Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Hii nchi kuna mji uliopangika vizuri??
Kote ni za uso tu.
Miji yetu ni vijiji vikubwa, hatua mbili mbele unakutana na slums ni kama magomeni na posta au kigamboni na poata yani ukivuka maji tu tayari uabubwada hui hapa.

Mbeya nawatetea bado wanalitengeneza jiji lao.

Majiji ya zamani yaliendelezwa sana na watu wa makabila ya huko, mfano watu wa kaskazini wameendeleza sana huko kwao.

Huku Mbeya kulikua na wasafwa, hawa watu hawawazagi madndeleo ya jumuia.
Walivyofika wageni wengi mbeya ndio imeanza kubadilika sasa.
 
Tunataka kuwasaidia tuwavushe kutoka mji wa kijima mpaka mji ufanane angalau kama singida kwa mpangilio naona anashipaza fuvu kama zamadamu.
Nachoipendea Kula misosi tu Ila Jiji bado sana shida mjini sio Kwa wanyakyusa wamejaa Wasafwa wanafeli wapi nimekumbuka Savoi,moondust,SAE,Iwambi na Forest [emoji2][emoji2]
 
Ukiacha mpangilio Kuna jipya jingine umeliona huko kwingine?

Haya umetaja Tabora,Mwanza Ina mpangilio gani ukiacha

Mipangilio ya miji yetu mingi inareflect thinking capacity tuliyonayo wala sio vinginevyo. Na hii ni kwa Africa nzima I think wala sio kwa bahati mbaya.
Mh,mkuu Kuna baadhi ya miji Afrika ni mizuri mkuu,ebu jaribu kusearch miji ya Nigeria ya kawaida tuu,ila Angalia miundombinu na planings zao
 

Attachments

  • Screenshot_20230614-200521.png
    Screenshot_20230614-200521.png
    358.5 KB · Views: 12
  • Screenshot_20230614-200521.png
    Screenshot_20230614-200521.png
    358.5 KB · Views: 10
Kama umetembea sana duniani huko au kama haujatembe jitahidi utembee na ukirudi ndiyo utagundua kwamba dar es salaam ni kijiji kilichochangamka tu
Hilo nalo ni likijiji la kijamaa linalowakutanisha wavuvi kutoka sehemu mbalimbali, jiji kila sehemu ni harufu ya vibua, harufu ya maji machafu, jiji limejaa slum basi watu wanajiona wapo NYC.
 
Nachoipendea Kula misosi tu Ila Jiji bado sana shida mjini sio Kwa wanyakyusa wamejaa Wasafwa wanafeli wapi nimekumbuka Savoi,moondust,SAE,Iwambi na Forest [emoji2][emoji2]
Ukiona jiji lina gharama ndogo jua hapo hakuna mzunguko wa pesa.
 
Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city, hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla in typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.


Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)


Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako [emoji817]. Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

Huna akili wewe
 
We mluga luga acha ushamba na unatakiwa kutembea uone miji, hilo vumbi na nyumba za tembe za hapo mbeya basi unaona mbeya ni jiji zuriii kama Las vegas
Nimetembea sana hasa Mwanza nilichokiona ni mara 1000 Mbeya, yaani Mwanza ya mabanda ya nguruwe ndio mtu anaweza sema ametembea? Acha ujinga wewe ngumbaru
 
Mtoa mada ni mtu wa Iringa na anaishi mbeya kwasasa, mnataka kusaidiwa ili gulio lenu livutie lakini unajifanya mjuaji hii yote ni Tanzania naweza kutaka kuishi huko mbeya lakini kama hakuna facilities za msingi sitaweza kuwekeza huko.
Sasa mtu wa Iringa kwenye mabanda ya udongo nae ana nini Cha kuongea? Huyo akawaringishie Simiyu sio Mbeya 😁😁
 
Leta hoja tukuparure na limji lako la ajabu.
Baada ya Dar na Dom ,Mbeya ndio Jiji litakuwa na dual carriage ndefu kushinda takataka yeyote hapa Tanzania km 35..

Mbeya ndio Mkoa wa kwanza Tanzania utapata Dual Carriage road ndefu ambayo ni highway ya km 215 igawa-Tunduma so mtakuwa mnakuja kupiga picha 😆😆
 
Nimetembea sana hasa Mwanza nilichokiona ni mara 1000 Mbeya, yaani Mwanza ya mabanda ya nguruwe ndio mtu anaweza sema ametembea? Acha ujinga wewe ngumbaru
Nan ameleta mambo ya Mwanza, hiyo mwanza siijui na wala sijawahi kwenda, lakini mjitahidi kwenye suala la makazi na mpangilio wa mji sio kila sehemu mnaweka vibanda na bado barabara hazipitiki.
 
Baada ya Dar na Dom ,Mbeya ndio Jiji litakuwa na dual carriage ndefu kushinda takataka yeyote hapa Tanzania km 35..

Mbeya ndio Mkoa wa kwanza Tanzania utapata Dual Carriage road ndefu ambayo ni highway ya km 215 igawa-Tunduma so mtakuwa mnakuja kupiga picha 😆😆
Hiyo highway ndio itabadirisha uchafu na maudongo ya mji wenu, raha ya jiju ni skyscrappers na mpangilio mzuli ikiwemo shopping centres, recreational parks, malls na barabara za uhakika.
 
Back
Top Bottom