Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mwanza sio Mji ni slums everywhere,huna hata aibu?
Hivi wewe kwenu ni wapi ulinganishe na Mwanza? watu wameshakwambia Mbeya ilikuwaje ikawa jiji hauwelewi. Mwanza imepimwa CBD yote, Nyegezi yote, Buswelu yote, Nyamongolo yote, Igoma yote, Ghana yote, Nyamanoro yote Nyakato yote! hivi haunaga aibu kulinganisha Mwanza na vimiji vyako hivyo?.Mwanza ile inayojengwa daraja refu nchini km 3.2,daraja la juu la sgr (Viaduct)km 1.4,soko kubwa pale City Center, stend 2 za maana, meli kubwa kuliko yoyote nchi hii.Tuwe wakweli tu Mbeya bado sana kwa Mwanza tuache chuki za kijinga hazitusaidii nchi hii ni yetu sote hata Mwanza ni kwetu wote wa Tanzania. All in all Mwanza is most developed City by everything after Dar es Salaam.

Sent from my D6503 using JamiiForums mobile app
 
Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city, hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla in typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.


Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)


Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako [emoji817]. Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

Ndiyo limeshakua Jiji sasa amua.
 
Wewe kinachokusumbua ni ushamba,Sasa ni hivi hizo malls kajenge wewe huko kwenye Miji ya Kisasa,Mbeya hawazihitaji Wala hawana shida na ndio maana wawekezaji hawawezi kujenga huo ujinga..

Tena hapo Kabwe Pako safi kabisa sio sawa na Kariakoo kukikomwagwa bidhaa Hadi sehemu ya kupiga hakuna au Mbagala kule Kuna nuka Kila sehemu Sasa umewahi sikia Mbeya inanuka?

Unaposema Watu wa Mbeya hawazihitaji, unaongea kama nani sasa , mkuu wa mkoa au mbunge wa mbeya au Mayor? Wewe ni msemaji wa watu wa mbeya ? Kaa kwa kutulia mshamba mmoja wa umalila.
Sisi watu wa mbeya tunataka hivyo vitu , tunataka shopping malls , tunataka kumbi za Cinema , tunataka kila aina ya maendeleao. Mambo ya vumbi la mwanjelwa na soweto inatosha.
 
Unaposema Watu wa Mbeya hawazihitaji, unaongea kama nani sasa , mkuu wa mkoa au mbunge wa mbeya au Mayor? Wewe ni msemaji wa watu wa mbeya ? Kaa kwa kutulia mshamba mmoja wa umalila.
Sisi watu wa mbeya tunataka hivyo vitu , tunataka shopping malls , tunataka kumbi za Cinema , tunataka kila aina ya maendeleao. Mambo ya vumbi la mwanjelwa na soweto inatosha.
Kama mwana Mbeya na ukiweka utafungasha mwenyewe..

Nyinyi watu wa Mbeya wewe na nani? Jenga Sasa unataka nani akujengee? Hayo ma Mall yangekuwa yanahitajika yangeshakuwepo kitambo,what's so special Kwa hayo ma hall mnaita mall?

Mwisho badala ya kuhangaika na huo ushamba wa mall ungekuwa unapigania Barabara za mitaa,Mpango Miji,na Gardens au Public Parks..
 
Kama mwana Mbeya na ukiweka utafungasha mwenyewe..

Nyinyi watu wa Mbeya wewe na nani? Jenga Sasa unataka nani akujengee? Hayo ma Mall yangekuwa yanahitajika yangeshakuwepo kitambo,what's so special Kwa hayo ma hall mnaita mall?

Mwisho badala ya kuhangaika na huo ushamba wa mall ungekuwa unapigania Barabara za mitaa,Mpango Miji,na Gardens au Public Parks..

upo Sawa , a reason tunasema mbeya ni kijiji fulani kikubwa, sababu hata akili kama zako ni typical mwanakijiji.
 
Okay tuondoe Mbalizi, tunabaki na Airport , uyole hadi igawilo, ilemi , isanga, meta, mabatini, soko matola , iganzu, gana, kote huko ni mavumbi mavumbini, mama Joni , ilomba, isyesye, uwata, kote huku uswazi.

Mara kadhaa nikiwa natokea chunya najaribu kupiga picha nipate view ya mbeya ila siipati, yaani hakuna angle utakaa upige picha ya jiji. Hakuna jiji pale. Hovyo kabisa . In short there is nothing to show off.
Mkuu kati ya mbeya na Iringa wapi kuna afadhali na bata kuliko sehemu nyingine naomba unielezee tofauti ya mbeya na Iringa.
 
Mkuu kati ya mbeya na Iringa wapi kuna afadhali na bata kuliko sehemu nyingine naomba unielezee tofauti ya mbeya na Iringa.

Kote huko hakuna hizo bata kama mtu umebahatika kusafiri duniani.
Although naweza Chagua Iringa over mbeya sababu Iringa ni pasafi Hapana Vumbi kama Mbeya , Iringa pana ustaarabu na utulivu sio chaotic, noisy na vurugu kama Mbeya , hata mji wa iringa kwa ujumla ni mzuri kuliko mbeya.
 
Ulivyo ongea kwa ukali utadhani kuna mtu kakulazimisha kuishi mbeya

Kila sehemu na utaratibu wao wa maisha hujapapenda sepa

Wengine tulipaona pazuri tu
 
FB_IMG_14596240700727249.jpg
nikiwa new york hapa niki wa-zoom tu mnavyowashambulia majirani zetu 🤣🤣🤣
 
Ulivyo ongea kwa ukali utadhani kuna mtu kakulazimisha kuishi mbeya

Kila sehemu na utaratibu wao wa maisha hujapapenda sepa

Wengine tulipaona pazuri tu

Hakuna utaratibu wa maisha unaosema mji uwe na vumbi, mchafu, hauna ustaarabu, na miundombinu duni. Mimi kama mlipakodi Nina haki ya kuyasema haya ikiwa yananikera.
 
Seems like uko na exposure ndogo ya sehemu kubwa ya Mbeya! Yapo machache unaweza kuwa sahihi!

Anyway, reli zijengwe mitaani Mbeya jiji? Unajua jiografia ya Mbeya kweli? Unajua nature ya ujenzi wa reli inavyotaka tambarale? Au unazungumzia subways?
Mbeya ni kijiji kikubwa huo ndio ukweli
 
Ukitaka kijua kuwa swala la mipangilio siyo moja ya utaratibu na tamaduni zetu , wewe nenda hata kaangalie sehemu au maeneo tunayowazika wapendwa wetu waliotutangulia ??.. jibu utakaro lipata kule basi ndiyo linalotoa picha halisi ya jinsi tulivyo..
 
Mimi home ni Mbeya lakini siwezi kusifia uchafu Mimi,nmetembea miji mingine ya nchi hii mbona wanajitahidi kuipangilia!hapo jirani zao Sumbawanga tuu imeiacha mbali Mbeya Kwa mpangilio mzuri,now nipo Tabora,pia huwezi fananisha mpangilio wa mji wa Tabora na Mbeya,hata Njombe wakituliza akili watatushangaza[emoji17][emoji17].

Mbeya tuna eneo kubwa sana,mipango miji wanasinzia.

Well said , CC huyu mbanga [mention]ChoiceVariable [/mention] , haya sasa hata tabora haoni ndani [emoji1787]
 
Back
Top Bottom