Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

Mods mumeamua kulinganisha Uzi kwenye mada inayowafurahisha Kwa heading yake si ndio? πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Haiondoi ukweli huu hapa πŸ‘‡
 
#Jaji Ndunguru: Tunakubaliana na hoja ya Waleta Maombi, kwamba ibara za IGA imevunja sheria za ulinzi wa Rasilimali, kwa kupeleka migogoro nje ya nchi.

Hata hivyo, dosari hiyo haitatumika kuutangaza IGA kuwa ni batili.

#Jaji Ndunguru: Uandishi bora wa vifungu
vya IGA unaweza kurekebisha Vifungu hivyo na kuondoa dosari hii.

Tunashangaa kwamba IGA itaongozwa na sheria za nchi, na mikataba ya miradi itaongozwa na sheria za ndani lakini migogoro yake itatatuliwa nje ya nchi.


Chaliii pwaaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huu mkataba unaligawa Taifa lenu, wananchi wengi hawautaki, na hao ndio wenye nchi, hata Kama mkataba ungekuwa hauna shida ila wenye nchi wameukataa
 
Chaliii pwaaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Yani nashangaa unachoshangilia nini?

Ukiisikia Hukumu inasikitisha kiasi unaweza sema tuna mihimili bendera kabisa! Mahakama inapata shakha ya wazi kwa Dubai kuingia mikataba ya kimataifa alafu bado inashindwa kusema mkataba ni Batili? Nawe mwananchi unashangilia kwa maamuzi haya?

Mahakama inakiri kuwa Sheria za ulinzi wa rasimali za Taifa zilikiukwa na bado inasema haiwezi kubatilisha Mkataba? Kwaiyo wewe unaweza kufanya kitu kinyume na sheria alafu kikawa halali?
 
Sasa vifungu kama vilikiuka sheria si ndiyo ubatili wenyewe? Hii si ni kama ku "sugar coat" sheria
Utabadilishaje vifungu wakati mkataba umesainiwa?

Mahakama Mbeya yatupilia mbali kesi ya Bandari walalamikaji kukata rufaa​

d2dcd05a-5648-4a28-a656-735d5d587e67.jpg

Humphery Mgonja
BBC Field Producer
Mbeya

BBCCopyright: BBC
Mahakama Kuu nchini Tanzania hii leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inapinga mkataba (IGA) wa uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na falme ya Dubai.

Kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.
 
Alphonce Lusako ambaye ni mlalamikaji wa kwanza, kwenye kesi ya Wazalendo dhidi ya Serikali ya Tanzania ya kupinga Mkataba mbovu wa Bandari na DP WORLD, tayari yuko kwenye korido za Mahakama kwa ajili ya kuwasilisha kusudio la kukata rufaa.

Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imekiri kwamba Mkataba huo umejaa madudu ya kutisha, lakini imedai kwamba haiwezi kuingilia Mhimili wa Bunge.

Naye Wakili Mwabukusi ameipa serikali siku 14 tu kuufuta Mkataba huo kabla ya uamuzi wa kuwaamuru wenye nchi ambao ni Wananchi kuchukua hatua.

Kuhusu hukumu, soma Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya yatoa baraka Uwekezaji wa Dubai Bandarini
 
Yani nashangaa unachoshangilia nini?

Ukiisikia Hukumu inasikitisha kiasi unaweza sema tuna mihimili bendera kabisa! Mahakama inapata shakha ya wazi kwa Dubai kuingia mikataba ya kimataifa alafu bado inashindwa kusema mkataba ni Batili? Nawe mwananchi unashangilia kwa maamuzi haya?

Mahakama inakiri kuwa Sheria za ulinzi wa rasimali za Taifa zilikiukwa na bado inasema haiwezi kubatilisha Mkataba? Kwaiyo wewe unaweza kufanya kitu kinyume na sheria alafu kikawa halali?

Mahakama Mbeya yatupilia mbali kesi ya Bandari walalamikaji kukata rufaa​

d2dcd05a-5648-4a28-a656-735d5d587e67.jpg

Humphery Mgonja
BBC Field Producer
Mbeya

BBCCopyright: BBC
Mahakama Kuu nchini Tanzania hii leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inapinga mkataba (IGA) wa uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na falme ya Dubai.

Kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.
 
