Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Asanteni sana ndugu Watanzania kwa kusimama na mimi mpaka nimeachiwa.

Sina cha kuwalipa zaidi ya kusema asanteni sana.

Mapambano yaendee...

Kwa jamiiforums hii ndio account yangu na muda si mrefu itakua verified.
 
Leo Juni 28, 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuachia huru Mdude Nyagali baada ya kutomkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kusafirisha madawa ya kulevya.

Mpaluka Mdude Nyagali alikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin gramu 23.4 mwaka 2020.

Mdude ni Mwanaharakati na Mwanachama wa CHADEMA ambaye alitumia muda mwingi kuikosoa Serikali ya Awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati John Magufuli. Mdude anajitambulisha kama mpiganiaji uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuwepo mdahalo wa kisiasa.

Pia soma
- Mbeya: Mpaluka Nyagali Mdude akamatwa na Heroine, apandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya Uhujumu Uchumi

Siku ya leo ni siku ya Ukombozi kwa waliofungwa. Mungu wa Mbinguni alinuliwe milele amina.
 
Namna alivyoiwasilisha utadhani ni Wapigania uhuru wa zamani kama Kwame Nkrumah au Nelson Mandela , ama labda unaweza kudhani ni Mmarekani Mweusi Martin Luther , Hakika huyu kijana anacho kipawa fulani ndani yake , hebu Msikilize mwenyewe

View attachment 1833730
Tuwekee kwa maandishi mkuu, maandishi yanadumu sana hapa jukwaani ili tuweke kumbukumbu
 
Namna alivyoiwasilisha utadhani ni Wapigania uhuru wa zamani kama Kwame Nkrumah au Nelson Mandela , ama labda unaweza kudhani ni Mmarekani Mweusi Martin Luther , Hakika huyu kijana anacho kipawa fulani ndani yake , hebu Msikilize mwenyewe

View attachment 1833730
Mwenye haki anastawi milele na milele.

Bwana wa Majeshi ametenda miujiza.
 
Back
Top Bottom