Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Who taught you Mbalizi ni sehemu ya jiji la Mbeya? Mbalizi ni wilaya ya Mbeya vijijini haina hata Mamlaka ya Mji!

Kwani master plan huja kufanya overall ya sehemu zote? Ndio maana kuna Manzese, Magomeni, etc unadhani Dar haina Master Plan?
Ona sasa hajui hata kama Mbalizi ni Mbeya vijijini😂
 
Mkuu umeielezea Mbeya kwa chuki zako binafsi za kutoipenda Mbeya.
Unaelezea kama vile Mbeya haina makazi bora.
Umewahi kufika forest mpya, forest ya zamani, Iwambi mpya, Isyesye mpya, Ituha, Block T, Itezi .....
Pia nieleze jiji lililopo Tanzania ambalo halina maeneo ya hivyo.
Acha chuki mkuu, Mbeya ni jiji zuri na itabaki kuwa hivyo.
Kwa hyo mbeya hapo town hamna nyumba za udongo na vumbi kama lote?
 
Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city, hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla in typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.


Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)


Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako [emoji817]. Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

Bora umesema wewe ...maana sisi Kila siku tunawaambia wanasema wivu ... mbeya sio Kijiji ni zizi..ni aibu mno to call such trash a city..ni fedheha Kwa nchi
 
Mkuu umeielezea Mbeya kwa chuki zako binafsi za kutoipenda Mbeya.
Unaelezea kama vile Mbeya haina makazi bora.
Umewahi kufika forest mpya, forest ya zamani, Iwambi mpya, Isyesye mpya, Ituha, Block T, Itezi .....
Pia nieleze jiji lililopo Tanzania ambalo halina maeneo ya hivyo.
Acha chuki mkuu, Mbeya ni jiji zuri na itabaki kuwa hivyo.

Akili za namna hii huwa ni ngumu sana kudeal nazo, especially kwa watu kama mimi wenye zero tolerance when it comes to dullness.
Watu wenye uelewa wame take hii criticism positive.
Chuki na mbeya , for what? Nimesoma sekondari huko na mwaka wangu wa kwanza wa career nlikaa hapo forest ya zamani.
Ukweli usemwe, miji ya Tz ina safari ndefu bado ila Mbeya is the worst of all.
 
hivi serikali ina mpango gani na lile shamba uyole pale? inabidi litoke wagawe viwanja
Unasema litoke wakati wamekazana kuongeza eneo. Kuna ekari 64 za wananchi wanataka kuzikwapua. Mwezi wa 5 walileta suma jkt wazungushe ukuta hilo eneo wakati watu wamejenga mijengo yao. Palichimbika aisee


Mkuu wa wilaya akaja akasema watafanya tathmini na raia watalipwa fidia wapishe chuo wachukue eneo lao. Raia wakagoma katakata na wakamwambia kama ni hivyo amlete Rais samia ndio awaambie la sivyo hawatoki [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Utajua mwenyewe
Ndo jiji sasa na tunapapenda pazuri afu inaonekana upajui vizuri au una matatizo yakulinganisha sana

Heheh ,
Kulinganisha ni muhimu. Kama wewe unaona ni tatizo basi wewe ndio tatizo lenyewe.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja. Mleta mada ameeleza kero pamoja

Hoja hunibiwa kwa hoja. Mleta mada ameelezea kero kwa undani na kisha kushauri nini kifanyike.
Ukweli usemwe, ahadi kuijenga mbeya ni nyingi kuliko uhalisia wenyewe. Kama utakumbuka vizuri, uwanja wa Songwe uliahidiwa tangu mwanzoni mwa 2000, kwa. Ba ungekuja kuwa wenye hadhi ya kimataifa. Lakini wewe mwenyewe unajua umekamilika lini na upo katika kiwango gani.
Soko la uhindini lilipoungua miaka ya 2003 serikali ikasema itashusha mall pale kubwa ya hadhi ya jiji. Lakini mpaka sasa wewe unamajibu kamili nini kipo pale.
Kuna soko la mwanjelwa, baada ya kuungua, vilevile wakasema kutajengwa Soko la kisasa litakalohudumia nchi za SADC😂, bilions zimeenda na soko wewe mwenyewe unaliona lilivyo.
Stendi ya mabasi, ilikua inajengwa ya pale Sai tuliamini sasa kulingana na routes nyingi za mabasi, basi stendi hiyo itamaliza changamoto zote na itakua ya kisasa kama ya Nyegezi au Nyamongolo za Mwanza. Wewe unamajibu kamili nini kilichojengwa pale.
Turudi kwenye City Garden. Kama unakumbuka waliahidi ile garden itawakutanisha watu pale kwa ajili ya mapumziko na refreshment nyingine. Lakini nikuulize wewe kama wewe umewahi kwenda pale au kuna eneo specifically Mbeya la mapumziko ya watu kama ilivyo Mwanza? Nadhani majibu unayo.
Turudi kwenye barabara ya njia nne. Wewe kama wewe umeanza kusikia tetesi za kujengwa lini?? Kwa mimi nnchokumbuka ilikua ni kujenga njia ya mchepuko kutoka uyole mpaka Mbalizi lakini si hii ya njia nne. Sasa hivi ile mwezi wa pili au mwanzoni mwa mwezi Marxh tuliona utiwaji wa sign ujenzi wa barabara hiyo. Kwa sasa ni miezi mitatu imepita, je umeona hata maandalizi ya awali ya ujenzi huo???
MAMBO NI MENGI, lakini ukweli ni kwamba huo mkoa utauona ni mzuri kama hujafika Mwanza au Dodoma pamoja na Arusha ingawa Arusha stendi ya mabasi ndio mtihani lakini si haba mji upo clean.
Vijana wanaukimbia huo mkoa nyumba za majengo nyingi hazina watu kabisa
Nani kakwambia watu wa Mbeya wanataka Mall mbona mnahangaika na vitu vya kijinga

Mbeya tunataka Barabara mitaani,Barabara kuu iwe poa,stand ya Mkoa ya Kisasa na Barabara za kuunganisha na Mikoa ya jirani na Mbeya tunataka cold facilities kwenye airport yetu.

Hizo habari za Mall and such nonsenses ni ushamba pelekeni huko kwenu.
 
Yenye vigezo ni ipi? Sweet Mbeya itawapasua bandama

This one nah ?
IMG_4495.jpg
 
Nani kakwambia watu wa Mbeya wanataka Mall mbona mnahangaika na vitu vya kijinga

Mbeya tunataka Barabara mitaani,Barabara kuu iwe poa,stand ya Mkoa ya Kisasa na Barabara za kuunganisha na Mikoa ya jirani na Mbeya tunataka cold facilities kwenye airport yetu.

Hizo habari za Mall and such nonsenses ni ushamba pelekeni huko kwenu.
Mbona mall za dodoma Huwa unazishobokea
 
Sasa kwani ukileta picha za zamani ndio itakusaidia nini bwashee?

Hizo aluminum sheets zinaonekana zimepauka sababu ya vumbi ,
Ndio maana huwezi nawiri ukiwa mbeya.
a reason I have said, and I say it again, suala la kupanda miti linatakiwa liwe ni kipaumbele kwa mbeya . Sioni ugumu kwenye hili hasa ukizingatia hali ya hewa ya mbeya ni rafiki.
 
Back
Top Bottom