SOMA KURASA ZOTE ZA HUKUMU YA KESI :

IN THE HIGH COURT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
(MBEYA SUB-REGISTRY)AT MBEYA
(NDUNGURU, ISMAIL AND KAGOMBA, JJJ)

MISCELLANEOUS CIVIL CAUSE NO. 5 OF 2023

IN THE MATTER OF THE CONSTITUTION OF THE UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA, 1977 [CAP 2 R.E. 2002] AS AMENDED
FROM TIME TO TIME AND


IN THE MATTER OF A PETITION TO CHALLENGE PROVISIONS OF
THE CONTRACT AND PROCESS OF RATIFICATION OF THE
INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT BETWEEN THE UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA AND THE EMIRATE OF DUBAI (IGA) BY
THE NATIONAL ASSEMBLY OF THE UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA FOR BEING ILLEGAL AND UNCONSTITUTIONAL
BETWEEN

ALPHONCE LUSAKO.............................................. 1st APPLICANT

EMMANUEL KALIKENYA CHENGULA.................... 2nd APPLICANT

RAPHAEL JAPHET NGONDE................................... 3rd APPLICANT

FRANK JOHN NYALUS............................................4th APPLICANT

AND

THE ATTORNEY GENERAL......................................1st RESPONDENT

MINISTER FOR WORKS AND TRANSPORT........... 2nd RESPONDENT

PERMANENT SECRETARY MINISTRY OF WORKS AND TRANSPORT.................................... 3rd RESPONDENT

THE CLERK OF THE NATIONAL ASSEMBLY...........4th RESPONDENT
JUDGMENT

28th July, & 10th August, 2023
ISMAIL, J.

The Petitioners in this matter are a disgruntled quartet of citizens of Tanzania who are suing on an Intergovernmental Agreement (known in acronym as "IGA"), which has become the talk of the country for the past two months. This is an agreement executed between the United Republic of
Tanzania ("URT"), on one part, and the Emirate of Dubai ("Dubai"), on the other ("State Parties"), on 25th October, 2022. The subject matter of the Agreement is the economic and social partnership for the development and
improvement of performance of sea and lake ports in Tanzania.
The preambular part of the IGA reveals that its signing was in
furtherance of a major step which entailed execution of a Memorandum of Understanding ("MoU"), between Tanzania Ports Authority ("TPA") and DP World ("DPW"), a Dubai based state owned enterprise, signed on 28th

Page 3

February, 2022, on the sidelines of the Dubai Expo, which was attended by Her Excellency Samia Suluhu Hassan, the President of the United Republic of Tanzania. The MoU signaled the intention to cooperate and singled out areas of cooperation between TPA and DPW "for development and/or
improvement of the operations and management of strategic ports
infrastructure of Tanzania Sea and lake ports, special economic zones,logistic parks and trade corridors...."Subsequent to execution of the IGA, the ratification process on theTanzanian side began in earnest. This process was in pursuance of Article 25 (2) of the IGA which entailed tabling it in Parliament where it was debated
and ratified on 10th June, 2023. The debate on the floor of the Parliament was reportedly preceded by issuance of a notice to the public, for solicitation of opinions on the draft parliamentary resolution that was to be debated and
passed as a prelude to the ratification of the IGA. While the notice was issued on 5th June, 2023, public hearing was scheduled for 6th June, 2023. In the end, the IGA was given a resounding nod by a majority of Members of
Parliament in attendance on the day.

Execution of the IGA and the eventual ratification has elicited an
emotive discussion that has polarized the country, with a section of the population feeling that the IGA is flawed in many ways, and that it should

page 4

not be allowed to see the light of the day. Those who have found faults in the IGA include the petitioners. The quartet has come up with a raft of allegations which attempt to poke deep holes in the entire chain of the process that birthed the IGA and its eventual ratification. The blemishes are
thrown at Minister for Works and Transport; the Ministry's Permanent Secretary; and the Clerk to the National Assembly. The Attorney General is impleaded as a necessary party whose presence in the proceedings is, by law, indispensable. Through a petition, preferred by way of originating
summons, that is supported by the petitioners' affidavit, four grounds have been raised as the basis for their unreserved denunciation of the IGA. Thesegrounds are as reproduced hereunder:

