Mbeya: Mahakama imemuachia huru Gerald Mwakitalu (CHADEMA). Alifungwa maisha

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628

Tarehe 15/02/2022 Mahakama wilaya ya Kyela, Mbeya ilimpa hukumu Gerald Mwakitalu kifungo cha maisha kwa mashtaka ya kudaiwa kuchoma nyumba ya mgombea wa CCM wakati wa kampeni za uchafuzi 2020.

Leo 7/10/2022 ameshinda rufaa yake, amefutiwa hukumu hiyo, yupo huru.

======

Ni Gerald Mwakitalu aliyehukumiwa kutumikia adhabu hiyo Februari 15, 2022 kwa mashtaka ya kudaiwa kuchoma nyumba ya mgombea wa CCM wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020

Mwakitalu amefutiwa adhabu hiyo iliyotolewa kupitia Mahakama ya Wilaya ya Kyela baada kukata Rufaa ya kipinga hukumu.
 
Huu ni uthibitisho wa jinsi mafisi yasiyo na utu
 
Mahakama nyingi za Wilaya ni matawi ya CCM
 
Ilinishangaza sana. Yaani kudaiwa kuchoma nyumba ndiyo mtu anafungwa kifungo cha maisha??
Ndio hukumu kwa mtu yoyote anayepatikana na hatia ya kuchoma jengo au shamba. Ndio maana ninasema mawakili wa chadema ni vilaza.
 
Ndio hukumu kwa mtu yoyote anayepatikana na hatia ya kuchoma jengo au shamba. Ndio maana ninasema mawakili wa chadema ni vilaza.

Hii kumbakiza watu kesi tumeweka kwenye rekodi, wakati sahihi ukifika tutadili na wahusika wote wa matukio haya.
 
 
UCCM na ushetani ni vitu viwili vinavyonipa wakati mgumu sana kuvitenganisha. Kijana wa watu katumikia kifungo cha muda wote huo kwa kuwa tishio kwa shetani kutimiza majukumu yake!

Unamkuta kiongozi wa CCM anaongea kama vile CCM imeingia madarakani mwezi moja uliopita. Anasahau alipozaliwa CCM ilikuwa madarani na bendera ya CCM ikipepea chumbani alikozaliwa.

Yeye kalelewa, kakua, kakomaa na sasa naye karithi mkoba wa wazazi wake. Muangalie anavyokaza shindo akidai CCM ni chama imara na yeyote yule atakayethubutu kusema tofauti anyooshwe.

Anyooshwe, ashughulikiwe, apotezwe...yote sawa tu.Tundu Lissu alishughulikiwa, Ben Saanane alipotezwa, Gerald Mwakitalu amenyooshwa; CCM ni ile ile, iko pale pale. ni wale wale na kazi iendelee...kwa kweli shetani hana ndugu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…