Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Lakini polisi walivyokuwa wamewapa nafasi tangu Tundu Lissu amerudi, mliwasifu sana sasa mnawachokoza tena?
Richard ungekuwa ni timu, basi ungekuwa umeshuka daraja kwenye ujengaji wa hoja. Kusifiwa sio sifa ya kudumu. Ni sawa na mkulima kuisifia mvua iliyonyesha vizuri mpaka akapata mavuno ya kutosha. Siku hiyo mvua ikinyesha na kuleta mafuriko, usitegemee ataendelea kuisifia eti kisa kuna siku aliisifia baada ya kunyesha vyema. Kilichofanya polisi kusifiwa ni kwakuwa walifanya kazi kwa weledi, kinyume na tabia yao ya kunyanyasa wapinzani. Unaposema wanachokozwa unamaanisha nini? Au unaamini kwakuwa wao ni vyombo vya dola, basi wako juu ya sheria, na kitendo chochote cha kuwataka wafuate sheria ni kuwachokoza! Nyie ndio mnaomini kuwa polisi mara zote huwa sahihi, hivyo kumdhalilisha mtu ni sawa.