Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
- Thread starter
- #21
Kasongo yeyeeee ππππ wqkati inachanganyika huko tumboni ulikuwa unajiona nani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kasongo yeyeeee ππππ wqkati inachanganyika huko tumboni ulikuwa unajiona nani?
Hapo kwenye kila mavi yatatoka nimecheka kwa sauti mpaka watu wananishangaa..!! Wallah JF ni kumanyokoli kabisa na sihami ng'weeeeeee..!!Ni dawa ya kusafisha tumbo
Yani Kila mavi yatatoka tumboni iwe magumu mepesi meusi hadi maji yatatoka
Dawa yake ni unywe maji bariiiiiiiidi na chungwa ndio yanakata
Hii kitu sio poa Bora castor oilMatumizi ya mbegu za mbarika (mnyonyo) kiafya
Mnyonyo ni mbegu zinazotokana na mti wa Mbarika. Sasa mwenye kujua zaidi atuhabarishe, manake hizi mbegu mi nasikia ni zaidi ya dawa!! Kwa niliyoyasikia hasa toka kwa wazee wa zamani ni haya, naomba kujua ufafanuzi kwa mwenye kufahamu zaidi manake inaweza kusaidia wengi: - Kwanza inatumika...www.jamiiforums.com
Hakuna aliyetumia hiyo dawa na akarudia haifaiHapo kwenye kila mavi yatatoka nimecheka kwa sauti mpaka watu wananishangaa..!! Wallah JF ni kumanyokoli kabisa na sihami ng'weeeeeee..!!
Tupe uzoefu..!! Maana sentensi hii imekaa kiuzoefu haswaa..!!Uharo wake ni kama maji tu yamefunguliwa koki ni mwendo wa π¨π¨π¦π¦π¦π¦π₯΅π₯΅π
Na ungelimieza mbegu 3 za mnyonyo ungelikuwa ni RIp usingeweza hata kuja kuandika kitu hapa ungelikuwa ni marehemu usitumie hizo mbegu ni sumu kwa binadamu.Mbegu mbili unaweza kuharisha mpaka ubongo ππ
View attachment 3159973
Wauzaji muwe mnasema kuwa tukimeza tusiende kazini
Kumbe ubongo wako upo kwenye utumbo mpana?Mbegu mbili unaweza kuharisha mpaka ubongo ππ
View attachment 3159973
Wauzaji muwe mnasema kuwa tukimeza tusiende kazini
Ndugu Magical power embu toa ushahidi hapa. Wewe ulirudia?Hakuna aliyetumia hiyo dawa na akarudia haifai
Labda alihisi ini linavurugwa na linahamia matakoni huku likiwa rojo..!!ππ wqkati inachanganyika huko tumboni ulikuwa unajiona nani?
Heeh...! Mkaburi tena?Mkaburi π₯π₯
Mbegu za mnyonyo huruhusiwi kula mbegu mbili unaweza kufa wakati wowote ukila mbegu za mnyonyo zaidi ya moja.Mbegu mbili unaweza kuharisha mpaka ubongo ππ
View attachment 3159973
Wauzaji muwe mnasema kuwa tukimeza tusiende kazini
Sasa utaratibu gani huo, kwamba tumia mbegu moja,ukitumia mbili unakufa, halafu ina masharti kibao utafikiri maabara za silaha za nuclearHii kitu sio poa Bora castor oil
Majani yake ukiwa unaumwa na jino tafuna.LINAPOA.Mbegu za mnyonyo huruhusiwi kula mbegu mbili unaweza kufa wakati wowote ukila mbegu za mnyonyo zaidi ya moja.
FAIDA MBALIMBALI ZA MTI WA MNYONYO
![]()
Mti wa mnyonyo una faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Karibu kila kitu kinachopatikana kwenye mmea wa mnyonyo kina faida za kiafya kwa mwanadamu.
Majani ya nyonyo ni tiba ya kifua kikuu na mizizi yake ni dawa ya mafindofindo, kuungua, macho yanjano, uvimbe, koo, kisonono na kaswende.