1. That, the respondent's (sic) action of signing the International
Agreement (IGA) and tabling the same before the Parliament of the United Republic of Tanzania for ratification without a dully (sic)
notice to the public or making the same available to the general
member (sic) and without availing the member (sic) of public a
reasonable time to participate and give their opinion as required by law and the subsequent ratification of the same by the Parliament of the United Republic of Tanzania was given, submitted and givenratified in the ought (sic) right contravention of the provisions ofsection 11 (1) and (2) of the Natural Wealth and Resources
(Permanent Sovereignty) Act No. 5 of 2017 read together with
section 5 (1), 6 (2) (a), (b), (e) and (i) of the Natural Wealth and

page 5

Resources Contracts (Review and ReNegotiation of UnconscionableTerms Terms) Act No. 6 of 2017;

2. That, the Intergovernmental Agreement between the United
Republic of Tanzania and the Emirate of Dubai signed by the second respondent and witnessed by the third respondent by virtue of
articles 2 (1), 4 (2), 5 (1), 6 (2), 7 (2), 8(1) (a), (b) (c), 8 (2), 10
(1), 20 (2) (a), (e) (i) and (ii), Article 18, 21, Article 23 (1), (3) and
(4), articles 26, 27 and 30 (2) of the international agreement
contravene the laws and the Constitution of the United Republic of Tanzania;

3. That, by the acts and conduct of the 2nd and 3rd respondents, and circumstances of this case the respondents did not only violate the express provision of the law but exposed the important natural resource to wit ports and other strategic infrastructure in a lousy agreement full of uncertainty contrary to the interest of the Public;and

4. That, Respondent's action of signing the Intergovernmental
Agreement between the United Republic of Tanzania and the
Emirate of Dubai while there are terms which endanger not only
sovereignty but also security of our country as referred under
Articles 7 (2), 23 (4) of the signed and ratified contract.

The supporting affidavit, jointly sworn by the petitioners has laid
grounds on which the prayers sought in the originating summons are

page 6

premised. In general terms, the affidavit has taken a swipe at the process that culminated in the signing and ratification of the IGA; the danger that it poses to national security and sovereignty of the country in the control and
management of her natural resources as enshrined in the Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 ("the Constitution" or "URT Constitution") and Acts No. 5 and 6 of 2017. Of specific relevance in the petitioners' deposition are paragraphs 12, 13, 14, 15 and 16 of the said affidavit, whose substance is reproduced hereunder, with all their grammatical challenges:

12. That, the granting ofsuch tender to DWP for Emirate of Dubai is
discriminatory and in contravention of the laws of Public
Procurement Regulatory Authority Acts (PPPR) Cap 410 of 2011
as amended and other relevant laws as amended time to time.

13. That, the respondents' acts and conducts has;

(a) Undermined Sovereignty and Security of the United Republic of Tanzania in respect of its power to own manage and control its natural resources for the interest
of the United Republic of Tanzania;

(b) Infringed the Rights of the Member of the Public to participate in a meaningful discussion in respect of the Intergovernmental Agreement subject of this Petition;


page 7

(c) That the deliberate act of the 2nd Respondent to table the
Intergovernmental agreement without adhering to the due
process of law breached the provisions of the constitution,
rule oflaw, good governance and respect of the nation and
utilization of her natural resources.

14. That as the Intergovernmental Agreement subject of this
application touches issue of natural resources the respondent
ought to have complied with compulsory requirements of the law to make the agreement available for public scrutiny.

15. That, acts, conducts and circumstances of the 2nd and 3d
respondents would lead to anarchy in the administration of
harbor and ports and all other strategic economic zone subject
of the Intergovernmental Agreement and that there is no
administrative mechanism or organ in and outside the National
Assembly with power and authority to control or review, make
good the situation and return to the constitution and law.

16. That, on lCfh June 2023 the Parliament of the United Republic of Tanzania illegally and arbitrary ratified the aforesaid the
intergovernmental agreement between United Republic of
Tanzania and the Emirate of Dubai while the said agreement was
in violation ofthe Constitution of the United Republic of Tanzania
and other laws of the United Republic of Tanzania.
The respondents have fielded a ferocious opposition to the petition.
This was done through a reply to the originating summons and counter-


page 8

..........

