wa zamani wa ccm aliyeuziwa mashamba ya wakulima!!
Sasa hapa Kuna hoja kama nne,
Mosi,Hawa ngombe wa wananchi,mamlaka iimewafata kwenye makazi yao ikawchukua kwa nguvu,au wafugaji walivunja sheria kwa kuingiza mifugo kwenye hifadhi,serikali ikakamata hiyo mifugo.!
Pili Huyu Mbunge wa zamani,kosa lake lipo wapi kuuziwa mashamba na kampuni yake kupewa kibali,Tena na mahakama ya kusimamia mnada,kwani utaratibu haukufwatwa?
Tatu,kwanini wafugaji hawana eneo la kunyweshea mifugo?walitengewa eneo au la!!
Nne,Hayo mashamba wanayodai,wamepolwa,ni kiasi gani walikuwa wanazalisha,wanalipa Kodi kiasi gani,na huyo Mbunge aliyeuziwa ana plan ya kuzalisha kiasi gani?na kulipa Kodi kiasi gani?
Chadema hufatilia issues ambazo zinawapa milage
 
Ufugaji wa kuhamahama unapaswa kufika mwisho sasa, unchangia uharibifu mkubwa wa mazingira.
 
Ufugaji wa kuhamahama na biashara ya mkaa vitaleta janga la kimazingira, udhibiti wa nguvu unahitajika.
Ufugaji wa kuhama hama hauna nafasi tena kwenye Karne hii ya 21. Kama mtu hawezi kufuga kwa kutulia auze tu ng'ombe wake wote. Tukiwachekea wafugaji siku si nyingi nchi hii itageuka jangwa
 
Back
Top Bottom