Kikonyo chake ni dawa ya kwikwi.
JINSI YA KUTUMIA MMEA WA MNYONYO KUJITIBU MAGONJWA & MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA.
i. Kwikwi :
Jaza maji kwenye kikonyo, mpe mgonjwa anywe kila baada ya dakika 3 mpaka kwikwi iishe.
ii. Kuungua :
Meza punje za mti wa nyonyo kwa maji kiasi cha glasi moja kwa siku kwa muda wa siku tano.
iii. Kutibu miguu inayo uma :
Tumia majani kwa kufungia miguu inayouma.
iv. Maumivu Ya Mgongo :
v. Majani yake ukiyapasha moto yafaa kukanda mgongo wenye maumivu.
vi. Kutibu Kaswende na Kisonono :
Ponda mizizi ya mti wa mnyonyo, kisha chemsha na tumia kunywa glasi moja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.
vii. Kuondoa Kondo La Nyuma :
Mizizi ya mti wa mnyonyo ikitafunwa na mama mjamzito yafaa kwa kutoa mfuko wa uzazi ( kondo la nyuma ) kwa urahisi na usalama zaidi.
Myonyo/Mbarika (Castor)
Mnyonyo (KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka (KiRusi) ni mmea wa jamii ya Mbono Kaburi, kwa jina la kitaalamu Japtropha - nitauzungumzia siku zijazo.
Baadhi ya faida za mnyonyo na mazao yake.
Mbali na kuweza kutumia mnyonyo kama uzio hai, njia hii inaweza kutumika kwa wale wasio na eneo kubwa la shamba ndiposa wakapata faida zake kama ifuatavyo:
Majani ya mnyonyo yanaweza kutumika kama tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kukanda (massage) ili kuondoa maumivu na majani haya yakifungwa kwenye mguu unaouma huleta nafuu hasa kwa maumiviu yanayokuja baada ya kuteguka, pia hutumika kutibu uvimbe kwa wanyama.
Mizizi ya mnyonyo huweza kutumiwa kama dawa ya mafundo fundo, uvimbe, kuungua, macho ya manjano, kuumwa koo na magonjwa ya kuambukiza ya kisonono na kaswende. Ukijaza maji baridi kwenye kikonyo cha mnyonyo na kumpa mtu mwenye kwikwi kila baada ya dakika mbili au tatu hivi, mara nyingi huondoa usumbufu unaoletwa na kwikwi.
Mbegu/Punje/Tunda/Njugu
za mnyonyo zikimezwa na maji bilauri moja kila siku kwa muda wa siku tano huweza kutibu maumivu yaliyosababishwa na kuungua. Vile vile, mbegu hizi huweza kusagwa na kisha kuenguliwa mafuta kwa ajili ya kulainisha mashine na mitambo viwandani.
Mbegu za mnyonyo kabla ya kukomaa
Mafuta yatokanayo na mbegu za nyonyo mfano Ricinoleic Acid, Oleic Acid, Linoleic Acid nk hutumika kutibu ugonjwa wa wa jongo (rheumatism) unaowakumba watu wengi wanaoishi maeneo ya miinuko na baridi, pia hutibu ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalamu kama arthritis na gauti.Mafuta ya mnyonyo pia yanaweza kutumika kama njia ya
kupanga uzazi
kwani yana kiasi fulani cha sumu ya protini ijulikanayo kitaalamu kama ricin ambayo ikitumiwa kwa kiasi kidogo huharibu utungo, huweza pia kutumiwa kama mafuta ya kupaka ama losheni katika sehemu za siri ili kuua mbegu za uzazi za kiume wakati wa tendo la kujamiiana. zazi wa mpango.
Tahadhari:
Mnyonyo ni mti wenye sumu inayoweza kuua binadamu au wanyama endapo itatumika kuzidi kipimo.
Mbegu za mnyonyo baada ya kukomaa
- Mazao yoyote yatokanayo na mnyonyo huhatarisha au/na kuharibu mimba na hata kuweza kusababisha kifo cha mjamzito, hivyo, matumizi yake lazima yawe ya uangalifu mkubwa.