Page 91

In the upshot of all this we find this, petition barren of fruits.
Accordingly, the same is hereby dismissed. Since this is a public interest matter, we do not find any justification for granting of costs. We, therefore, make no order as to costs.

Order accordingly.

DATED at MBEYA this 10th August, 2023.

DUNSTAN B. NDUNGURU
JUDGE
10/08/2023

MUSTAFA K. ISMAIL
JUDGE
10/08/2023

ABDI S. KAGOMBA
JUDGE
10/08/2023
Page 91

Endelea kusoma kurasa zone 91 za judgement hii : source :
 
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imebariki mkataba uwekezaji bandarini na kusema ni halali na kwamba malalamiko yaliyowasilishwa na Wakili Mwabukusi hayana mashiko.

Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo leo Alhamisi Agosti 10, 2023 na kubariki mkataba wa IGA kuwa ni halali

Uamuzi huo umetolewa katika kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii Kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA).

Baada ya uamuzi wa Mahakama kuhusu uhalali wa mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuwa sahihi na haujakiuka utaratibu, walalamikaji katika kesi hiyo wamesema wanajipanga kukata rufaa kuupinga uamuzi huo.

Alphonce Lusako ambaye ni mlalamikaji wa kwanza katika kesi hiyo iliyotolewa uamuzi leo Alhamisi Agosti 10, 2023 amesema; β€œTumesikia kigugumizi cha Mahakama, tumeshamwelekeza wakili wetu tutakata rufaa na tutawasilisha leo hii notisi ya kukata rufaa,”amesema.

Wakili aliyesimamia upande wa walalamikaji katika kesi hiyo, Boniphace Mwabukusi amesema wanatoa siku 14 Serikali kubadili mkataba huo.

β€œKwa kuwa Mahakama imesema haina mamlaka ya kuingilia shughuli za Bunge sasa sisi tunakwenda kutumia Civil Bunge (Bunge la Wananchi) tutatoa siku 14 wabadiki mkataba huu,”amesema.

Mwabukusi ameongeza kuwa wanajipanga kwenda Mahakama ya Rufani.
 
Watanzania bhana watu wa ajabu sana! Watu wameenda mahakamani wakiamini huko ndiko kuna haki, lakini hukumu ikitoka wasivyotaka wao wanasema majaji hawafai. sasa ulitaka Jaji atoe hukumu kwa kufata hisia au kwa kufata sheria?

Waliotoa hukumu wameusoma mkataba vema na sheria pia wamezisoma. Sisi tunaopinga hatujasoma hata kifungu kimoja cha huo mkataba na sheria zenyewe hatuzijui zaidi ya kufata mkumbo tu!
 


Breaking News:​

Mahakama Mbeya yatupilia mbali kesi ya Bandari walalamikaji kukata rufaa​

d2dcd05a-5648-4a28-a656-735d5d587e67.jpg

Humphery Mgonja
BBC Field Producer
View attachment 2713456
BBCCopyright: BBC
Mahakama Kuu nchini Tanzania hii leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inapinga mkataba (IGA) wa uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na falme ya Dubai.
Kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba.
Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.
 
Tunakumbushana tu leo ndio tarehe 10/08/2023

Mungu wa mbinguni atubariki Sote, Amen


===

Sasa ni 09:00 Asubuhi ukumbi wa kwanza umejaa na ukumbi wa pili umejaa na bado kuna idadi kubwa ya watu nje waliendelea kuingia.

Leo majaji wa kesi hii wataandika historia ya maamuzi yao kwa vyovyote watakavyoamua.

Majaji wote watatu wameingia muda huu saa 3:42.

MAJAJI WA KESI HII
  • Mhe. Ndunguru
  • Mhe. Ismail
  • Mhe. Kagomba
Wakili wa serikali anatambulisha mawakili wa pande zote mbili. Na wote wako tayari kupokea hukumu.

Mahakama imetulia kwa ukimya mkuu. Majaji wanazungumza kidogo, Mhe. Ismail na Ndunguru. Kisha, Jaji Kagomba na Ndunguru pia wanazungumza kidogo. Wanaendelea kuandika.Karani wa Mahakama leo ni MAPUNDA.

Majaji wanasema wako tayari kusoma hukumu na kwamba itasomwa kwa kiswahili.

Jaji Ndunguru anaanza kusoma hukumu.

