Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Wengi katika mkoa wa Songwe wako ndani kwa kesiza kusingiziwa, ilimradi walijihusisha na vyama vya upinzani. Walitakiwa yule Rc na Rpc watupwe ndani kwa kutumia madaraka yao vibaya huku matumbo yao yakijazwa na Kodi za wananchi!!,Tupa ndani wote!!
 
Amtukane nani wakati dhalimu hayupo? Tatizo lake lilikuwa ni yule rais muovu, na muovu hayupo na uovu sasa umepungua, baada ya muovu kuelekea kuzimu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Si ndio maana kila siku huwa nasema sasa tuko vizuri,?

Mambo ni super, hata Mbowe sasa atabatilisha lile wazo la kwamba hamtashiriki uchaguzi maana mambo ni bam bam, mbaya wenu hayupo!

Hata mdude hutaona akitukana mtu tena maana mambo ni safi sana!
 
Hahaa!!!!!chama chakavu ni wapigania tumbo tu
Umoja ni kitu muhimu sana na kipekee niwapongeze Bavicha na Chadema kwa ujumla kwa namna walivyompigania Mdude Nyagali mwanzo mwisho na leo yuko huru.

Nategemea UVCCM na CCM kwa ujumla mtaiga " roho ya Upendo " kutoka kwa wenzenu wa Chadema ili mumpiganie komredi Ole Sabaya aliyeko magereza au Lupango.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Angehukumiwa kwenda Gerezani basi muda huu Hakim angekuwa anajadiliwa vikali lakin Kwa kuwa kaachiwa huru hakuna hata anayefaham jina la hakimu. Tatizo CDM wanapenda sana kuonewa huruma

Cdm hawahitaji huruma ya mtu yoyote, bali wanahitaji haki tu. Yoyote asiyetenda wakati analipwa ili atoe haki ni adui yao mkubwa.
 
masikini mataga pori roho imewauwa mmeumbuka [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Tumeumbukaje?

Waliompeleka kumshikisha adabu ni ccm na waliomtoa ni ccm baada ya kuona kabadirika.

Au wewe unaona kuna mfumo mwingine ndani ya hii nchi?
 
Leo Juni 28, 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuachia huru Mdude Nyagali baada ya kutomkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kusafirisha madawa ya kulevya.

Mpaluka Mdude Nyagali alikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin gramu 23.4 mwaka 2020.

Mdude ni Mwanaharakati na Mwanachama wa CHADEMA ambaye alitumia muda mwingi kuikosoa Serikali ya Awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati John Magufuli. Mdude anajitambulisha kama mpiganiaji uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuwepo mdahalo wa kisiasa.

Pia soma
- Mbeya: Mpaluka Nyagali Mdude akamatwa na Heroine, apandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya Uhujumu Uchumi

ASANTE MUNGU KWA KUTUONDOLEA SHETANI NA KUTULETEA MALAIKA
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta
Pia ni aibu kwa mwendazake na waliokuwa wanamsifia, hapa ndio nimeamini mama alishawahi kutaka kujiuzuru
 
Sifa na utukufu ni kwa Mungu alieamua kutuondolea yule dhalimu
 
Leo Juni 28, 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuachia huru Mdude Nyagali baada ya kutomkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kusafirisha madawa ya kulevya.

Mpaluka Mdude Nyagali alikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin gramu 23.4 mwaka 2020.

Mdude ni Mwanaharakati na Mwanachama wa CHADEMA ambaye alitumia muda mwingi kuikosoa Serikali ya Awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati John Magufuli. Mdude anajitambulisha kama mpiganiaji uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuwepo mdahalo wa kisiasa.

Pia soma
- Mbeya: Mpaluka Nyagali Mdude akamatwa na Heroine, apandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya Uhujumu Uchumi

Kijana umepambana vya kutosha Mungu akubariki sana na kukutetea, umeendesha mapambano hadi haki imepatikana
 
Kwa mara ya kwanza nasikia mtuhumiwa wa Madawa ya kulevya anaachiwa huru kiroho safi.

Huu ushahidi kuwa sio wote wanaofungwa ni wakosaji kwa hizo kesi walizotuhumiwa.
 
Nasema hivi. Huko kuzimu kama kuna jela basi jiwe atakua anatumikia kifungo cha maisha
 
Back
Top Bottom