Mafuta ya Ricinoleic acid yanayopatikana kutokana na mnyonyo vile vile yanaweza kutumika kurekebisha hedhi (mzunguko wa damu ya mwezi kwa wanawake) ikiwa mzunguko umechelewa ama kusimama katika umri usiotarajiwa. Huweza pia kupunguza maumivu makali yanayotokea wakati wa hedhi.
Mafuta ya mnyonyo yanayojulikana kitaalamu kama Undecylenic Acid huweza kutumika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi na vidonda vinavyosababishwa na bakteria ama ukungu (fungus).
![]()
Akina mama wanao nyonyesha
pia wanaweza kutumia mafuta baridi ya mnyonyo kiasi kidogo ili kuepuka madhara ya mafuta hayo kwa mtoto, kumbuka hapo awali nimeandika kuwa mafuta haya yakitumiwa kwa kiwango kikubwa ni sumu kuongeza wingi na mtiririko rahisi wa maziwa
Mnyonyo unaweza pia kuwafaa watu wanaoishi na VVU (Virusi Vya UKIMWI) kwani mafuta yake ni sumu ya kuua vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na ukungu (fungus)
![]()
- Kupakaza: Chukua kipande cha nguo ama kitambaa, kisha kiloweke kwenye mafuta ya mnyonyo ndipo ufunge katika kiwiko ama eneo lenye maumivu ama kidonda. Vinginevyo, chukua kiasi cha mafuta na kupaka eneo linalohusika mfano, penye kidonda, kuugua ama pakaza kichwani au juu ya tumbo wakati wa maumivu ya hedhi nk. Unaweza kuacha kwa muda wa saa moja kabla ya kunawa ili uipe ngozi muda wa kunyonya kiasi cha mafuta. Unaweza kujifunga kitambaa hicho tumboni ama mgongoni kama kibwebwe na kuendelea
![]()
- na shughuli za kawaida
Kunywa: Chemsha mbegu chache za mnyonyo pamoja na maji na maziwa kisha unywe kiasi kidogo kadiri ya nusu hadi bilauri moja ya ujazo wa mili lita mia mbili na arobaini.Kusafisha utumbo: Kunywa mafuta ya mnyonyo vijiko viwili vikubwa vya chakula asubuhi, kisha pumzika kwa saa mbili ndipo unywe maji glasi mbili na endelea kunywa maji glasi moja kila baada ya saa moja.
Yeah ndo dawa YANGU pendwaNdugu Magical power embu toa ushahidi hapa. Wewe ulirudia?
Dah! Hiyo ilinifanya nikimbilie hospital, jamaa aliniambie nitumie tatu kubababake. Ila sikuhizi nikitaka kuflash hua nakula robo tu.Kidogo iniue ,inaitwa habat mulik,ukila utaharisha sana ila dawa yake ni maji ya kwenye friji.ila mbegu zake ni sumu,ni Bora utumie Castrol oil
Hujasoma komenti zote ndo maana ukaja na huu uharo kama umemeza mbegu zinazojadiliwa..!!mtoa mada na walio comment huko juu wote wapuuzi...mnabwabwaja tu kama wote tunajua hizo ni takataka gani mnajadili...yaani koment zaidi ya 20 hakuna hata mmoja aliyesema hivo ni vitu gani na vinatumika kwa shida ipi na huyo mtoa mada alitumia kujitibu nini hadi akatapika ubongo na kweli alipost bila kuwa na ubongo ndio maana hajaeleweka ni watumiaji wenzake tu wa hio kitu ndio waliomuelewa na comment zao ni kama wamekatwa vichwa hata haijulikani wanajadili nini...
Hvi wanaowaambia wenzao watumie mbegu hizo, hawatoi prescription?Na ungelimieza mbegu 3 za mnyonyo ungelikuwa ni RIp usingeweza hata kuja kuandika kitu hapa ungelikuwa ni marehemu usitumie hizo mbegu ni sumu kwa binadamu.