Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu Castr, mimi nimefanya ubalozi wa Uingereza. NV ni Note Verbale, ni document ya mawasiliano ya kibalozi, tulipoungana Balozi wa Tanzania UN, Chief Erasto Mang'enya aliwasilisha NV kutoka serikali ya Tanganyika kuiarifu UN kuwa tumeungana na Zanzibar sasa ni nchi moja. Balozi zote wakitaka kutembelea popote nje ya mawanda ya ubalozi, lazima kwanza watume NV MFA kuomba ruhusa na MFA wanatoa NV kuruhusu ndipo balozi anasafiri.Uliwahi sema umefanya kazi Ubalozi wa Marekani hivyo basi ulichoandika hapa sina sababu ya kukikataa labda nikajisomee ili kuongezea nyama kutokea hiki kidogo nilichokiona.
MFA naamini ni Ministry of Foreign Affairs, hii NV nashindwa kuzalisha full form yake, ninaomba unisaidie. Sasa kutokana na nilichowahi kusoma n.k niliwahi soma ya kwamba balozi haguswi na sheria za nchi aliyopo na kwamba ubalozi unahesabiwa ni nchi kiasi kwamba balozi anaweza fanya uhalifu akiwa majengo ya ubalozi na nchi mwenyeji akashindwa ingilia.
Niliwahi soma mifano ya hapo juu kwa balozi Georgi Ivanova wa Bulgaria akiwa Washington na Aljubeir wa Saudi Arabia akiwa New Mexico.
Kwanini ishu ndogo kama kutembelea sehemu ihitaji MFA iingilie?
Eneo la ubalozi wowote linahesabika ni nchi hisika, hata wewe ukifanya uhalifu wowote na kukimbilia ubalozi wowote, polisi hawawezi kukukamata wataishia getini!.
Sababu za kuomba kibali ni ili kuzuia Ujasusi hata kwako mgeni akija akafikia kwako, utamuonyesha chumba chake, sitting room na rest room. Siku ukimkuta anapekua chumbani kwako lazima utashangaa. Hivyo Balozi hawezi kujiendea popote ugenini
Hili la Balozi kujiendea popote, niliwahi kulileta humu, Ujasusi wa Balozi wa Uingereza: Tanzania, Can We Stand Au Maselle Kugeuzwa Mbuzi wa Kafara? na kufuatia mimi kufanya kazi ubalozini, nimewahi kuandika makala elimishi kuhusu ubalozi Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?
P