HUKUMU YA MAHAKAMA
Katika lalamiko hili waleta maombi wanne ni raia wa Tanzania wameleta maombi haya dhidi ya Mkataba wa TZ na Emirati ya Dubai.

Jaji Ndunguru: Mkataba huo uliingiwa mwaka 2022 na sehemu ya utangulizi wa Mkataba huo unarejea M.O.U iliyosaiwa tarehe 25/2/2022 wakati wa Maonyesho ya Dubai yaliyosainiwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania.

Jaji Ndunguru; Baada ya kusainiwa Mkataba huo hatua za kuridhia mkataba huo hapa Tanzania ulianza kwa mujibu wa Ibara ya 25 ya Mkataba huo.Bunge lilitoa taarifa kwa umma tarehe 5 Juni, 2023 na kuelekeza maoni yangepokelewa tarehe 6 Juni, 2023.

Jaji Ndunguru: Kusainiwa kwa Mkataba huo kumezua mgawanyiko mkubwa kimtazamo, na watu wengi wakisema mkataba huo una dosari na kwamba haukustahili kuwepo.

Jaji Ndunguru; Wanaolalamikiwa ni Waziri wa Ujenzi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Katibu wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anapaswa kuunganishwa katika mashtaka yanayohusu Serikali.

Jaji Ndunguru: Malalamiko hayo yameletwa katika misingi minne.Misingi hiyo ni pamoja na kwamba IGA ibara zake kadhaa kama zilivyotajwa katika Hati ya Mashtaka, kwamba zinakiuka sheria na Katiba ya Tanzania.

Jaji Ndunguru: Kiapo cha pamoja cha Waleta Maombi kiliunga mkono maombi yaliyowekwa katika Hati ya Malalamiko.Kwa ujumla Kiapo hicho kimelalamikia Mchakato mzima wa Upatikanaji wa Mkataba huo na mwenendo wa Bunge juu ya uvunjifu wa Sheria za nchi.

Jaji Ndunguru: Wajibu maombi walijibu mashtaka hayo kwa kiapo cha watu wawili, MOHAMED SALUM na MARIAM ambaye ni Mwanasheria kutoka Bungeni.

Jaji Ndunguru: Wajibu Maombi wamejibu kwamba mambo yanayolalamikiwa hayana msingi, na kwamba sheria na Katiba zimezingatiwa na masuala ya Usalama yametazamwa kikamilifu katika mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Wajibu Maombi wameeleza kwamba Bunge lilitoa taarifa kwa umma ili kupata maoni, na wamesema kwamba watu 72 walijitokeza kutoa maombi. Shauri hilo lilisikilizwa kwa njia ya mdomo, mawakili wa pande zote mbili wakiwakilisha wadaawa.

Jaji Ndunguru: Kabla ya kuanza usililizwaji huo, Mawakili wa pande zote mbili waliunda kwanza viini vya kuamuliwa (Issues) pamoja na kiini kimoja ambacho kiliongezwa na Mahakama.

Jaji Ndunguru: Viini hivyo ni pamoja na kuhoji iwapo Ibara kadhaa ya IGA zinakiuka Ubara ya 1, 8, 28(1)(3) za Katiba ya Tanzania.Pia, kiini kingine kilihoji iwapo IGA ni mkataba.

Jaji Ndunguru: Kiini cha kingine kilihoji iwapo Mkataba wa IGA ulifuata taratibu za uteuzi wa Mzabuni katika kuzingatia sheria ya Manunuzi ya Umma.Hoja zote muhimu zilizingatiwa na Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hata hivyo, kabla ya kutoa umauzi Mahakama inapenda kuwashukuru Mawakili wa pande zote mbili kwa kufanya kazi yao nzuri na kusaidia kutupatia Mahakama maarifa na uelekeo mzuri katika kutoa uamuzi.

Jaji Ndunguru: Ukiachia kiini cha tatu, viini vingine vyote havijajielekeza katika uvunjifu wa Katiba.Hata hivyo, kiu ya Watanzania inajikita kupata majibu kwa viini vyote vilivyoletwa mbele ya Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hata hivyo, kiu ya Watanzania inajikita kupata majibu kwa viini vyote vilivyoletwa mbele ya Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hii ni kwa sababu kila shauri linapaswa kuamuliwa kwa kuzingatia mazingira yake, na pia kwa kuzingatia ibara ya 107A (2)(e) kwamba Mahakama inapotoa uamuzi na haki isifungwe na mambo ya kiufundi.

