Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Mkuu uko sahihi, kama Lowassa alikuwa na hizo nguvu akiwa na miezi miwili ndani ya cdm, je akiwa na miaka miwili nguvu zake zilienda wapi?Maalim Seif na Lowasa hawa watu walikuwa ni taasisi, kama huzijui nguvu zao basi huzielewi vizuri siasa za Tanzania.
Licha ya wizi wa kura Lowasa alipata kura million 6, Arusha aliongoza Lowasa, Zanzibar aliongoza Lowasa kwa influence ya Maalim Seif na huu ni ushahidi wa wazi aliyeshinda Urais Zanzibar alikuwa Maalim Seif na Dr Shein alishakubali kushindwa.
Maalimu Seif alikuwa na nguvu za kweli za kisiasa huko Zanzibar, ningebisha hapa hapo ningekuwa sijui vizuri siasa za Zanzibar. Mkuu hizo nguvu za Lowassa Mimi sikuziona zaidi ya kuwa na hela za kuhonga Ili kupata publicity. Cdm bila Lowassa ingepata kura ilizozipata na hata zaidi.
Kikubwa zaidi bila Lowassa cdm ingebaki na sifa yake ya kitaasisi badala ya kuokota mgombea aliyekuwa haamini kwenye itikadi Yao, zaidi ya kusaka madaraka. Katika hilo viongozi wa cdm walitukosea sana tuliokuwa tunataka mabadiliko ya kweli. Au mkuu ww ndio ulitoa ushauri kwa cdm kuokota yule mgombea wa vodafasta aliyekuwa mgonjwa, hata kuongea jukwaani alikuwa hawezi 😂