Mbaroni kwa kumkamata, kumshambulia na kusambaza picha za utupu za waliyemfumania

Mbaroni kwa kumkamata, kumshambulia na kusambaza picha za utupu za waliyemfumania

Hawakuwafumania hao wote waliokamatwa ni mwanaume na ndugu zake ndio walifanya kitendo hicho, huyo dada namfahamu vizuri waliaashaachana na huyo mwanaume zaidi ya miezi mitatu, na kila mmoja kuwa na maisha yake, kinachowauma ndugu ni huyo dada alitolewa kijijini walitegemea baada ya kuachwa angeyumba, matokeo yake amezidi kupendeza.

Na akapata mwanaume mwingine akawa anaishi nae, hao ndugu baaa ya kupajua alipokuwa anaishi wakapanga mpango huo wa kumvamia kwenye nyumba aliyokuwa anaishi na mume mpya lengo kumzalilisha na kumkomoa tu .

Waliwavua na nguo na kuwapiga wenyewe acha wakenyee ndoo kwanza akili ziwakae sawa
Walimuombea adui njaa ila hawakufanikiwa shwaini zao
 
Yani wananchi sijui wakoje , mtu anaingia na kufanya fujo kwa kusingizia kuwa kamfumania alafu wapo tu si mwenyekiti wa mtaa au kitongoji yani watu wanaweza kufanya mauaji alafu watu wapo tu... kitendo cha kupiga , kufunga kamba na kuwatembeza watu njiani wakiwa uchi hii sio sheria , ukimfumania mtu vyombo vya sheria vipo kwanini uchukue maamuzi ya kupiga wakati hauna hayo mamlaka, na sisi wananchi tunaangalia tu lakini tujue kuwa tunaruhusiwa kuingilia kati sio kuangalia na kushangilia tu...
Watanyea debe kwa ushamba wa mapenzi!
 
Hawakuwafumania hao wote waliokamatwa ni mwanaume na ndugu zake ndio walifanya kitendo hicho, huyo dada namfahamu vizuri waliaashaachana na huyo mwanaume zaidi ya miezi mitatu, na kila mmoja kuwa na maisha yake, kinachowauma ndugu ni huyo dada alitolewa kijijini walitegemea baada ya kuachwa angeyumba, matokeo yake amezidi kupendeza.

Na akapata mwanaume mwingine akawa anaishi nae, hao ndugu baaa ya kupajua alipokuwa anaishi wakapanga mpango huo wa kumvamia kwenye nyumba aliyokuwa anaishi na mume mpya lengo kumzalilisha na kumkomoa tu .

Waliwavua na nguo na kuwapiga wenyewe acha wakenyee ndoo kwanza akili ziwakae sawa
Mkuu una uhakika walipeana talaka......au waliachana kimasihara.
 
Huwezi kuchunga mtu mzima. Ukimfumania mkeo
1. Umsamehe na mrudiane
2. Muachane
N. B
Kuwapiga picha au kuwachukua video ni uvunjifu wa sheria
Kumlawiti au kumpiga wagoni wako ni uvunjifu wa sheria
Hayupo binadamu yoyote duniani anayemiliki mwanadamu mwenzio
Hata mtoto. Akiwa tumboni ni wako ila akizaliwa siyo wako tena
Kwann uende jela kwasabb ya mwanamke ambaye mekutana ukubwani?
Kugongewa wife kunauma aise, afande aombe yasimkute.🚶🚶
 
Huwezi kuchunga mtu mzima. Ukimfumania mkeo
1. Umsamehe na mrudiane
2. Muachane
N. B
Kuwapiga picha au kuwachukua video ni uvunjifu wa sheria
Kumlawiti au kumpiga wagoni wako ni uvunjifu wa sheria
Hayupo binadamu yoyote duniani anayemiliki mwanadamu mwenzio
Hata mtoto. Akiwa tumboni ni wako ila akizaliwa siyo wako tena
Kwann uende jela kwasabb ya mwanamke ambaye mekutana ukubwani?
Uko sahihi mkuu siyo sawa kuwatendea hayo ya ulawiti pia kuwapiga picha ila nilichosema mimi ni kugongewa kunauma sana ila sijajustify kwamba wafanyiwe unyama wakikutwa.
 
Kugongewa kunauma ila huwa haiepukiki km mwanamke kaamua.
Huwa tunalawaumu bure na kuwafanyia unyama wanaume wenzetu ila hawana makosa 100%. Wanawake waliolewa hawana alama
Kosa lipo kwa mwanamke mwenyewe. Mwanamke hata km ni mkeo upo naye kitandani akikataa kutoa mzigo huwezi kufanya chochote.
Uko sahihi mkuu siyo sawa kuwatendea hayo ya ulawiti pia kuwapiga picha ila nilichosema mimi ni kugongewa kunauma sana ila sijajustify kwamba wafanyiwe unyama wakikutwa.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwarekodi video za utupu watu wawili wanaodaiwa kufumaniwa na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Singiba Buchadi (42) ambaye ni fundi umeme na mfanyabiashara Dephina Buchadi (42).

Kamanda Muliro amewataja wengine kuwa ni Doratea Mathayo (39), Wilbard Teobard (55), Albert Buchadi (30), Valenzi Silvester (40).

Amesema kuwa watuhumiwa hao wote ni wakazi wa Kongowe Wilaya ya Mkuranga.

“Vitendo vya kikatili walivyovifanya watuhumiwa hawa ni pamoja na kutoa adhabu wakati wao si mahakimu wala majaji, vitendo hivi havikubaliki kisheria katika nchi inayofuata mfumo wa utawala wa sheria na kwa sababu hizo watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo,”alisema Muliro.

Huyu yeye hakupigwa wala nini...ila..!!!
 
Huyo mwamaume na ndugu zake hawana akili, yan walimpeleka huyo mama hadi kwa watoto na wakamuona mama yao bila nguo,mtoto wa kike akarudi ndani huku akilia
 
Naona tunaotembea na wake za watu tunahangaika kupata video tujue adhabu gani mpya kagewa mshirika mpaka polisi wameingilia kati
 
Back
Top Bottom