Jaji Ndunguru: Kwa kuanzia na Kiini cha tano, Walalamikaji wanasema IGA haijakidhi vigezo vya kuwa mkataba kwani hakuna consideration na mambo mengine chini ya Sheria za Mikataba hapa nchini.

Jaji Ndunguru: Mawakili wa Wajibu Maombi wao walijibu kwamba, IGA sio mkataba wa kawaida bali ni makubaliano ya upeo tu, sisi Mahakama tunakubaliana na hoja hiyo.

Jaji Ndunguru: Kuhusu hoja kwamba Emirati ya Dubai sio dola, tumepitia Montevideo Convention, tumeona Emirati ya Dubai inakidhi vigezo vingine lakini tunapata mashaka kuhusu uwezo wa Emirati hiyo kuingia kwenye mikataba ya kimataifa.

Jaji Ndunguru: Mawakili wa Waleta Maombi hawakutuelezea kama Emirati ya Dubai imezuiwa kuingia katika mkataba wa kimataifa.Ni maoni yetu kwamba, katika IGA kila upande ulikuwa na uwezo wa kuingia katika mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Hivyo ni maoni yetu kuwa IGA ni mkataba wa Kimataifa hausimamiwi na Sheria za Mikataba za Tanzania.Kuhusu kiini kwamba Mchakato wa IGA ulikiuka sheria za Manunuzi.

Jaji Ndunguru; Ni mtazamo wetu kwamba, Waleta maombi hawakujielekeza vyema katika sheria za kimataifa ambazo zinakataza kutumiwa kwa sheria za ndani katika mikataba ya kimataifa.

Jaji Ndunguru: Mahakama haijaridhishwa na hoja ya Waleta maombi kwamba Sheria ya Manunuzi ya Umma haikuzingatiwa katika kupima uhalali wa IGA.Kuhusu kiini cha kupima iwapo Umma ulipata muda wa kutosha kupata maoni kwa umma.

Jaji Ndunguru: Kukosekana kwa Viambatanisho muhimu kama Mkataba wa IGA katika Tangazo hilo, na kutokea kwa watu 72 tu, ndiyo hoja ya Waleta Maombi.

Jaji Ndunguru: Wajibu maombi wamejenga hoja kwamba suala hilo ni la ndani ya Bunge.Mahakama inatambua kuwa Ibara ya 63(3)(e) na Kanuni ya 108(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Jaji Ndunguru: Baada ya kupitia hoja za pande zote, tunakubaliana na hoja za wajibu maombi kwamba Bunge halitakiwi kuingiliwa katika majukumu yake.

Jaji Ndunguru: Msimamo huu umeelekezwa pia na Wasomi mbalimbali kuhusu masuala ya Bunge, akiwemo Pius Msekwa.Licha ya dosari inayoonekana katika ushirikishwaji wa umma kutoa maoni, hata hivyo tunajizuia kufanya uamuzi wa kiasi cha kubatilisha mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Malalamiko makubwa katika Kiini cha mwisho, ni juu ya kuanzisha mchakato wa kuanzisha mahakama za nje katika migogoro ya rasilimali.

Jaji Ndunguru: Tunakubaliana na hoja ya Waleta Maombi, kwamba ibara za IGA imevunja sheria za ulinzi wa Rasilimali, kwa kupeleka migogoro nje ya nchi. Hata hivyo, dosari hiyo haitatumika kuutangaza IGA kuwa ni batili.

Jaji Ndunguru: Uandishi bora wa vifungu vya IGA unaweza kurekebisha Vifungu hivyo na kuondoa dosari hii.Tunashangaa kwamba IGA itaongozwa na sheria za nchi, na mikataba ya miradi itaongozwa na sheria za ndani lakini migogoro yake itatatuliwa nje ya nchi.

Jaji Ndunguru: Kwa hoja tajwa hapo juu mahakama hii inatupilia mbali hoja za waleta maombi. Anamaliza kusoma hukumu hiyo .Watu wanasimama majaji wanatoka.
Kwa kilatini Tunasemaga β€˜locuta causa finita β€˜
 
Back
Top Bottom